Uislamu hauruhusu mambo haya dhidi ya Mtawala: Kumkosoa hadharani, kumdhalilisha, kufanya maandamano na kutoka dhidi yake

Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu

Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969
LONG STORY SHORT UNAMAANISHA WAISLAMU HAWANA HAKI YA KUKOSOA WALICHOCHAGUA?
 
Mvuta bangi kama wewe ni kuwa ignore tu,ni kujishusha hadhi na kujibizana nawe..
You a pathetic Scumbag , If you are Man stop complaining do some actions and fight bravely , don't be like a stupid fool.

Only Cowards can sit but for commander to die on battleground is a honour.

Shame on you a Keyboard Warrior, Maarass!!!

Cc : The Mongolian Savage
 
TATIZO AFRIKA TUNAONGOZWA NA MAWAZO YA KIDINI NA SAYANSI YA MZUNGU... NA DINI ZOTE MBILI ZIMETOKA KWA MZUNGU NA MUARABU NANI ANAELA HAPA DUNIANI KAMA SIO MUARABU NA MZUNGU... JE WEWE MUAFRIKA AMBAE BABU ZAKO WALIPITA UTUMWANI TUNASHAURI NINI JUU YA HILO??
BINAFSI UKIMCHAGUA KIONGOZI AKUTAWALE ANAWAJIBU WOTE WAKUJIBU SHTAKA ZANGU KWAKE NA ANAOWAJIBU WAKUTENDA MEMA KWAAJILI YANGU...
MIMI SIO MTUMWA AMBAE NITAMWAMBIE SLAVE MASTER ASANTEH
 
Moja kwa moja..

Sababu ya kuandika huu uzi ni kutokana na baadhi ya fikra za Wabongo wanona kutokana na mapungufu ya serikali bora tukiwashe na kukinikisha wengine wakienda mbali wanasema damu zikimwagika ndio tutaheshimiana. Nawaambia ndugu zangu Amani ni jambo muhimu sana bila kujali mambo gani yanaendelea waulizeni Hamas waliona bora kukiwasha kuliko unyonge sasa wamepata Faida na madhara gani , cheki Sudan mambo ya kupindua utawala yamepeleka uovu zaidi na hali mbaya mno , Libya nk mnoshadadia tukiwashe hamjui huku kwetu machafuko yatafika mbali kiasi gani na kusababisha madhara gani , kwa sisi ambao tumewahi kuishi sehemu kukiwa na mabomu na mitutu mara kwa mara tunaelewa Amani ni jambo zito kiasi gani.

Uislamu ni dini kamili ina sheria na miongozo yake inayojitosheleza katika kila jambo na tatizo lilipo Waislamu wengi tumekuwa wavivu wa kukaa chini kusoma dini yetu kwa uhakika na usahihi na hili swala ndio chanzo kikubwa cha matatizo kwa Umma wa Kiislamu kupelekea wengi kufuata mihemko , mkumbo na matamanio ndio maana Kuna kipindi baadhi ya Waislamu Osama walimuona kama Kidume na shujaa wa Kiislamu , wengine wakafuata mikumbo kuingia katika makundi potofu ya Jihadi na kuanzisha vuguvugu mbalimbali.

Na upande wa Wakristo wengi pia hawana ufahamu sahihi na Elimu ya uhakika kuhusu Uislamu ndio maana sio ajabu kukuta eti Mkiristo kukuambia Qur'an ina majini , Kufunga majini nk . Tatizo hili kuu la kukosa Elimu limepelekea wengi katika Wakristo au Waislamu ukiwaelekeza jambo Fulani la sawa kuhusu Uislamu wanaona kama ni jambo geni kwao na wanaweza kukupinga tu.

MIAKA YA VUGUVUGU ZA UASI KWA WAISLAMU

Kama mnakumbukumbu vizuri miaka kuanzia 2010 - 2013 hapa bongo kulitokea vuguvugu kubwa lililopamba moto kwa Waislamu wanaonewa na serikali katika nyanja mbalimbali na wengine wanaojiita Masheikh walikuwa Mstari wa mbele waliwahamaisha kuhamasisha maandamano, Fujo , uasi nk na ilileta madhara makubwa mpaka serikali ikaamua sasa kuvalia njuga ikakamata Masheikh na watu wengi Wenye hatia , wasio na hatia hata redio Moja maarufu ya Waislamu ilifungiwa kutokana na kuchochea chuki na uasi hatimaye hali ikapoa vuguvugu likapotea mpka sasa hali shwari.

MAANDIKO YANASEMAJE ?

