Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UJINGA ULIOWAGHARIMU WENGI KWENYE MAISHA!
Anaandika, Robert Heriel.
Kila binadamu anakiwango chake cha ujinga, hata Yule unayemuona anaakili Sana ujue anakaujinga kake.
Sasa unaweza ukawa mjinga lakini kamwe Epuka kuwa MPUUZI, mpuuziaji ambaye baadaye itakufanywa uitwe mjuaji wakati hukuwa unajua. Mjinga ajifanyaye anajua huingia katika kundi la wapumbavu, hivyo ndivyo ilivyo ni Sawa na mwerevu mwenye upuuziaji nayr huingia kwenye kundi la wapumbavu.
Na hii sasa ndio orodha ya ujinga ambao ulisababishwa na upuuziaji uliowagharimu watu wengi Duniani;
1. "Kusoma sio kufanikiwa maisha" wakati Vijana wengi walipoambiwa wasome baadhi Yao walikuwa wakisema maneno hayo au Kuambiwa maneno hayo na watu walioshindwa shule. Wapo waliokuwa wakisema kimoyo moyo.
Usiposoma lazima utumie nguvu kuyamudu maisha hasa ukiwa umetoka familia Masikini. Tena utatumia nguvu na bado utalipwa Kama kibarua. Hii ni Kwa sababu huna tofauti na mnyama Kama punda au ng'ombe ambao nao hutumia nguvu tuu.
Lakini ukitumia akili maslahi yake huwa ya juu.
Vijana Kama huna elimu ni Bora ujiajiri Kwa kweli. Maana wewe ni kibarua na wala haupo kundi la Wafanyakazi. Mshahara wako utakuwa kidunchu wa kula tuu.
Ni Bora ukatembeze karanga, ukauze henge, mkaa, ukawa bodaboda au konda na kazi zingine zisizohitaji elimu kuliko uajiriwe maana utalipwa posho tuu.
2. "Uliona wapi pipi ikaliwa na maganda yake?"
Wengi Kwa ujinga walitumia Kauli hiyo wakaishia kupata UKIMWI, kupata mimba wasizokuwa wamezitarajia. Tena walioolewa au kuoa wakauleta UKIMWI nyumbani na kuiangamiza familia.
3. " Siwezi kujenga na kuishi kijijini Mimi" "Hivyo viwanja vipo mbali na mji"
Wengi wamejikuta wakizeeka pasipo kuwa na Nyumba za kuwastiri wao na watoto wao Kwa akili za kijinga jinga.
Hawakujua kuwa hata hapo wanapopaita Mjini palikuwa kijijini zamani, tena hapakuwa na Nyumba hata moja.
Hujikuta wakiishi maisha Yao Kwa taabu hasa umri ukiwa umeenda, mwishowe huwatesa watoto.
4. " Ngoja nikupe/niolewe naye nitambadilisha au atabadilika"
Wengi wamejikuta wakiyaharibu maisha Yao Kwa ujinga na upuuzi. Unakuta limwanamke ni kahaba, halina sehemu za siri, karibu wanaume wote WA mtaani wanamjua sehemu zake nyeti. Ati unamuoa alafu unahama mtaa, wewe si CHIZI tuu! Malaya hata umpeleke mbinguni ataleta umalaya wake Kwa Malaika. Hujiulizi Kwa nini Huko mbinguni hawataki Malaya, hujiulizi! Sehemu haimbadilishi mtu.
Mtu Kama anatabia mbaya achana naye, tafuta wenye tabia nzuri mbona wapo.
Au unakuta limwanaume haliheshimu wanawake, linazalisha hovyo, linapiga wanawake, linatukana tukana hovyo matusi ya aibu, alafu Kwa ujinga wako unaolewa nalo Kwa matarajio ya kumbadilisha, unaumwa wewe! Mtu kujibadilisha mwenyewe ni shughuli pevu sembuse wewe umbadilishe.
Ndio yake baadaye linatukana wazazi wako, ndugu zako, wengine wanafikia hatua ya kutoka na Dada yako au Mama yako.
Alafu unamlaumu, unalaumu nini wakati wewe ndio ulikuwa mjinga!
Acha Shetani waoane na mashetani.
Malaika waoane na Malaika!
Majini Kwa Majini
Walevi Kwa walevi
Malaya Kwa Malaya n.k.
5. " Acha Nile ujana, nitaolewa tuu"
Asilimia 90 ya wanawake ambao wanaumri wa miaka 30+ waliringa kuolewa na wanaume Fulani Kwa sababu kadha wa kadha!
Wengine walijiona bado wadogo, wakati mwanamke mwenye miaka 20 tuu tayari ni mtu mzima anaukaribia uzee. Akishafikisha 30 tayari keshaondoka kwenye soko.
Ujinga wa baadhi ya wanawake kufikiri Kama wanaume ndio inawagharimu leo hii. Huwezi kuhangaika kutafuta mchumba ukiwa umezeeka, labda utafuta mshirika wa kusogeza siku ziende.
Raha ya Mke umfaidi akiwa mbichi, mtoto bado ngozi inateleza bila hata Mafuta.
Sasa sijui Nani aliwadanganya dada zetu kutafuta kuolewa wakati Sura zao zikiwa zinadondoka chini, na ngozi zikiwa tepetepe!
Anyway!
