Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Andiko lako Lina vingi ambavyo ninatakiwa nikujibu na kuweka sawa ila nakupa msingi mmoja wa Uwezo .

Ibada nyingi za Kiislamu inazingatia uwezo maana mtu isipokuwa na uwezo uwajibu unaondoka au unawepesishiwa mfano kama hauna uwezo wa kwenda kuhiji basi hakuna lawama juu yako.

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume Makkah Uislamu ilipokuwa hauna nguvu Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina.
Unajizungusha zungusha na kukwepa navyo kuuliza.

Muhammad alipigana hivi vita kwa nini ?
•Uhud
•Badr
•Khaibar
•Muta
•Mecca
•Tabuk
 
Tokea enzi tawala za Kifalme mtu amabaye ana hatari kubwa ya kupandikiza chuki , Fitna na ushawishi haubakishwi unafyekwa mapema maana nchi haziwezi kuingia kwenye hatari kwa kulea kumbe mmoja tu.

Twende Suala la Saudi Arabia :

Hii inchi inaongoza kwa kuwekeza kwenye Elimu ya mafundisho sahihi ya Uislamu ndio maana hukuti vuguvugu za mapinduzi na kuutoa utawala kutoka kwa raia sababu Serikali ipo makini sana katika kuwekeza kwenye Elimu na kuwazima watu Wenye fikra potufu.

Ndio maana Leo Saudia pamoja na mapungufu yake mfano kusupport mambo ya entertainments haukuti raia wakiikosoa hadharani serikali Wala kutaka kuwapondia kwa sababu hizo , sababu suala Hilo ni jambo zito na Lina hukumu na Sheria zake
Labda ndio maana CCP China imeamua kuwatoa kafara Waislamu wa Uyghurs na Myanmar junta imeamua kuwatoa kafara Waislamu Rohingya.
 
Unajizungusha zungusha na kukwepa navyo kuuliza.

Muhammad alipigana hivi vita kwa nini ?
•Uhud
•Badr
•Khaibar
•Muta
•Mecca
•Tabuk
Elimu yako ndogo sana , nadhani soma kwanza historia maana isije kuwa napoteza muda tu.

Vita vyote vilipiganwa wakati Uislamu ni Dola kamili maana Ina Jeshi na utawala , sio kipindi Cha Makkah miaka ya mwanzo ya utume ambao hakukuwa na vita vyovyote sababu hawakuwa na uwezo wa kupambana sio dola , Jeshi Wala utawala .

Walivumia kila madhila na mateso na wakamcha Allaah hapo ndio unakuja msingi wa uwezo katika kufanya mambo.
 
Elimu yako ndogo sana , nadhani soma kwanza historia maana isije kuwa napoteza muda tu.

Vita vyote vilipiganwa wakati Uislamu ni Dola kamili maana Ina Jeshi na utawala , sio kipindi Cha Makkah miaka ya mwanzo ya utume ambao hakukuwa na vita vyovyote sababu hawakuwa na uwezo wa kupambana sio dola , Jeshi Wala utawala .

Walivumia kila madhila na mateso na wakamcha Allaah hapo ndio unakuja msingi wa uwezo katika kufanya mambo.
Swali ni hili lijibu habari ya mimi kuwa na elimu ndogo sio muhimu katika swali langu wewe mwenye elimu kubwa jibu maswali nayo kuuliza acha kujizungusha zungusha kama kichaa naona umeanza kujaa upepo wewe chawa wa sasha.

Muhammad alipigana hivi vita kwa nini ?
•Uhud
•Badr
•Khaibar
•Muta
•Mecca
•Tabuk
 
Bibi yangu hawezi kuingilia mambo yasiyo muhusu Wala kuwa na uwezo nayo ndio maana hawezi kutekwa.
Kwa sababu wewe na yeye hamna akili za kujadili mambo muhimu endelea kubishana Simba na Yanga sio kosa lako ni akili ulizo nazo.
 
Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu


Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969
Uo mfano wa nabii Musa auusiani kabisa na yanayoedelea Tanzania, Musa aliagizwa na MUNGU kuwatoa utumwani Wana wa Israel awaeudishe nyumbani , sasa "Tanzania ni yetu sote" hakuna mtumwa hapa we Kaa Kwa kutulia tu usikilizie kama unajiona upo salama no reform no election ⚒️ 💯
Hatuwezi kuwa kwenye nchi isiyo fata utawala wa Sheria , nchi imejaa uonevu na kutekana imekuwa katabia endelevu hapana kabisa "utekaji aukubaliki"
Tutakuwepo 😎
 
Swali ni hili lijibu habari ya mimi kuwa na elimu ndogo sio muhimu katika swali langu wewe mwenye elimu kubwa jibu maswali nayo kuuliza acha kujizungusha zungusha kama kichaa naona umeanza kujaa upepo wewe chawa wa sasha.

Muhammad alipigana hivi vita kwa nini ?
•Uhud
•Badr
•Khaibar
•Muta
•Mecca
•Tabuk
Kama kwenye Hilo andiko haujaona majibu basi tatizo sio Elimu pekee Baki hata akili ni Akilindogosana
 
Kwa sababu wewe na yeye hamna akili za kujadili mambo muhimu endelea kubishana Simba na Yanga sio kosa lako ni akili ulizo nazo.
Mimi sina muda wa kufuatilia upuuzi wa Simba na Yanga najishughulisha na Masomo bado natafuta Elimu ya dini na Dunia .

Kama wewe mwenye akili kidume mbona haujatoka front umeishiwa kuwa Keyboard Warrior ? Do some actions kama kutype nyuma ya kiboard hata mama Muuza Vitumbua anaweza

Soma huu Uzi wangu jinsi nilivyoponda mambo ya Simba na Yanga

 
Uislamu wa wapi unaotaka mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzuie la kulia ?
Mpalestina angetumia option Hii wakati akifikiria Kwa Kina option nyingine nzuri..Lakini akisema jino Kwa jino hio haiwezi yeye wala Iran.
 
Mkuu wakenya hawampendi Ruto.Walitaka mswada flani usipite lakini bunge likaupitisha,,vurugu ilikuwa kubwa na watu wakafa..ili kupata katiba mpya watu walikufa na baada ya kupata katiba mpya still watu wanakufa..Mi nadhani siasa ya afrika inataka ufumbuzi WA watu huru wasio wanasiasa.
Sio Kenya tu watu walikufa au wamewahi kufa katika mchakato wa kusimamisha utawala wa raia unaowajibika kwa raia, ilitokea hivyo Marekani pia 1775-1783 na kwenye civil rights movement 1950's na 1960's. Ilitokea hivyo pia Uingereza kikapatikana kitu inaitwa Magna Carta 1215 lakini utekelezaji wake ulikuwa shughuli pevu kwa muda mrefu sana mpaka ufalme ukakubali tu baadaye, Hiyo Magna Carta ndio msingi wa utawala wa sheria katika sehemu kubwa ya dunia ya leo hadi nchi yako unaosema watu wote ni sawa mbele ya sheria, mifano ni mingi.
 
Nakuuliza wewe unaona ni kipi bora kwa Palestine kupata nchi yao na kuondokana na uonevu wa miaka yote ya Israel kwa miaka zaidi ya 70 wafanye nini tofauti na kilichofanywa na kinachofanywa na Hamas ?

Nakukumbusha unapojibu swali hili kumbuka Gaza ni gereza la Israel kwa miaka na miaka na mashambulizi ya Hamas ya oktoba yalifanyika katika maeneo ya walowezi wa Israel.
Uwezo wa Allah ni zaidi ya haya unayoyafikiria. Mche Allah. Allah ndo mbadilisha mambo yasiyowezekana, muonesha njia pasipo na njia. Allah kwa mapana yake ni wakutegemewa.Ukweli wakutegemewa. Waeshimu viongozi wako kwani katika hilo akiwa hakuamrishi kuacha swala na mambo mengine wayatekeleza mtii mtawala Allah atawafedhehesha tu. Subrah ina matokeo na unishindi.
 
Uwezo wa Allah ni zaidi ya haya unayoyafikiria. Mche Allah. Allah ndo mbadilisha mambo yasiyowezekana, muonesha njia pasipo na njia. Allah kwa mapana yake ni wakutegemewa.Ukweli wakutegemewa. Waeshimu viongozi wako kwani katika hilo akiwa hakuamrishi kuacha swala na mambo mengine wayatekeleza mtii mtawala Allah atawafedhehesha tu. Subrah ina matokeo na unishindi.
Huyo Allah kama angekuwa na msaada angenza kuwasaidia watoto wa Gaza, watu wa Sudan na wanawake wa Afghanistan, angewasaidia Uyghurs na Rohingyas.
 
Waislam wengi duniani huwa reasoning yao ni ndogo sana.
Utaona mfano ambao hauna uhalisia , thread yako iko relevant kwa nchi ambazo zina utawala wa kifalme na mfanano wa hizo,
lakini kwa nchi za kidemokrasia hatuna watawala tuna serikali/ viongozi ambao wanapaswa kufanya kazi kwa matwaka ya wananchi.
Ndio maana wanatuomba ridhaa tuwachague.
Waislam wengi au "wapumbavu" wachache kama haka katoa mada?
Usijumuishe waislam wote kwa upotofu wa vipumbavu vichache kama katoa mada
 
Ajabu ya watu wenye upeo mdogo kama huyu mtoa mada ni kujiona wamesoma dini kwa kule kumezeshwa fikra za "kimadkhali" kuwa punda wa watawala ilhali dini iko mbali na kila aina ya ukondoo na upunda .. asichokijua ni kuwa uislam ni dini ya ukombozi na iko mbali na dhulma na uonevu
 
Unajizungusha zungusha na kukwepa navyo kuuliza.

Muhammad alipigana hivi vita kwa nini ?
•Uhud
•Badr
•Khaibar
•Muta
•Mecca
•Tabuk
Hakawezi kukuelezea hako ka kondoo ka "kimadhkali"
 
Nadhani watanzania tujue kuwa hii si nchi ya kidini, na haiendeshwi kwa misingi ya dini. Tumeamua wenyewe iwe nchi ya kidemokrasia lkn hatutaki misingi ya demokrasia. Kifupi watz tumekuwa vilaza maeneo hayo. Tunaendeshwa na utashi wa kiongozi aliyepo.
 
Back
Top Bottom