Samahani sana mkuu, 'Sky...'
Ndugu Lissu anaharibu kuyaweka haya mbele. Hana sababu ya kuyatangaza haya, kwa sababu inajulikana, na yeye mwenyewe anajua fika kwamba haya ndiyo atakayofanyiwa; na pengine zaidi ya haya.
Tulichotarajia toka kwake, tangia alipoahirisha kurudi baada ya kuruhusiwa toka hospitali, ni kwamba muda huo angeutumia vizuri sana kujipanga vizuri kuwakabili hawa watu kuhusu mipango yote hiyo anayoizungumzia.
Mategemeo yalikuwa kwamba atakuwa yeye mwenyewe na familia yake na chama chake, wameweka mikakati madhubuti zidi ya maovu zidi yake.
Tulitegemea hii ingekuwa ni kazi na maandalizi ya kimya kimya. Tunatarajia kurudi kwake sio swali tena la kujadili na kupima upepo kama anavyofanya sasa hivi.
Ni lazima sasa akubali, amekwishakunywa nusu glasi, asiogope kuimaliza glasi nzima ya machungu.
Mwambie aachane na haya ya kuonyesha kulialia. Yeye alishapita ngazi hiyo, ni lazima aonyeshe ushujaa kwenda mbele.
Haya awaachie waTanzania wayapime wenyewe na kutoa uamzi sahihi.