6. "Pesa hainunui furaha"
Wanaume wenye mtazamo huu huishia kuumia na kugharamika maradufu. Huchukulia mambo rahisi. Hivyo hawawekezi nguvu zao kwenye utafutaji. Mwishowe huishia maisha ya kulalamika.
Mwanaume asipokuwa na pesa hawezi kuwa na nguvu ndani ya Nyumba, na hapa sisemi uwe na pesa nyingi Sana hapana, nazungumzia pesa inayokutosha wewe, Mkeo, na watoto.
Ukikosa hiyo basi Mkeo atakusumbua, asipokusumbua yeye basi Vijana wa mtaani watamsumbua, wasipomsumbua yeye basi watasumbua vibinti vyako vikiwa hata havijafika sekondari wataanza Kula embe na chumvi.
Uchunguzi wangu unaonyesha umasikini WA wasichana wengi husababisha kujiingiza katika mapenzi wakiwa wadogo Sana. Kwani hudanganywa na vijana wa mtaani Kama bodaboda, wauza magenge ya chipsi n.k.
Watoto wengu huiga maisha ya wazazi wao. Hupenda kuona kile unachowashauri wewe mwenyewe ulikifuata. Lakini ni watoto wachache Sana wanaofuata maneno ya wazazi pasipo kuangalia uhalisia wa wazazi.
Mtoto anakuwa inspired na Mzazi Kwa uhalisia sio maneno. Na ndio maana ukiwa hujasoma na Masikini ni rahisi Sana mtoto kuwa Masikini na asiwe na Elimu.
Halikadhalika ukiwa umesoma ni rahisi Sana mtoto kuwa kama Mzazi wake hata usipomwambia mtoto anataka kuwa kama Mzazi wake.
Ndio maana inashauriwa mtoto umwonyeshee matendo zaidi kuliko maneno.
Kama hujasoma na ni Masikini Taikon atakushauri ufanye utakavyoweza uoe msomi na mtu mwenye kipato cha kueleweka Kwa faida ya watoto. Vinginevyo utakuwa unapoteza muda. Ingawaje wapo Exceptional ambao ni wachache Mno, tena wachache Sana.
7. " Dini sio tatizo, kila mtu atakuwa na dini yake, ilimradi tunapendana"
Ukiona uliwahi fikiiria kitu Kama hiki ujue wewe ni mjinga wa kiwango cha juu kabisa. Wengi imewagharimu walipoamua kufuata mtazamo huu. Dini humfanya mtu kuwa na Imani Fulani, Imani huleta falsafa, falsafa huleta Mtazamo wa mtu juu ya Maisha. Kama watu mnatofautiana mtazamo mtawezaje kuishi pamoja, Kama sio kujidanganya.
8. " Kuoa single mother sio tatizo, Inategemea na Mwanamke mwenyewe"
Wengi imewagharimu, tena Sana. Wengi Hufanya hivyo Kwa hisia tuu, tena hisia za kitoto ambazo mtu mwenye akili iliyotulia hawezi kufanya hivyo.
Kuoa tuu mwanamke kama Mwanamke ambaye Hana mtoto na hata hajawahi kumjua mwanaume inatakiwa mwanaume ujishike, uwe umekomaa sembuse mwanamke ambaye ni single mother.
Huwa nawashauri Vijana wadogo ambao ndio Kwanza wanaingia kwenye ndoa, wasiingie ndoani na single mother bali Watafute wanawake WA level zao ambao nao hawajawahi kuolewa.
Single mother wawaachie single father, au Wazee waliofiwa na wake zao, au wastaafu au wanaume wanaotaka kuongeza mke WA pili au watatu kuendelea.
Kanuni ni Ileile!
Mchanga Kwa mchanga
Komavu Kwa komavu
Zee Kwa zee au kuukuu Kwa kuukuu!
Sio mwanaume mchanga achukue mwanamke mkuukuu hiyo ni kutafuta matatizo tuu!
9. " Ninatetea na kusaidia Masikini na wanaoonewa, Mungu atamlipa"
Wengi imewagharimu, hakuna malipo ya hivyo ndugu zangu. Maisha ya mwanadamu ni Kama maisha ya wanyama Porini. Wapo swala wanaoonewa na kila mnyama na kila mahali watakapoenda wataonewa tuu. Ndivyo ilivyo Kwa maisha yetu. Kuna watu wapo Kwa ajili ya kuonea wengine, na wapo waliopo Kwa ajili ya kuonea.
Ukijifanya mtetezi unakuwa kundi la watakaoumizwa.
Aliyeumba hii dunia aliweka hivyo, na ndiye mwenye uwezo wa kuondoa na sio wewe.
Niliwahi kusema; Kama tunataka tusioneana Kama Watanzania basi itatupasa tuvamia mataifa mengine ili tuyapekekea uonevu wetu huko. Yaani tupunguze uonevu ndani ya nchi yetu.
Lakini huwezi kuuondoa uonevu pasipo kujua mahali pa kuupeleka.
Huwezi kuondoa Giza hapa ukadhani limeondoka hapana ulichofanya ni kulihamisha Giza kutoka kwako na kukupeleka sehemu nyingine.
Hata Mungu aliuondoa Uovu na Shetani mbinguni na kuutupa/ kumtupa Duniani.
Huwezi kuondoa takataka alafu usijue pakuzitupa utaishia kuchafua zaidi.
Kama hujanielewa basi.
Taikon nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam