Lakini urusi amekua akinunua silaha nyingi tu kama Drones na makombora kutoka hiran na China
We jamaa chuki inakupotezea weledi kwenye uchambuzi wa baadhi ya mambo. Hivi Urusi analazimika vp kununua system ambazo ni inferior kwa alizonazo? Hivi ukanunua AD systems za Mchina wakati mchina mwenyewe anategemea ujuzi wako kutengeneza baadhi ya siraha zake under license? Mbona Urusi wananunua Shaheeds za Iran ila pia juzi kati hapa si jeshi la Akhmat ya wa Chechniya si wamenunua ShaanXi Tiger 4×4 za wachina. Au kwako hadi inunuliwe AD ndo unaelewa?
Urusi ananunua maji yakifika shingoni, sio kwa mahitaji ila kwa kulazimika. Yani badala ya kinga yeye anatafuta tiba.
Hizo Tiger 4×4 wamenunua sababu ni cheap na widely available, production ya factories za Urusi haifikii demand waliyonayo kipindi hiki.
Shaheed walinunua sababu hawakuwa na suicide drones za uhakika na hawakuwa na mass production, ilikuwa concept mpya kwao wakati kwa Iran ni concept ya miaka mingi. Mpaka baadae Urusi ilivyoendeleza na kutoa drones kama Lancent.
Hao kina Ujerumani, Israel, Marekani wananunua kipindi hawana vita. Wanafanya assesment wanaona silaha gani ina performance nzuri wananunua, hawasubiri zao zifeli au production isifike mahitaji ndio wachukue chochote kinachopatikana kwa allies.
China ina uwezo wa kutengeneza meli kuizidi Urusi, makombora, smart munitions ndio usiseme, drones kuanzia za kiraia hao DJI na za kijeshi, microchips na vitu vingi ambavyo Russia anasuasua.
Kwenye radars Wachina wana hatua nzuri sana, kwenye hypersonic wako mbali, kwenye stealth technology mbali. Kitu kimoja muhimu ambacho bado wako nyuma kwa Mrusi ni turbofan engines za jet fighters.
China ina hela, ikiona superior product inaagiza mkigoma kuuza hilo ni jambo lingine. Iko radhi inunue teknolojia ya civilian version ya kifaa cha kijeshi kama hizo European heavy trucks au ifanye licence production.
Urusi hajui kitu kwenye civilian technology ambayo ndio iko wazi, alafu kuna watu wanaamini anajua sana kwenye military tech ambayo ni ngumu zaidi. Kompyuta, simu, magari, kamera, TV sets, ndege za kiraia na tech products nyingine Urusi inategemea mataifa ya nje na hiyo China kwa wingi. Ghafla kwenye jeshi ndio eti Urusi inajua kila kitu mpaka maji yafike shingoni ndio iwafikirie Iran na China.