Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Utawala wa kiislam ni sumu katika jamii yoyote inayojitambua akili na ipendayo haki. Bila ubishi, angalieni tu nchi zilizo kwenye utawala wa Kiislam, watu wanashinda kuvaa shuka tu na kushinda misikitini kuangaliana nani anakula mara tatu kwa siku na nani asiyefunga ili wamzidhibiti. Wananchi wa hizo nchi wanaishi kwa hofu na kutawaliwa na ujinga zaidi badala ya common sense. Mwanamke kuvaa magunia mwilini ama kufanana na mke wa shetani (kuvaa burqa na hijab) eti ndiyo fashion. Huyu Mama Samia akamatwe tu asije kutuletea upuuzi wa sharia law ndani ya nchi yetu.
 
Acha bhangi kijana
 
Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu

Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969
Je vipi kuhusu haki?
 
Uislam una njia rahisi sana ya kudeal na kiongozi dhalimu. Njia yenyewe ni kuuawa.
Kati ya makhalifa wanne wa kwanza, watatu kati yao waliuawa.
Hawaliouwawa ni Umar (634-644CE), Uthman (644-656CE) na Ali (644-661CE)

Hata kwa dola ya Kiislam ya Ummayad na Abbasid viongozi madhalimu walikuwa wakiuawa tu. Hapakuwa na sababu ya kusubiri maandamano kuwaondosha.
Kwa uchache upande wa Ummayad waliouawa ni:
Al Walid II (744), Ibrahim ibn Al Walid (744CE) na Marwan II (750CE),

Kwa uchache Abbasid makhalifa madhalimu waliouawa ni Al Amin (813CE) na, Al Mutawakkil (861CE).

adriz nakuung mkono tutmie njia ya Kiislam kudeal na viongozi madhalimu

Najua wewe sio Muislam ila uache kuropoka.

Makhalifa 'Umar, 'Uthman na 'Ali hawakuwa madhalimu. Walikuwa ni maswahaba watukufu waliobashiriwa Pepo wakiwa hai na ni watu bora katika Ummah huu. Ni watu ambao uadilifu wao umethibiti.

Khalifa 'Umar (Allah Amridhie) aliuawa na mmajusi Abu Lu-lu. Hivyo mtu huyo aliyemuua Khalifa 'Umar wala hakuwa Muislam.

Khalifa 'Uthmaan (Allah Amridhie) aliuliwa na makhawaarij, mbwa wa motoni. Tena matukio yaliyopelekea kifo cha Swahaba Mtukufu 'Uthmaan yanatuachia funzo sisi katika mifano ya kihistoria ya namna makhawaarij walivyo watu wabaya na fitna yao kwa Ummah ilivyo mbaya. Kifo cha Swahaba 'Uthmaan kilipelekea fitna kubwa.

Khalifa 'Ali (Allah Amridhie) naye aliuliwa na makhawaarij, mbwa wa motoni.

Makhawaarij, walitabiriwa na walipewa wasifu mbaya na Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) ambaye aliwaita mbwa wa motoni.

Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) huyo huyo aliyewaita khawaarij kuwa ni mbwa wa motoni ndio kawakataza Waislam kujiondoa katika twaa ya mtawala Muislam (kumfanyia uasi) hata kama mtawala huyo ni muovu.

Na hata mtawala akiwa kafiri, hatofanyiwa uasi iwapo kama kufanya hivyo kutapelekea fitna na umwagikaji damu.

Lakini khawaarij wanahalalisha kufanya uasi dhidi ya mtawala Muislam. Wanahalalisha kuondoa mkono wa utiifu kwake na kuimwaga damu yake. Kwa visingizio mbalimbali kama kujidai wanaondoa dhulma, au wanaondoa uovu au wanataka kusimamisha Shari'ah.

