Ujumbe kutoka Tundu Lissu kwa wote wenye mapenzi mema

Ujumbe kutoka Tundu Lissu kwa wote wenye mapenzi mema

Huu ni mtego amewatega CCM na kama watamweka ndani hapo watakuwa wanajivua nguo wenyewe pia hata jumuia ya kimataifa watajua ukatili unaofanywa na CCM....
Hata Mimi naomba wamweke ndani ili tupate point 3 kipindi cha campaign maana CCM Kwa UJINGA wao mwingi wataingia Kwenye mtego
Aisee... Kwamba ccm wanaogopa wazungu?

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Stori hizi za kila siku....jamaa yenu kaona katangaza nia ila kapotezewa balaa..hata chadema nao wamempotezea wako bize kumpa airtime gambo
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Lisu sasa hivi ni takataka tu mbele ya Membe kwa wanachadema linapokuja suala la urais.

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
na #TUNDU_LISSU

Kuhusu sarakasi za Mahakama ya Kisutu, nina haya ya kusema;

Acheni hofu. Kama nitakamatwa na kuwekwa mahabusu, hilo litakuwa ni jambo jema kuliko jambo lingine lolote Magufuli na watu wake watayatendea mapambano ya kudai demokrasia katika nchi yetu.

Wakifanya hivyo basi kampeni yote ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu itakuwa juu ya kukamatwa kwangu.

Ni hivi: kabla ya September 7, nilikuwa na kesi 6 za jinai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Nilikuwa sijawahi kukosa kwenda mahakamani kuhudhuria kesi hizo. Sijawahi kuogopa kesi zao za kijinga.

Kitu pekee kilichonifanya niache kuhudhuria kesi ni kile ambacho dunia nzima inakifahamu. Nilishambuliwa na kujeruhiwa vibaya na kusababisha niondoshwe nchini kwa ajili ya matibabu.

Walionishambulia na waliowatuma, kuwalipa na kuwawezesha hadi sasa wanaitwa 'watu wasiojulikana.' Waliotakiwa wanitibu kwa mujibu wa sheria za nchi yetu walikataa kunitibu. Badala yake wakanifuta Ubunge kwa visingizio vya kijinga tu.

Sasa nikirudi nchini kwa hiari yangu baada ya miaka mitatu ya kujihangaikia mwenyewe wanikamate na kuniweka gerezani kwa visingizio vingine vya kijinga.

Hilo litakuwa jambo jema sana. Itabidi wawaeleze wananchi wa Tanzania na waieleze dunia inayofahamu mambo haya kwa nini wamefanya hivyo. Na watoe maelezo hayo katikati ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge na waeleweke kwa wapiga kura.

Mimi binafsi nitafurahia sana wakifanya hivyo, maana hatutazungumzia kitu kingine chochote katika kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Tundu Lissu.
Arudi apambane na kesi zake aache longolongo. Na wenye saccos wameshasema hawampitishi kugombea Urais alie tu!
 
huyu jamaa kwa mipasho hana mpinzani, anaropokaga tu hovyo nadhani cdm haifundishi nidham kwa viongozi wao ndo maana wamejawa ujinga wa kutaka sifa ajili ya kuwafurahisha mabeberu
 
Mkuu mimi natofautiana nawe. Nadhani Lissu kasema haya ili kutuandaa Watanzania kiakili hasa wale ambao ni wanachama, wapenzi na mashabiki wa Chadema na wanaompenda Lissu ili TUSISONONEKE sana atakaporudi na kufikia lupango. Huo ni mchango wangu wa senti kumi Mkuu.
Sawa, lakini sio kwa namna hii ilivyowasilishwa hapa.

Hana kitu cha kufichaficha tena kwa waTanzania. Awe 'direct', azungumze nao na kutoa msimamo wake kikakamavu kama jemadari aliyekwishaonja vita na sasa yupo tayari kuongoza jeshi kikakamavu.

Lissu anayo sababu yoyote tena ya kulembalemba, baada ya kupitia yote aliyokwishayapitia?

Afanye mipango ya safari yake kurudi na aiweke wazi na jinsi alivyojiandaa kushiriki mapambano, ili watu wasiwe na mashaka juu yake.

Sasa hivi amekwishajitabiria yatakayompata, na hata wale waliokuwa wakimtegemea wanaanza kukubali hatma hiyo juu yake; kana kwamba ni yeye aliyeyasababisha yote!

Yaani hakuna mapambano tena!
 
Kule juu uliandika kiroho mbaya... "aje apambane na hali yake..".
Jamaa aliumizwa regardless na watawala au watu baki, na watawala wanakuwa katika upande wa lawama kwa sababu ya namna walivyoliendea jambo hili...
Sasa kwa upande wako ni manufaa gani unapata pindi haki ya mtu mwenye mawazo mbadala na ya kwako anapokandamizwa?
Hakuna roho mbaya hapo!!! Ni kweli apambane na Hali yake, mwana kulitafuta mwana kulipata, Sasa ulitaka apambane na Hali ya nani? Aje kumalizana na kesi zake huku hakuna mzungu ataekae beba mashtaka yake.by the way mwambie karibu nyumbani kumenoga kamamanda
 
Kwa bahati mbaya mahakama zinafanya kazi kisiasa na kutii amri za mtu kitu ambacho kimefanya mahakama zetu ziwe na sifa zote za Kangaroo Courts.
 
Back
Top Bottom