Uasi (khurooj) hufafanuliwa kama kujaribu kunyang’anya mamlaka kutoka kwa mtawala, kumpinga hadharani, kujaribu kumwondoa madarakani kwa nguvu, kuwachochea watu dhidi yake (kupitia maandamano, mikutano ya hadhara, maandamano ya barabarani, migomo, n.k.), kupanga njama dhidi yake na kuinuka kumpinga kwa maandishi, kwa khutuba au kwa upanga.

Haya yote yanachukuliwa kuwa ni khurooj. Mtume (ﷺ) alikataza jambo hili katika hadithi zilizo wazi na zenye nguvu. Hadithi ambazo haziwezi kupingwa na matamanio, maoni binafsi au akili, wala kwa maamuzi yasiyo sahihi ya watu, bila kujali daraja yao mbele ya watu. Mtume (ﷺ) alizungumza kwa wahyi (ufunuo) kutoka kwa Allah, lakini waliokuja baada yake hawakuwa na wahyi. Kwa sababu hiyo, wakati ijmā’ (makubaliano ya pamoja ya wanazuoni) ilipothibitishwa, hakuna aliyepinga isipokuwa Khawārij, Shia, Mu’tazilah na matawi yao hadi wakati wetu huu.

Imepokewa na Muslim katika Sahih yake (1847) kutoka kwa Wā’il Ibn Hujr kuwa: Salamah Ibn Yazeed Al-Ju’fee alimuuliza Mtume wa Allah (ﷺ): “Ewe Mtume wa Allah, tufanye nini ikiwa tutakuwa na watawala juu yetu wanaotaka haki zao lakini wanatunyima haki zetu?” Akajibu: “Wasikilizeni na watiini [bila kujali]. Juu yao ni mzigo wao, na juu yenu ni mzigo wenu .”

MY TAKE :

Fikra za Kikhawarij (kutoka chini ya utii wa matawala ) ndio zimesababisha madhara ya Leo kuwepo Al Shabaab, Al Qaeda , Boko Haram nk wote hawa madai yao kwamba watawala hawaendesh kisawasawa wanaendesha mambo Kikafiri vurugu , kuingia msituni na kutoka dhidi yake.

Kubadilisha mtawala sio solutions ya matatizo yote ya kutawala , wakati wa kifo cha JPM baadhi ya watu mlishangilia na kumdhihaki vibaya mno na kuona matatizo yameisha na makundi yote yaliungana na kuimba mapambio ya "Mama anaupia mwingi " kuwaumiza wafuasi wa JPM sasa mmebadili gia angani.

Uzi huu unaendelea maana bado sijatoa solutions na Kuna mambo Muhimu bado sijayagusia

UPDATES :

1. Tuone kwa Manabii wa Mwenyezi Mungu

Nabii Musa (Amani iwe juu yake ) alikuta Wana wa Israeli wakionewa chini ya utawala wa Kiongozi Dhalimu mkubwa Firauni lakini hakuwa kuhubili Wana wa Israeli wafanye njama ya kumtoa Firauni Madarakani au wafanye maandamano na Uasi bali yeye aliwaningania katika neno la Mungu .

Na hiyo ndio wito wa Manabii mara nyingi hawapendi kushindana na Serikali kwa kutaka kupanga njama za kuwapondua uasi , fujo nk wao wamefocuos kuwapa neno la haki kwa njia Bora . Mfano Yesu , Nuh , Shuayb, Yusuph na wengineo ( Amani iwe juu Yao wote
a)Kutoka kwenye maisha ya Kiigizo chema Mtume Muhammad (ﷺ)

Msingi mwingine dini ya Uislamu katika kila ibada kiigizo chetu ni Mtume Muhammad (ﷺ) lazima iangaliwe yeye alifanya vipi ili jambo liitwe dini kinyume na hapo ni uzushi , sasa angalia maisha yake kipindi Cha utume katika mji wa Makkah ambapo Uislamu ulipokuwa hauna nguvu. Je , Waislamu wangapi waliuwawa kwa dhuluma , kuteswa , kuporwa mali zao , dhihaka na madhila mengine makubwa ? Je alimarisha kisasi , maandamano, Fujo , njama , mapinduzi nk ?

Jawabu hapana, walifanya subra na wakamcha Allaah hatimaye wakafanya Hijra kuhamia Madina ili kuepuka dhuluma na manyaso na sio kutumia Maguvu kuminyana na watawala wakati hata nguvu zenyewe hauna na madhara yatakayo patikana kwa watu ni makubwa mno.

#LindaAmaniYaNchiYako

View attachment 3353969
Acha porojo........kiongozi hata akiongoza kwa maovu tumpigie makofi na kumsifu??
Naona BAKWATA mmeanza kazi yenu.
 