Hata kama mtawala sio dhalimu watamtafutia visingizio ili wamfanyie uasi, kama walivyofanya kwa 'Uthmaan Swahaba Mtukufu kabisa ambaye mpaka Malaika walikuwa wakimuonea haya, Mtu mwema kabisa ambaye walimsingizia na kufanya propaganda dhidi yake na wakaibua hisia za baadhi ya watu dhidi yake mpaka akauawa shahidi akiwa anasoma Qur’an.

Khawaarij, mbwa wa motoni, walimuua 'Ali Swahaba mwengine mtukufu (Allah Amridhie) wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake), ambao kwa ujinga wao khawaarij walikataa suluhu baina yake Swahaba 'Ali (Allah Amridhie) na Swahaba Mu'awiya (Allah Amridhie) khawaarij wakidai kwa ujinga kuwa Khalifa Muongofu na Swahaba Mtukufu aliyebashiriwa Pepo akiwa hai 'Ali (Allah Amridhie) eti alikwenda kinyume na Shari'ah kwa kufanya suluhu na Swahaba Mtukufu na Amiri wa Waumini (ambaye alikuja kuwa Mfalme wa kwanza katika Ummah huu na mbora wa wafalme wa kiislam) Mu'awiya (Allah Amridhie), ilhali 'Ali ni mjuzi wa Dini kuliko wao khawaarij mbwa wa motoni na alikuwa sahihi kabisa kufanya suluhu. Lakini khawaarij walimkufurisha 'Ali, Mu'awiya na Waislam wote ambao hawakuwa pamoja nao hao makhawaarij na wakazihalalisha damu zao na mwisho wakamuua Khalifa Muongofu 'Ali (Allah Amridhie).

Lakini waliyoyafanya yalileta mabalaa tu na siku zote wanayoyafanya huongeza fitna na mabalaa kwa Ummah.

Mfano mkubwa ikiwa walipomuua Amiri wa Waumini 'Uthmaan Dhun Nuurayn (Allah Amridhie) fitna zikazidi zaidi katika Ummah na migawanyiko mpaka leo hii.

Ndio maana Mtume aliwaita mbwa wa motoni na kuwa ni watu waovu zaidi wanaouawa chini ya Mbingu. Kwa sababu ya fitna yao na uovu wao.

Waislam tumefundishwa subra juu ya dhulma ya mtawala. Tumpe haki yake hata kama yeye atatunyima zetu. Na kumsikiliza na kumtii kwa sababu sisi tutakuwa tumeutua mzigo wetu na yeye ana mzigo wake. Tumekatazwa kuondoa mkono wa utiifu kwake na tumeamrishwa kumsikiliza na kumtii (maadamu sio katika haramu) hata kama ni dhalimu na tuwe na subra juu ya dhulma yake. Na unapopata fursa ya kumnasihi uso kwa uso, umnasihi kwa siri au kama kumuandikia basi umuandikie kwa siri na sio kumsema mbele za watu.

Katufundisha hili Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake) na wema waliotangulia walisimama katika hili.

Mtume alitabiri kudhihiri kwa watawala wenye mioyo ya mashetani katika viwiliwili vya wanadamu, alitabiri watawala ambao hawaongozi kwa mwenendo wake ila akataka Waislam wasikilize na watii.

Salaf walisimama juu ya hili

Kulipotokea watawala waovu kama Hajjaj Ibn Yusuf ath-Thaqafi ambaye alimuua mpaka Swahaba 'Abdullah Ibn Zubayr (Allah Amridhie yeye na baba yake), alimuua mwanachuoni mkubwa katika Taabi'in, Sa'id ibn Jubayr (Allah Amrehemu) na watu wengine wengi, Salaf walikuwa na subra na wakawazuia watu kufanya uasi. Mfano Taabi'i al-Hasan Al-Basri (Allah Amrehemu) alipofuatwa na baadhi ya vijana waliotaka kufanya uasi dhidi ya Hajjaj, wakamuomba ushauri akawakataza hilo akawaambia kama Hajjaj ni adhabu ya Allah kwao basi hawataweza kuiondoa kwa panga zao na kama ni mtihani tu wa Allah, basi wawe na subra mpaka hukumu ya Allah itakapokuja. Ila hawakumsikiliza na wakaenda kupigana na Hajjaj, wakauwawa wote.

