Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Hakuna kitu kinaitwa "umadkhali" ni jina tu wametupiwa masalafi kuwachafua na kutaka kuwakimbiza watu kuikimbia Da'awah ya Salaf. Na hamtafanikiwa, kwa Idhini ya Allah, kama ambavyo wameshindwa/wanashindwa waliosema/wanaosema kuna "Uwahabi". Huwezi kuthibitisha uwepo wa huo unaoitwa "umadkhali" . Shaykh Rabee' Al Madkhali (Allah Amhifadhi) ni Mwanachuoni wa Kisalafi. Hakuleta pote jipya. Huwezi kuthibitisha uwepo wa fikra za "kimadkhali".
Umadhkali upo.. ni pote linalomfuata Rabee Madhkali na lipo mbali na usalafi,likijikita kutetea watawala kwa kupindisha mafundisho sahihi kwa maslahi ya watawala waovu na vibaraka wao.. msingi wake ni serikali ya Saudia
 
Mambo ya Dini huwa sipendi kuyasema sanaa lakini ujinga wa mtu kama wewe ni mkubwa hivi mtume alipigania nini ili iweje?? walioandamana Tunisia..Misri..Libya Uturuki ni wa Ufufuo na uzima?
 
Mambo ya Dini huwa sipendi kuyasema sanaa lakini ujinga wa mtu kama wewe ni mkubwa hivi mtume alipigania nini ili iweje?? walioandamana Tunisia..Misri..Libya Uturuki ni wa Ufufuo na uzima?
Jinga hilo
 
Kijana hongera umejitahidi kadri ya uwezo wako kuelimisha ummah ila watu hawatokuelewa kwa sasa ivi

Nb:Mtawala hadhihakiwi

«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad iliyo bora kabisa ni kusema neno la kweli mbele ya mtawala jeuri.”
 
Ni kweli unachosema! Mtu kama hajawahi kuiona vita na madhara yake siyo rahisi kusikiliza ushauri kama huu! Amani unayosema ni AMANI YA KUTOGUSA WATAWALA HATA WAKIKOSEA!

«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad iliyo bora kabisa ni kusema neno la kweli mbele ya mtawala jeuri.”
 
Kwani mtume alikuwa akiongea kwa matamanio yake au kwa kufuata wahyi toka kwa Allah?

Huwezi kuwa unafuata njia ya Mtume sababu baadae "alikiwasha" kwa maneno yako..ndio maana akaiacha dini imekamilika
Wahyi

Kipi kilichosababisha asipigane dhidi ya dhuluma kipindi kile apigane baadae baada ya miaka Mingi kupita ?
 
We kweli akili ndogo,yaani kutetea dhulma na uonevu ndio kukomboa watu kifikra? Kichwa kinafanya kazi kweli? Hivi unaelewa maana ya kukomboa?
Uislamu kila kitu kimeelekeza njia yake ya kuliendea kuanzia swala , zaka nk sio kwa sababu umeambia uswali basi mtu anaswali kwa namna atakayo au anayoona sawa hiyo si sawa
 
Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu

Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969
Nchi ya Tanzania inaendeshwa kwa sheria za kutofuata dini yoyote.

Nchi haiendeshwi kwa Uislamu.

Sasa kwa nini unatanguliza Uislamu hapa?

Wengine tunaona Uislamu umejaa ujinga tu.
 
Wahyi

Kipi kilichosababisha asipigane dhidi ya dhuluma kipindi kile apigane baadae baada ya miaka Mingi kupita ?
Mbona unarudia swali hilohilo?
Sasa kwani alikuwa kaamrishwa?
Mbona huulizi nini kilimfanya asifunge Ramadhan mpaka miaka mingi kupita?
Kwani alikuwa akifanya mambo kwa matamanio yake?
 
Uislamu kila kitu kimeelekeza njia yake ya kuliendea kuanzia swala , zaka nk sio kwa sababu umeambia uswali basi mtu anaswali kwa namna atakayo au anayoona sawa hiyo si sawa
Sasa nani hajui hilo?
Acha hekaya kijana
 
Nxhi ya Tanzania inaendeshwa kwa sheria za kutofuata dini yoyote.

Nchi haiendeshwi kwa Uislamu.

Sasa kwa nini unatanguliza Uislamu hapa?

Wengine tunaona Uislamu umejaa ujinga tu.
Hoja kama hizi tulizitegemea kwa kijana mpumbavu kama huyu mleta thread kuleta bandiko lake huku
Hakika "ukasuku" ni janga
 
Nxhi ya Tanzania inaendeshwa kwa sheria za kutofuata dini yoyote.

Nchi haiendeshwi kwa Uislamu.

Sasa kwa nini unatanguliza Uislamu hapa?

Wengine tunaona Uislamu umejaa ujinga tu.
Popote wanaosema vibaya Serikali na kwenda kinyume yaani wale potential threats serikali inawafyeka na kuwakandamiza hata nchi zinazojiita za Kidemokrasia.

