Vyovyote iwavyo hairuhusiwi. Pale UDSM vyama vya kufa na kuzikana vinavyohusisha makabila vilipigwa marufuku kwa madai kuwa vinahamasisha ukabila.
Vyama vya siasa ama NGO zenye mrengo wa kabila havipewi usajili.
Amka
Mbona wamaasai wanajificha nyuma ya mgongo wa wafugaji lakini hatuoni wakichanganyika na wafugaji wa Kinyaturu, kimbulu, kimang'ati,kisonjo,kigogo, n.k. ?
Ukabila utaisha pakiwa na uhuru wa kisasa na utawala Bora. Utawala Bora hua unatabia ya kumaliza harakati zote bila kutumia nguvu.
Katiba mpya iweke uhuru wa kisiasa ili anayeona anaweza kuleta mabadiliko apitie kwanye vyama na awashawishi hata kama ni watu wa nyumbani kwake lakini tutauona maono yake Kwa Taifa na tutamuuliza maswali kwenye midahalo.
Hata ugaidi unashamiri kama hakuna demokrasia. Wekeni demokrasia nzuri ili kila mtu awe huru kuja na mrengo wake. Kuna watu wanavutiwa sana na Namna wasukuma wanavyoongoza nchi na kusimamia rasilimali za Nchi. Lakini wao nao wanaona Kuna harakati za kuwazuia kabisa wasije wakagusa Tena uongozi wa juu. Lakini hao wanaowazuia wanawazuia Kwa lengo la kuiba Sio Kwa lengo jema Kwa Taifa.
Sioni Kwa Nini wakatazwe kufanya vikao watu wa Kanda hiyo ya kisukuma.
Ukabila utakwisha wenyewe tujifunze Kenya.
Mara nyingi pakiwa na Chama Dume ndipo panapokuwa na mambo kama hayo ya ukabila ,uchifu,udini , ukanda ,uzanjibari na Utanganyika ,upemba na uunguja n.k. Yote ni watawala wanacheza na akili za watu kutengeneza kura. Huenda hata hicho kikao kitatumika kutafuta kura za watu wenye madaraka. Pale Namuona Cheyo. Cheyo ni Wakala wa watawala tangu Mkapa.
Demokrasia ya kweli inaua Ukabila