Sijasema umsifu , kama hauna access ya kumfuata kumnasihi na kumshauri Bora ukae kimya.
 
Hakuna kitu kama hicho...... uislamu unasemaje kuhusu jambo baya??liondoe kwa mkono wako,lisema,au lichukie!
 
Huwa najiuliza kuhusu nchi ya Kenya.Mbona Wana katiba mpya,,tume huru ya uchaguzi na washafanya reform za kutosha chama cha kanu kilishakufa wapinzani wameshashika nchi lakini bado wanalalamika.?? Inawezekana tatizo likawa linahitajika kutafutwa na wasio wanasiasa Kwa taratibu ndio Uma ujue kuna tatizo lililoonwa na akili ya watu wali huru??
Tatizo siyo yaliyoandikwa (Kurani, Biblia, Katiba) bali NAFSI (malezi na mazingira yake) ya aliyeko MADARAKANI. Mamlaka ya mwenye madaraka uipa nafsi ya muhsika kufanya anavyotaka. Iko mifano mingi katika historia (Hitler, Mobutu, Idd Amin).

Kuna uwezekano mkubwa tuko kwenye awamu ya utawala wa wenye kusukumwa na NAFSI katika maamuzi yao.
 
Utulivu bila Tawheed na uadilfu ni upotofu
Acha hekaya za kulaza umma bwn mdogo,dini hii ipo mbali na fikra za dhulma na uonevu..Mitume wote walikuja duniani kwa ukombozi,hawakuja kwa fikra za kutetea dhulma
Ukileta reference ya hawa mitume wakombozi litakuwa jambo jema sana. Tenda uwadilifu kwa manufaa ya wengine. Oainisha kila kitu kutetea hii hoja yako.
 
Huwa najiuliza kuhusu nchi ya Kenya.Mbona Wana katiba mpya,,tume huru ya uchaguzi na washafanya reform za kutosha chama cha kanu kilishakufa wapinzani wameshashika nchi lakini bado wanalalamika.?? Inawezekana tatizo likawa linahitajika kutafutwa na wasio wanasiasa Kwa taratibu ndio Uma ujue kuna tatizo lililoonwa na akili ya watu wali huru??
Harakati za ukombozi wa mwanadamu zilikuwepo, zipo na zitaendelea nyakati zote hadi mwisho wa mwanadamu.
Matabaka yalikuwepo, yapo na yatakuwepo hivyo ni haki ya wanaokandamizwa kujiweka huru na kuwadhibiti wakandamizaji (struggle for existence/survival).
Hakuna mwenye huruma ya kweli kwa mwingine. Kupambana na hali yako ndiyo mpango halisi.
 
Nakuuliza wewe unaona ni kipi bora kwa Palestine kupata nchi yao na kuondokana na uonevu wa miaka yote ya Israel kwa miaka zaidi ya 70 wafanye nini tofauti na kilichofanywa na kinachofanywa na Hamas ?

Nakukumbusha unapojibu swali hili kumbuka Gaza ni gereza la Israel kwa miaka na miaka na mashambulizi ya Hamas ya oktoba yalifanyika katika maeneo ya walowezi wa Israel.
Kwenye dini yetu maelekezo yapo muda mrefu sana, shida ya ndugu zetu Wapalestina hawataki kufata maelekezo na dini.

Pale Wapalestina wanatakiwa waondoke na walishapewa maelekezo waende nchi kadhaa za kiislamu, lakini wao hawataki.

Ile ardhi ya Palestina ni ardhi ya Waislamu wote, na imeshaandikwa katika Zaburi na kwenye Qur'an kwamba ardhi Ile itarithiwa na Waislamu.
 
Hakuna kitu kama hicho...... uislamu unasemaje kuhusu jambo baya??liondoe kwa mkono wako,lisema,au lichukie!
Hadithi imesema liondoe kwa mkono wako ikishi mtu atashindwa (asipokuwa na uwezo huu ) , basi kwa ulimi asipoweza achukie.

Hapo tunaona jambo la uwezo limekuwa sharti , uwezo linajumuisha pia accessibility kwa hiyo kama hauna uwezo wa kumfikia kumwambia basi Kaa .
 
«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad iliyo bora kabisa ni kusema neno la kweli mbele ya mtawala jeuri.”

Hapa ni mbele ya mtawala?

Nenda basi mbele yake ukaseme mbona unasemea huku mitandaoni

Banii israil waliwahi kumkaripia Firauni?
Hujui lolote ww mbele ya kuheshimu mtawala

Anafikiri hiyo Hadith ya Mtume (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) inawahusu keyboard warriors, wazee wa maandamano na wanao wasema watawala katika mimbar na majukwaa.