Licha ya uovu wake Hajjaj, Salaf hawajitoa katika mkono wa utiifu kwake na mpaka wapo wengine kama 'Abdullah 'Ibn 'Umar (Allah Amridhie yeye na baba yake) waliswali nyuma yake.

Imam Ahmad Ibn Hanbal (Allah Amridhie), mmoja katika Wanachuoni wakubwa wa Ummah huu, aliteswa wakati baadhi ya watawala wa Dola ya Abbasiya (Abbasid Empire) walipoathirika na itikadi za Mu'utazila wakawa wanawalazimisha watu kukiri itikadi ya kikafiri kuwa "Qur’an ni kiumbe" na ilhali Qur’an sio kiumbe bali ni maneno ya Allah aliyoyasema kwa Herufi na Sauti. Imam Ahmad na Wanachuoni wenzie wengi tu wa Ahlus Sunnah (Allah Awarehemu) waliteswa na kufungwa kwa sababu tu walikataa kukiri kuwa "Qur’an ni kiumbe".

Lakini;

Imam Ahmad licha ya kuwa alisimamia msimamo wa kuwa Qur’an sio kiumbe bali Qur’an ni Maneno ya Allah, ila hakuondoa mkono wa utii kwa mtawala aliyekuwa akimtesa, bali alipokuwa akimzungumzisha mtawala alikuwa anamuita Amiri wa Waumini. Na alipofuatwa na baadhi ya watu kumtaka aungane nao kumpinga mtawala na kuasi, kumbuka Imam alikuwa anaungwa mkono, akakataa na akawakataza wasifanye uasi wala wasiondoe mkono wa utiifu kwa mtawala na akiwataka wachunge damu zao na za Waislam. Hilo ni pamoja na kukataa kabisa itikadi ile ya kikafiri na kukubali kuteswa na kukaa gerezani.

Zaidi alikuwa akimuombea dua za kheri mtawala.

Hawa ni Salaf wetu.

Tofauti na khawaarij waliokuwa wakihalalisha kujitoa katika twaa ya mtawala Muislam na kumpiga vita na hata kuhalalisha damu yake.

Na itikadi za hawa khawaarij zimedhihiri tena katika zama zetu hizi kupitia fikra za akina Sayyid Qutb wakazifuata akina Muslim Brotherhood, Hizbu Tahrir, akina Osama Bin Laden na al-Qaeda yao, akina Ayman Al Zawahiri, Abu Mus'ab Al Zarqawi, Abu Bakr Al Baghdadi, hawa ash-Shabaab , Boko Haram na wengine wanaofanya ukhawaarij kwa vitendo au maneno.

Allahul Musta'an

Tunamuomba Allah afya na salama
 
Ni kweli unachosema! Mtu kama hajawahi kuiona vita na madhara yake siyo rahisi kusikiliza ushauri kama huu! Amani unayosema ni AMANI YA KUTOGUSA WATAWALA HATA WAKIKOSEA!
 
Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu

Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969
Jamaa umeongea elimu kubwa sana ambayo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuwa nayo katika Maisha watu inabidi waangalie jambo lenye maslahi kwa ummah mzima na sio madhara kwa ummah
 
Sijasoma upuuzi wako, swali moja: Nani kakwambia hii nchi ya kiislamu?
 
Mi ni muislamu ,we unazungumzia uislamu gani mkuu
Kinachoponza viongozi wa kiislamu ni unafki na kujipendekeza kwa watawala
Wanaharakat wengi huwa ni waislamu ila wanachomwa na viongozi wao wa juu
 
Ajabu ya watu wenye upeo mdogo kama huyu mtoa mada ni kujiona wamesoma dini kwa kule kumezeshwa fikra za "kimadkhali" kuwa punda wa watawala ilhali dini iko mbali na kila aina ya ukondoo na upunda .. asichokijua ni kuwa uislam ni dini ya ukombozi na iko mbali na dhulma na uonevu
Eti Fikra za kimadhali ! Wewe si unaelimu twende kwenye majadiliano ya kielimu hoja by hoja kwa dalili bila kukimbia .

Mimi natetea hoja kutokana na dalili halafu wewe unaleta fikra zako ? hii ndio shida ya MaKhwawarij na watu wenye Elimu na upeo mdogo wa Dini.

Haya jibu swali fupi Je , Mtume Muhammad (ﷺ) alifanya Nini kipindi Yuko Makkah kupinga uonevu na dhuluma dhidi ya Waislamu kwa miaka Mingi alioishi pale ? naomba twende kielimu na usikimbia maswali na huu mjadala maana umeyataka mwenyewe.
 
Utawala wa kiislam ni sumu katika jamii yoyote inayojitambua akili na ipendayo haki. Bila ubishi, angalieni tu nchi zilizo kwenye utawala wa Kiislam, watu wanashinda kuvaa shuka tu na kushinda misikitini kuangaliana nani anakula mara tatu kwa siku na nani asiyefunga ili wamzidhibiti. Wananchi wa hizo nchi wanaishi kwa hofu na kutawaliwa na ujinga zaidi badala ya common sense. Mwanamke kuvaa magunia mwilini ama kufanana na mke wa shetani (kuvaa burqa na hijab) eti ndiyo fashion. Huyu Mama Samia akamatwe tu asije kutuletea upuuzi wa sharia law ndani ya nchi yetu.
Ukiwa mjinga Kiasi hiki haustahili kujibiwa.

Idiot detected , ahsante kwa kushiriki.
 
Jamaa umeongea elimu kubwa sana ambayo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuwa nayo katika Maisha watu inabidi waangalie jambo lenye maslahi kwa ummah mzima na sio madhara kwa ummah
Shukrani Al Akh Allaah akulipe kheri, aamiyn.

Laiti Waislamu tungesoma dini yetu kisawasawa na kuifanyia kazi matatizo mengi yangeondokana katika Jamii na watu wengi wangeufuta Uislamu kwa kuuenda tatizo tuko mbali na Elimu na kufanyia kazi.

Mimi mwenyewe miaka ya nyuma nilikuwa na fikra mbaya sana za uasi moyoni na harakati za kutawala na Dola si ajabu kwa kujua kwamba ndio mapambano ya kweli na ni dini.

Unakuta Muislamu huyo anayeshadadia uongozi mbovu na Mabadiliko yeye mwenyewe ameshindwa kuibadili nafsi yake na kuiongoza vyema Familia yake ndogo tu . Unakuta Kuna miziki , hawaswali mmonyoko wa maadili nk sasa baada aanze na jambo ambalo ataulizwa siku ya kiyama kurekebisha anashadadia juu kwenye uongozi wakati siku ya Qiyama hautoulizwa kuhusu Rais bali ni wewe na Familia yako.
 
Huwa najiuliza kuhusu nchi ya Kenya.Mbona Wana katiba mpya,,tume huru ya uchaguzi na washafanya reform za kutosha chama cha kanu kilishakufa wapinzani wameshashika nchi lakini bado wanalalamika.?? Inawezekana tatizo likawa linahitajika kutafutwa na wasio wanasiasa Kwa taratibu ndio Uma ujue kuna tatizo lililoonwa na akili ya watu wali huru??
Wanasiasa walishatukwamisha sasa hivi ni wakati mwafaka kwa Jeshi kuchukua nchi. Nchi zote za kiafrika zinatakiwa kuchukuliwa kijeshi.
 
Wanasiasa walishatukwamisha sasa hivi ni wakati mwafaka kwa Jeshi kuchukua nchi. Nchi zote za kiafrika zinatakiwa kuchukuliwa kijeshi.
Kesho hili linalopiga watu wakati wa uchaguzi , na Viongozi wake ndio hawa skina Kikwete ?
 
Back
Top Bottom