Marekani ; Wanafunzi wanaonga mkona Palestina wamezimwa na wengine kufukuzwa z kufanyiwa figisu nk.

Israel ; ndio kabisa hawataki masihara wanafanyia vitimbi activists na diplomats mbalimbali

Jullian Assange nae yalimkuta.

Kwa vile nchi hii ina Waislamu na Mimi ni Muislamu jukumu langu ni kusafisha fikra mbovu kwa Waislamu warejee katika njia sahihi ya dini na haya ndio makusidio mama ya huu Uzi mengine ni ziada.
 
Hata Uislamu huujui.

Uislamu unasisitiza haki na watu kupigania haki.

Sasa wewe unatetea Uislamu gani huo wa kukubali kutekwa na kuuawa?
 
Sasa nani hajui hilo?
Acha hekaya kijana
Ndio nakuambia kutokana na msingi huo hata huko kupinga dhulma na uonevu dhidi ya mtawala Kuna namna na utaratibu wake kutokana na mafundisho sahihi ya dini ya Kiislamu , kama ilivyokuwa swala na mambo mengine yana sheria na taratibu basi hata Hilo jambo unalodai pia Lina taratibu zake Kaa chini usome au ufundishwe . Kwenye Uislamu hakuna Jazba , mihemko na matamanio bali mambo yanaenda kielimu.
 
Ndio ngonjera zako za upeo mdogo zilipoishia..Hakika "ukasuku" ni janga kwa vijana..
Yaani vimaneno vya kukaririshwa tu,uwezo mdogo wa kujenga na kutetea hoja
Sasa wapi nimekwambia halina utaratibu? Kwa hiyo hoja yako halipo au lina utaratibu wake?
Na huo utaratibu wake ni upi?
 
Hata Uislamu huujui.

Uislamu unasisitiza haki na watu kupigania haki.

Sasa wewe unatetea Uislamu gani huo wa kukubali kutekwa na kuuawa?
Kapumbavu hako..
Hutu tu vijana tunatovamia dini kwa misafara ya mwenge ni tatizo..ushamba na upeo mdogo ndio umevitawala

Hivi kuna dini inayosisitiza haki na kupinga dhulma isiyokuwa uislam?

Ila usichokijua hivi vijitu ni zao la utawala muovu wa Al Saud pale saudia ambao ndio umezalisha kakikundi chini ya sheikh wao Rabee Madhkali lengo na madhumuni kulinda ufalme wao muovu usipingwe!
 
Hata Uislamu huujui.

Uislamu unasisitiza haki na watu kupigania haki.

Sasa wewe unatetea Uislamu gani huo wa kukubali kutekwa na kuuawa?
Hapa umefika pazuri napenda watu kama nyinyi .

Katika kila jambo lazima Kuna kuwa na miongozo na taratibu mfano hata shuleni mkiambiwa siku Fulani Wanafunzi mripoti huwezi kuripoti hivi hivi lazima utakuta taratibu na namna ya kuripoti mfano uje ukiwa na Uniform , Majembe nk.

Hata ukiambiwa kwenye kula kisa umeambiwa ule hauwezi kula kama mnyama lazima unakuta Kuta taratibu za kula mfano kunawa mikono kwanza , kula kupitia kinywa nk.

Tukirudi kwenye Uislamu ibada na matendo yote yanataratibu zake , mfano Qur'an imeamrisha kuswali je , kila mtu ataswali kwa namna ayavyotaka bila muongozo ? Qur'an imeamrisha Jihad je mtu atachukua upanga na kuua kila mtu wakati wowote hadi watoto ?

Jibu hapana ili kitu kiitwe dini kwenye Uislamu lazima muongozo wa kufanya utoke kutokana na jinsi Mtume Muhammad (ﷺ) alivyofanya na kuamrisha na kufundisha namna ya ufanyaji wake .

Uislamu unasisitiza kupigania haki na kupinga dhuluma na uonevu ila imeweka namna na misingi yake katika kuendelea Hilo kama ilivyo kwenye mambo mengine kama Swala , Ndoa , Zaka nk sasa haiwezekani mtu aibuke kufanya jambo katika Uislamu kwa namna anayoona yeye ni sawa.
 
Ndio nakuambia kutokana na msingi huo hata huko kupinga dhulma na uonevu dhidi ya mtawala Kuna namna na utaratibu wake kutokana na mafundisho sahihi ya dini ya Kiislamu , kama ilivyokuwa swala na mambo mengine yana sheria na taratibu basi hata Hilo jambo unalodai pia Lina taratibu zake Kaa chini usome au ufundishwe . Kwenye Uislamu hakuna Jazba , mihemko na matamanio bali mambo yanaenda kielimu.
Kwa hiyo hoja ni namna na utaratibu na sio kwamba haifai?
Duu hakika madhkalia ni mojawapo ya maajabu ya dunia!
 
Back
Top Bottom