Umeandika jambo la msingi sana.
Kuoa ni zaidi ya kupata mke, kuoa ni kupata mwenza wa maisha, kuoa ni kupata mama wa watoto wako, kuoa ni kupata roll model wa Watoto wako.
Kuoa ni kuanzisha safari, safari usiyojua yaliyopo mbele. Unahitaji mtu imara zaidi ya mtu mrembo. Ukibahatika kupata mwanamke mrembo na imara hiyo ni advantage kwako.
Huwezi tu kukurupuka kuoa mwanamke kwa sababu ya sura na tako.
Mwaka mmoja Katika ndoa muonekano huwa hauna faida yoyote katika maisha ya ndoa.
Nikiangalia classmates zangu wa kike pale UDSM wale ambao walikuwa wa kawaida wote wapo kwenye ndoa. Wale warembo, waliokuwa wanajiona naona bado wanakula maisha huku umri unaenda bila mahusiano imara.
Inawezekana ukawa mrembo, mwenye shape na bado ukawa mwanamke imara na mwenye kujua maisha halisi.
Wapo wadada warembo, wenye miili inayovutia ambao waliamua kwa makusudi kuona maisha ni zaidi ya sura zao nzuri na maumbo yao mazuri.
Ukitaka kufanikiwa, uwe mwanamke au mwanaume kaa ukijua kuwa maisha ni zaidi ya muonekano wako.
Ngoja niwahi kazini watanzania wenzangu.