Uhusiano wa Intelijensia na watu kama kina James Bond

Uhusiano wa Intelijensia na watu kama kina James Bond

Mbombongafu! Duu kama ndio hivi, tanzania hamna hicho kitu au ndio wale wanaoshinda wanacheza pool pale break point, wenyewe wanajihita wazee wa geti jeusi!
 
TISS nao ni binadamu kama sisi hata wakiwa na mafunzo mazuri sana lakini wakiachwa na njaa ule moyo wa kazi unapungua. Tunawafamu baadhi mbona ni njaa kali tu kama sisi, hivyo ni rahisi kununuliwa na mafisadi wa EPA na mengineyo.

kiasi kikubwa umenijibia swali la ndugu yangu! tatizo ni hapo hapo nilipo hailaiti!! na moyo wa kazi ukifa na wakaamua kufanyia kazi ule upande mwingine hapo ni hatari!!
 
Nani kakwambia hatuna ghosts? Waliomtesa dr. Uli wasingekuwa ghosts wangesha patikana.
Wacha kujidanganya wewe, hao wanaotakiwa wawakamate si ndo haohao wenyewe!?
Ikiwa mtu kama Saeed Kubenea anawajua, itakua polisi? Hakuna ghost hapa Tanzania!!
 
TISS ni kama kampuni ya ulinzi tu,, hufanya kazi kwenye pesa na sio kwenye HAKI au UZALENDO
 
Wapo mkuu, tena wamefundwa zaidi ya uonapo movie hizo!

Unapoona tukio lolote la kifisadi au vyovyote vile limewafikia Chadema au mbunge yeyote jua kuwa limetokea TISS!

Hakuna kitu ndani ya nchi hii kinachoweza kutokea bila TISS kujua!

Tatizo ni watawala, TISS wakishamaliza uchunguzi unaoonyesha kuwa kuna tukio linakuja au lipo wao hupeleka file mahali husika huko ndiko hupewa amri na maelekezo ya nini wafanye!

Jidanganye kuwa hawapo ulijua jiji mkuu!

Tanzania ndio nchi inayoongoza kwakuwa na Usalama wa Taifa imara kuliko nchi yoyote Afrika!

Sikubaliani na wewe coz kuna mambo mengi yametendeka bila TISS kujua
 
una hakika gani kama kuna mambo mengi yametendeka bila TISS kujua? tukubali tu kwamba corruption na kutowajibika kwa viongozi wenye mamlaka ya kutoa maamuzi imeharibu kila jema tulilotegemea kuliona nchi hii. naamini TISS wanafanya kazi nzuri tu lakini inafika mahali wao kama wao sio waamuzi wa kile walichofanyia kazi, watalipeleka jambo au ripoti katika taasisi husika then inapokuja suala la kufanyia kazi kile kilicholetwa mezani, kizungumkuti kinaanza. Sina uelewa halisi wa utendaji kazi wa TISS lakini laiti kama ikiwa ni mamlaka inayojitegemea bila kuingiliwa na mfumo uliopo na siasa za nchi hii nadhani ingeongeza tija. lakini kwa sasa ni ile kesi ya ngedere unampelekea Nyani. Naamini yapo mambo yanayohusu usalama wa hili taifa yanafanyiwa kazi vizuri kabisa bila sisi kujua lakini pia yapo mambo ambayo hata mtu wa kawaida inafika muda anajiuliza hii nchi yetu usalama wa taifa wapo kweli? hivyo kwa mimi nadhani ni mfumo tu unatakiwa kubadilika na wahusika katika kutolea maamuzi kazi inayofanywa na ndugu zetu wa TISS kuwa wazalendo.
Sikubaliani na wewe coz kuna mambo mengi yametendeka bila TISS kujua
 
tiss yetu bado sana,ikiwa kama mtu ni intelejensia unagundua kitu hatarishi cha usalama wa taifa kisha unapeleka sehemu husika,file halifanyiwa kazi,mimi naona ni ukosefu wa akili na uzalendo,kama if this people are real intelegence wangeondea huo mfumo unaokwamisha kazi za akili yao,ila kinachoonekana wanasiasa ndio wamekua more intelegence than tiss
 
je hao wamakala wao wamefanya nini kudhibiti ufasadi katika ardhi za vijiji zinazovamiwa na wawekezaji wababaishaji?
Tiss hana nguvu tena kama zamani,

na tumisikia wapo kila taasisi na mashirika ya umma, je walisaidiaje taifa hili katika uvumbua ubadhirifu, wizi, ufisadi, na ughaidi ? Hakuna kitu!

Wazo binafsi

1. Tiss iwe taasisi independent, yaani isiwe chini ya ofisi ya rais.
2.tiss ipewe mamlaka ya kukamata,kuhoji, kuweka kizuizini yeyote kwa maslahi na usalama wa taifa,
3. Tiss ipadilishwe jina iitwe tisa, yaani tanzania intelegence and security authority, kwa kiswahili, mamlaka ya intelejensia na usalama ya tanzania.
4. Kuwe na vitengo vikuu viwili yaani intelegence na security.

