Ujumbe makini kwa mabinti toka kwa baba wa kiroho - "Mabinti msijilazimishe kwa wanaume"!

Utafiti kiwango cha SGR! hatari nanusu aisee!
 
Wanaume kwenye kuoa wako makini jamaniiiii yaani hata wale wanaume wabovu kabisa unakuta anachagua mwanamke makini ajabu.. na baada ya hapo ndio waolewaji ndio wanakuja kushtuka na kuishia kulia na kusaga meno😂😂😂
Katika moja mafundisho yake ambayo yapo YouTube marehemu mchungaji Mitimingi anasema mwanaume na mwanamke wanapoingia kwenye ndoa, ni mwanaume ndio mwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa au ya kuharibikiwa kwenye maisha. Ili ni somo kubwa sana.
 
Kabisa hakuna mtu anaependa azae na kilaza.
 
Umeandika jambo la msingi sana.
Kuoa ni zaidi ya kupata mke, kuoa ni kupata mwenza wa maisha, kuoa ni kupata mama wa watoto wako, kuoa ni kupata roll model wa Watoto wako.
Kuoa ni kuanzisha safari, safari usiyojua yaliyopo mbele. Unahitaji mtu imara zaidi ya mtu mrembo. Ukibahatika kupata mwanamke mrembo na imara hiyo ni advantage kwako.

Huwezi tu kukurupuka kuoa mwanamke kwa sababu ya sura na tako.
Mwaka mmoja Katika ndoa muonekano huwa hauna faida yoyote katika maisha ya ndoa.

Nikiangalia classmates zangu wa kike pale UDSM wale ambao walikuwa wa kawaida wote wapo kwenye ndoa. Wale warembo, waliokuwa wanajiona naona bado wanakula maisha huku umri unaenda bila mahusiano imara.

Inawezekana ukawa mrembo, mwenye shape na bado ukawa mwanamke imara na mwenye kujua maisha halisi.

Wapo wadada warembo, wenye miili inayovutia ambao waliamua kwa makusudi kuona maisha ni zaidi ya sura zao nzuri na maumbo yao mazuri.

Ukitaka kufanikiwa, uwe mwanamke au mwanaume kaa ukijua kuwa maisha ni zaidi ya muonekano wako.

Ngoja niwahi kazini watanzania wenzangu.
 

Uwe na siku njema affinitytz
 
Wanaume kwenye kuoa wako makini jamaniiiii yaani hata wale wanaume wabovu kabisa unakuta anachagua mwanamke makini ajabu.. na baada ya hapo ndio waolewaji ndio wanakuja kushtuka na kuishia kulia na kusaga meno[emoji23][emoji23][emoji23]
Umenena vya rohoni na ukweli Mama D. Mwanaume anayetaka kutengeneza familia bora lazima apate mke sahihi na bora. Mke ndio mtendaji mkuu wa taasisi sasa warembo wengi wao wanaangalia sana maisha ya anasa. Ukiangalia wadada wazuri wengi sana wameangukia katika mikono sio salama na kuzalishwa akina Junior wengi sana kutokana na kuzaa na waume za watu ambao wamewarubuni. Kuoa mke sahihi ni sawa na kutafuta shamba lenye uhakika wa kukuletea mazao mengi na mazuri. Tofauti na shamba la kuweka mbolea kila msimu.
 
Uko sahihi mama D wanaume hawa sio watu anakutumia weeee ila anakuja kuolewa mwingine(wenyewe wanaita waifu matirio)
Kama mwendazake wa arusha alietaka kuoa malaya wa bungeni viti maalum
 
Nimeelewa, maana nilikuwa namuuliza huyu bwana kwanini kaamua kunichukua Mimi ilhali anao uwezo wa kugonga celebrity wengi tu Tena wakali kinoma,,

Wanaume wako makini Sana katika kufanya maamuzi ya kuoa zaidi ya akili zetu wanawake tunavyofikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…