The Messenger of Allāh (salallāhu ʿalaihi wassallam) made it explicitly clear that it is forbidden to speak openly against the Muslim ruler. It is the Sunnah to advise him in private, regardless of his tyranny:

مَنْ أَرَادَ أَنْ يَنْصَحَ ‌لِذِي ‌سُلْطَانٍ فَلَا يُبْدِهِ عَلَانِيَةً، وَلَكِنْ يَأْخُذُ بِيَدِهِ فَيَخْلُوا بِهِ، فَإِنْ قَبِلَ مِنْهُ فَذَاكَ، وَإِلَّا كَانَ قَدْ أَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ

“Whosoever wishes to advise the Ruler, let him not do so openly. Rather he should take him by his hand into seclusion [and advise him]. If he accepts that from him, it is in his favour, and if he does not accept, he has fulfilled his duty.” (Imām Ahmad in al-Musnad, no. 15359, As-Sunnah Ibn Abī ʿĀsim, no. 1096-1097 with Shaikh Al-Albānī’s checking – an authentic hadeeth)

Mkuu mbona kama ikiwa hivyo unawapa roophole watawala ya kufanya lolote kisa raia mnafata dini hamuwezi wakemea?

Bila spana bungeni enzi zile raia wasingejua ufisadi unaofanywa na viongozi wao, bila kelele za watu mitandaoni baadhi ya watu waliotekwa na kupatikana wasingepatikana kama wengine wengi.

Japo wewe unahisi italeta taharuki na fujo ila inasaidia sana watawala kutotumia madaraka yao hovyo.

Sasa wote tukiwa kama kondoo ni hatari zaidi mkuu, tutaandaa madikteta na kwa jinsi nchi ilivyo na vyeo vingi raia watapata tabu mno tukienda kikondoo namna hiyo. Kila kiongozi kwa uwezo wake ataweza kumpoteza au kumchezea rafu yeyote na asifanywe chochote kisa ni kiongozi.
 
Uislamu una majibu ya kila kitu na uneweka njia zake katika kila kitu na inatazama maslahi na Mafisadi katika kupima mambo.
 
Kwa hali kama ya hapa Tz, unasuluhisha vipi hili?

Maana bila kelele madhara yanaweza kua makubwa zaidi ya haya, si mara moja au mbili watu kutumia madaraka vibaya, wakiachwa kwa namna hiyo si twafwa??
 
Mkuu mbona kama ikiwa hivyo unawapa roophole watawala ya kufanya lolote kisa raia mnafata dini hamuwezi wakemea?

Bila spana bungeni enzi zile raia wasingejua ufisadi unaofanywa na viongozi wao, bila kelele za watu mitandaoni baadhi ya watu waliotekwa na kupatikana wasingepatikana kama wengine wengi.

Japo wewe unahisi italeta taharuki na fujo ila inasaidia sana watawala kutotumia madaraka yao hovyo.

Sasa wote tukiwa kama kondoo ni hatari zaidi mkuu, tutaandaa madikteta na kwa jinsi nchi ilivyo na vyeo vingi raia watapata tabu mno tukienda kikondoo namna hiyo. Kila kiongozi kwa uwezo wake ataweza kumpoteza au kumchezea rafu yeyote na asifanywe chochote kisa ni kiongozi.
Ikiwa njia ni kukiwasha kila Kiongozi akija afadhali yule aliyotoka na mkapewa viongozi waovu kama 7 mfululizo utakiwasha mara ngapi ?

Kuna nchi Africa Magharibi hapiti mwaka wanapinduana yaani kiongozi hadumu na hiyo ndio waliona solution je walifanikiwa kupata viongozi Bora na utulivu kupitia njia hiyo ?

Je , unajua gharama za machafuko ?
 
Kwa hali kama ya hapa Tz, unasuluhisha vipi hili?

Maana bila kelele madhara yanaweza kua makubwa zaidi ya haya, si mara moja au mbili watu kutumia madaraka vibaya, wakiachwa kwa namna hiyo si twafwa??
Kwanza tuanze na hili , hali gani ambazo unaziona hazipo sawa hapa Tz zitafutiwe tiba ?

Kumbuka huyu anayesemwa sasa CDM na mengine walikuwa wanamsifia na kusema Bora Magu kaondokana walikuwa wanamponda Magufuli kama ndio chanzo Cha matatizo yote Duniani . Je , vipi baada ya mchawi wao Magu yameisha ?
 
Back
Top Bottom