List itaendelea baadaee...

usichokijua ni sawa na usiku wa giza
 
tiss yetu bado sana,ikiwa kama mtu ni intelejensia unagundua kitu hatarishi cha usalama wa taifa kisha unapeleka sehemu husika,file halifanyiwa kazi,mimi naona ni ukosefu wa akili na uzalendo,kama if this people are real intelegence wangeondea huo mfumo unaokwamisha kazi za akili yao,ila kinachoonekana wanasiasa ndio wamekua more intelegence than tiss

Tatizo sio ukosefu wa akili mkuu, akili wanazo sana tu labda wawe wanajitoa hizo akili but tatizo kubwa ni uzalendo na discipline ya kazi hasa kwa ngazi za juu. sina tatizo kabisa na hawa watendaji wa kawaida but issue inapofika kwamba taarifa tumezipata na tunazo mezani kwa ajili ya utekelezaji au maamuzi zinafunikwa kiaina aina. Na hii inatokana na kuingiza siasa kwenye mambo ambayo yanahusu hata usalama wa nchi. kila ukigeuka ni siasa mpaka sehemu ambazo ilitakiwa siasa kuwekwa pembeni na kuangalia maslahi ya nchi. Kila siku ninaangalia hii nchi ya Rwanda na jinsi walivyo serious na mambo yao, very soon watapiga hatua ya ajabu sisi tumekaa kuzozana na mikataba mibovu ya madini, ufisadi na rushwa afu hakuna kinachofanyika chenye kuleta impact. Yaani hata hili la uhujumu uchumi, pesa kibao zimefichwa nje afu linageuzwa geuzwa kuwa jambo la kisiasa tu afu linaachwa juu kwa juu. I wish ningekuwa rais wa nchi hii................
 
Sikubaliani na wewe coz kuna mambo mengi yametendeka bila TISS kujua

TISS wanajua kila kitu uenda na wao wameshiriki ktk huo wizi,msikilize Yericko Nyerere anasemaje!!! Ila ndio hvo tiss kama kampuni ya ulinzi vile(nimenukuu mdau wa juu hapo)
 
Last edited by a moderator:
Sasa kama walishindwa kimchomoa roho Dokta kuna kitu kweli hapo tena na live tracing? na wakajulikana...ubwabwa huo bila chumvi.
 
Sasa kama walishindwa kimchomoa roho Dokta kuna kitu kweli hapo tena na live tracing? na wakajulikana...ubwabwa huo bila chumvi.

Kuna dereva taxi mmoja alikodiwa na majambazi na baada ya muda mfupi akawekwa chini ya himaya yao na kuambiwa atekeleze kila alichoambiwa. akaanza kupokea amri, endesha gari kuelekea sehemu fulani, akafanya!! lakini ikatokea wako katika foleni, alichofanya ni kuligonga gari la mbele kwa makusudi akijua watashuka kumuuliza kwanini kawagonga na vile kulikua na watu wengi basi kweli watu wakaanza kuja. Majambazi wale taratibu wakashuka na kuondoka mpaka dereva alipokuja kujieleza kilichokua kimemsibu ndio watu wakapata picha ya kilichokua kinaendelea. Sio kwamba dereva alikua mzembe, bali hakuwa huru kwa alichokua anakifanya. Nachotaka kusema hapa, si kila jambo liko katika picha uionayo wewe. mambo mengine yanakua na mafumbo makubwa ndani yake. Sijui kama umepata point yangu.
 
Mimi nimeshawahi kuwa mjeshi kitengo cha mil int pale ngome. Naisifia tiss kwa sababu imeweza kufanya kazi zake bila watu kujua undani wake ingawa ipo kwa miaka zaidi ya 51. Hiyo inaonesha umakini wao katika kazi zao. Kinachojulikana ni kile kinachotakiwa watu wakifahamu na ndicho kinachojadiliwa humu kikidhaniwa ndo issue. Ndo maana nasema usichokijua ni sawa na usiku wa giza. Mimi nimefanya nao kazi za kufa mtu lakini siwezi sema kwani inahuuuu.
 
Hapa ndugu zanguni ubavu sina napita zangu manake mnaposema milango ya nyumba iko wazi ni kwamba mnataka tukose usingizi
 
Wapo mkuu, tena wamefundwa zaidi ya uonapo movie hizo!

Unapoona tukio lolote la kifisadi au vyovyote vile limewafikia Chadema au mbunge yeyote jua kuwa limetokea TISS!

Hakuna kitu ndani ya nchi hii kinachoweza kutokea bila TISS kujua!

Tatizo ni watawala, TISS wakishamaliza uchunguzi unaoonyesha kuwa kuna tukio linakuja au lipo wao hupeleka file mahali husika huko ndiko hupewa amri na maelekezo ya nini wafanye!

Jidanganye kuwa hawapo ulijua jiji mkuu!

Tanzania ndio nchi inayoongoza kwakuwa na Usalama wa Taifa imara kuliko nchi yoyote Afrika!

hivi hizi taarifa za Tanzania ina jeshi bora na usalama wa taifa bora kuliko wote Africa Mnatoa wapi? kuna assessments kama za forbes zinafanyika? muwe mnatupa na sources wakuu.
 
Wapo mkuu, tena wamefundwa zaidi ya uonapo movie hizo!

Unapoona tukio lolote la kifisadi au vyovyote vile limewafikia Chadema au mbunge yeyote jua kuwa limetokea TISS!

Hakuna kitu ndani ya nchi hii kinachoweza kutokea bila TISS kujua!

Tatizo ni watawala, TISS wakishamaliza uchunguzi unaoonyesha kuwa kuna tukio linakuja au lipo wao hupeleka file mahali husika huko ndiko hupewa amri na maelekezo ya nini wafanye!

Jidanganye kuwa hawapo ulijua jiji mkuu!

Tanzania ndio nchi inayoongoza kwakuwa na Usalama wa Taifa imara kuliko nchi yoyote Afrika!

...Acha kujipa Matumaini Hewa Mkuu! Labda ilikuwa Zamani, Sio Sasa ambapo Mchangiaji mmoja amesema gapo ju Kuwa Mama mpaka mjukuu wanaweza wote kuwa huko...!
 
Back
Top Bottom