Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu


Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969
Kijana hongera umejitahidi kadri ya uwezo wako kuelimisha ummah ila watu hawatokuelewa kwa sasa ivi



Nb:Mtawala hadhihakiwi
 
Eti Fikra za kimadhali ! Wewe si unaelimu twende kwenye majadiliano ya kielimu hoja by hoja kwa dalili bila kukimbia .

Mimi natetea hoja kutokana na dalili halafu wewe unaleta fikra zako ? hii ndio shida ya MaKhwawarij na watu wenye Elimu na upeo mdogo wa Dini.

Haya jibu swali fupi Je , Mtume Muhammad (ﷺ) alifanya Nini kipindi Yuko Makkah kupinga uonevu na dhuluma dhidi ya Waislamu kwa miaka Mingi alioishi pale ? naomba twende kielimu na usikimbia maswali na huu mjadala maana umeyataka mwenyewe.
Eti twende kielimu kwa tuneno twa kukaririshwa,yaani nikimbie mjadala na kijimadhkali kwa elimu fupi ya kukaririshwa na kufungwa kwenye boksi! eti makhawarij,ukiambiwa utaje sifa za khawarij huwezi taja zaidi ya kukaririshwa kikasuku!
Haya na kaswali kako ka kitoto,eti mtume alifanya nn makkah kupinga uonevu na dhulma ...jibu,Alifanya subira na kuwausia aliokuwa pamoja naye kama Ammar Yasir kuwa wafanye subira na mafikio yao ni Jannah..
 
Jamaa umeongea elimu kubwa sana ambayo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuwa nayo katika Maisha watu inabidi waangalie jambo lenye maslahi kwa ummah mzima na sio madhara kwa ummah
Maslahi kwa ummah ni yapi na madhara ni yapi?
 
Hatutaki kumwaga damu sisi sote ni ndugu ni bora anaeyesababisha amani kuvunjika atoke tubakie salama
 
Mlango muhimu katika Uislamu ni kupima baina ya Maslahi(Faida ) na Mafisadi (Hasara) kwa kila jambo na focus inakuwa kwanza kuondoa Madhara kuliko kupata Faida na kama jambo madhara yake ni makubwa kuliko Faida basi tunaacha nalo .

Kwa msingi huo ndio najibu swali lako ni kweli Wapalestina kwa miaka Mingi wanaonewa hata Mimi inaniumiza sana . Sasa inajulikana wazi tabia ya Mayahudi hawana huruma ukiingia kwenye 18 zao na uwezo wa kupambana nao hauna na ukijaribu maafa makubwa kuliko manufaa.

Sasa hapo Bora jambo la kupigana uachane nao uishi kinyonge , pigana ukiwa na uhakika kuwa adui yako mna nguvu sawa na unaweza kumshinda vinginevyo utajisabaishia tabu kubwa mno.

Kwa maelezo zaidi soma huu Uzi wangu.


Cc : Baljurashi
Mayahudi wanatumia kanuni toka Biblia ya shetani inasema hivi.
Katika zile amri kumi na moja za shetani kwa wanadamu.
Usimchokoze Wala kumuumiza mwanadamu yeyeto lakini akikudhuru mlipizie mara kumi na yake hadi asivyoamini.
Ndo Wayahudi wakaja na damu ya Myahudi mmoja akiuliwa inalipwa na damu mia moja.
Thus hawana huruma hawa jamaa
 
Kijana hongera umejitahidi kadri ya uwezo wako kuelimisha ummah ila watu hawatokuelewa kwa sasa ivi



Nb:Mtawala hadhihakiwi
Shukran sana Al Akh, Jazaakallahu khayran.
 
kimadkhali

Hakuna kitu kinaitwa "umadkhali" ni jina tu wametupiwa masalafi kuwachafua na kutaka kuwakimbiza watu kuikimbia Da'awah ya Salaf. Na hamtafanikiwa, kwa Idhini ya Allah, kama ambavyo wameshindwa/wanashindwa waliosema/wanaosema kuna "Uwahabi". Huwezi kuthibitisha uwepo wa huo unaoitwa "umadkhali" . Shaykh Rabee' Al Madkhali (Allah Amhifadhi) ni Mwanachuoni wa Kisalafi. Hakuleta pote jipya. Huwezi kuthibitisha uwepo wa fikra za "kimadkhali".
 
Ajabu ya watu wenye upeo mdogo kama huyu mtoa mada ni kujiona wamesoma dini kwa kule kumezeshwa fikra za "kimadkhali" kuwa punda wa watawala ilhali dini iko mbali na kila aina ya ukondoo na upunda .. asichokijua ni kuwa uislam ni dini ya ukombozi na iko mbali na dhulma na uonevu
Lengo ni kuishi. Lengo ni amani. Lengo ni nafsi yako na yakwako kwakuyafanya kwa utulivu. Hapo ulipo najua hufurahishwi na kero za jirani muovu, huyo nijirani muovu. Vipi adui mwenye silaha. Akusumbulie na akuonee miezi,miaka. Acha kujiona unazo sana. Jitafakari na uwache kujitekenya na "reasoning" icho hakina ukomo. Upeo ni mazingatio. <Consistency viscosity>
 
Eti twende kielimu kwa tuneno twa kukaririshwa,yaani nikimbie mjadala na kijimadhkali kwa elimu fupi ya kukaririshwa na kufungwa kwenye boksi! eti makhawarij,ukiambiwa utaje sifa za khawarij huwezi taja zaidi ya kukaririshwa kikasuku!
Haya na kaswali kako ka kitoto,eti mtume alifanya nn makkah kupinga uonevu na dhulma ...jibu,Alifanya subira na kuwausia aliokuwa pamoja naye kama Ammar Yasir kuwa wafanye subira na mafikio yao ni Jannah..
Kwa nini aliwahisia subra na sio kukiwasha ?

Na Mimi ninayekataza watu fikra za kukiwasha hauoni kama nafuata njia ya Mtume Muhammad (ﷺ) ?
 
Sijasoma upuuzi wako, swali moja: Nani kakwambia hii nchi ya kiislamu?
Nimeandika kwa ajili ya kuwakomboa kiFikra Waislamu Wenye fikra potufu za kuwatunishia misuli watawala .

Kama Baba yako hauwezi kumuongolea hovyo Wala kumkusoa kwa nguvu hadharani halafu kwa watawala ndio unakuja front .......
 
DINI ni mpango wa WANASIASA kuendelea kudumaza ufahamu na akili ya watawaliwa... Huo UISLAM uko wapi nyakati za dhulma na maonevu yanayofanyika na hao wanasiasa?...
 
Kwa nini aliwahisia subra na sio kukiwasha ?

Na Mimi ninayekataza watu fikra za kukiwasha hauoni kama nafuata njia ya Mtume Muhammad (ﷺ) ?
Kwani mtume alikuwa akiongea kwa matamanio yake au kwa kufuata wahyi toka kwa Allah?

Huwezi kuwa unafuata njia ya Mtume sababu baadae "alikiwasha" kwa maneno yako..ndio maana akaiacha dini imekamilika
 
Lengo ni kuishi. Lengo ni amani. Lengo ni nafsi yako na yakwako kwakuyafanya kwa utulivu. Hapo ulipo najua hufurahishwi na kero za jirani muovu, huyo nijirani muovu. Vipi adui mwenye silaha. Akusumbulie na akuonee miezi,miaka. Acha kujiona unazo sana. Jitafakari na uwache kujitekenya na "reasoning" icho hakina ukomo. Upeo ni mazingatio. <Consistency viscosity>
Utulivu bila Tawheed na uadilfu ni upotofu
Acha hekaya za kulaza umma bwn mdogo,dini hii ipo mbali na fikra za dhulma na uonevu..Mitume wote walikuja duniani kwa ukombozi,hawakuja kwa fikra za kutetea dhulma
 
Nimeandika kwa ajili ya kuwakomboa kiFikra Waislamu Wenye fikra potufu za kuwatunishia misuli watawala .

Kama Baba yako hauwezi kumuongolea hovyo Wala kumkusoa kwa nguvu hadharani halafu kwa watawala ndio unakuja front .......
We kweli akili ndogo,yaani kutetea dhulma na uonevu ndio kukomboa watu kifikra? Kichwa kinafanya kazi kweli? Hivi unaelewa maana ya kukomboa?
 
Na nguruwe a.k.a kitimoto cjaona hapo
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom