😅😅😅mitano tenaAnyway, CCM hoyeeee, mitano tena
Somali situation is comming
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😅😅😅mitano tenaAnyway, CCM hoyeeee, mitano tena
😅😅😅wamisri na wayemeni wakitusikia tunahaha maji wanatushangaa ikiwa tumezungukwa na mito kibaoHata tende zinaota wametoboa miamba ardhini sisi tuko busy na politiki, shahidi analeta mahakamani ushahidi wa maganda ya risasi alizozitumia mwenyewe du!
HeheheeMbowe asipoachiwa basi mjiandae majibu haya mawili ya mafungo yenu:
Moja, mvua haitanyesha kabisa na ukame mkubwa utaiandama nchi na wengi wataathirika sana
Pili, mvua zitanyesha kubwa sana hadi kuharibu mazao, mali na kuchukua hata uhai.
The choice is yours
Gaidi hawezi kupangia watuMbowe asipoachiwa basi mjiandae majibu haya mawili ya mafungo yenu:
Moja, mvua haitanyesha kabisa na ukame mkubwa utaiandama nchi na wengi wataathirika sana
Pili, mvua zitanyesha kubwa sana hadi kuharibu mazao, mali na kuchukua hata uhai.
The choice is yours
Inauma sanaHawa Wachina wamebeba sana magogo kwa kusaidiwa na watu wenye tamaa za hela bila kujali madhara yake ya sasa na baadae
Hawa ni wa kushughulikiwa na kufungwa kabisa ila ndio hivyo tena mnabebana na hakuna wa kumkamata mwenzie
Inanyesha sasa[emoji38][emoji38][emoji38]
Kuna kitu unatumia mkuu? acha mara moja!Mkuu, kwa hiyo jangwani mvua hazinyeshagi.
Tupo hapa 2030 utasikia uzalishaji wa umeme upo chini ya kiwango kotokana na kupungua kwa maji sababu hasa ni ukame unaochangiwa na ...hapo utasikia ufagaji usio zingatia utanzaji wa mazingira ukataji miti hovyo na shughuli za kibinadamu kweny misitu ya asili hapa ndo utajua kuna viongozi waliopita kichwani palikuwa patupu..Aliyehoji ana matatizo ya akili; hiyo miti milioni 2 imekatwa kwenye chanzo cha maji?
Maji yote ya mto Rufiji yanatokea Iringa, Morogoro na Njombe
Tanzania nchi huru inajipangia shughuli zake yenyewe kwa manufaa ya vizazi vyake bila kuathiri uharibifu wa mazingira.
Hamzungumzii uharibifu unaofanyika kwa shughuli za kibinadamu kama kilimo zinazofanywa na wafanyabiashara kwenye mito kama Ruvu, Ngerengere, Wami kuanzia Kilosa, Dakawa, Dumila, Kilombero, Ruaha mkuu, Kilombero, Lumemo na Laegu wa Njombe
CC SYLLOGIST!Wakati tunatangaza kuharibu miti zaidi millioni mbili tulimuomba Mungu? Au wenzetu hamjui umuhimu wa miti?
Haya mlipanda miti mingapi? Leo hii mnataka kufunga eti Mungu alete mvua, you guys! Mko Sawa kweli?
Tusimdhibaki Mungu ana kazi za msingi sana kuliko hii, yaani tukate miti kwa mbwembwe vile kisa mnajenga bwawa? Liko wapi? Mtalijaza mikojo Wallah.
Anyway, CCM hoyeeee, mitano tena
=====
Zaidi ya miti milioni 2 kukatwa kupisha mradi wa umeme Tanzania
16 Mei 2018
Ukataji wa miti zaidi ya milioni 2 ni maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la kuzalisha umeme wa megawati
2,100
Serikali ya Tanzania inajiandaa kukata miti eneo la ukubwa wa asilimia tatu ya hifadhi ya taifa Selous.
Mapema asubuhi ya Jumatano, serikali ilipokea maombi ya zabuni ya kukata miti hiyo kutoka kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi yaliyoonyesha nia ya kutekeleza mradi huo wa kukata miti.
Serikali inasema ukataji huu wa miti zaidi ya milioni 2 ni maandalizi ya ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la kuzalisha umeme wa megawati 2,100 utakaojengwa ndani ya hifadhi hiyo.
Hatua hii inaongeza ukosoaji dhidi ya serikali kutoka kwa wanaharakati wa mazingira ambao tangu serikali kutangaza nia ya kujenga mradi huo wa umeme, wamekuwa wakipinga mradi huo kuwa ni hatari kwa wanyama pori na viumbe wengine waishio katika hifadhi hiyo ya Selous, ambayo inatambuliwa pia kama urithi wa dunia.
Wanamazingira watoa tahadhari kuhusu mpango wa serikali
Ni wazi kwamba serikali ya Tanzania imedhamiria kuendelea na mradi huu wa kufua umeme, huku kukiwa na ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa mazingira, ambao wanaelezea wasiwasi wao kuhusiana na athari za hali ya mfumo wa kiikolojia ndani ya hifadhi ya Selous.
Hata hivyo hivi karibuni kuhusu mradi huo Rais John Magufuli aliweka wazi kwamba, serikali yake haitakwamishwa na ukosoaji wa aina yoyote ya kimazingira katika kutekeleza mradi huu mkubwa wa umeme.
Rais alisistiza kuwa wakati serikali yake inatekeleza sera ya viwanda,mradi huu wa umeme,ni muhimu zaidi kufikia malengo hayo.
Mtendaji mkuu wa wakala wa misitu Tanzania Profesa Dosantos Silayo ameiambia BBC sababu za kuuzwa kwa miti itakayo katwa kwenye hifadhi hiyo kupisha mradi huo.
''Sasa serikali imeona si vizuri kuiondoa miti katika hali ya kuiharibu inaweza kuwa na thamani, serikali imeamua kuitoa kwa utaratibu ambao utaiwezesha iuzwe kwenye makampuni mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya kutengeneza samani ndani na nje ya nchi, hii si biashara, na kwa kweli haijawa nia ya serikali kufanya uharibifu kwenye hifadhi zake''.
Hata hivyo Mwanasheria wa mazingira Dokta Rugemeleza Nshala amezungumzia ni hatua gani za muhimu kuzingatiwa katika utekelezwaji wa mradi huo.
''Ni kitu ambacho kinapaswa kitekelezwe kwa umakini mkubwa kwa sababu eneo la hifadhi na bado lile eneo wanalotaka kukata miti bado halijatolewa kutoka eneo la hifadhi na ni eneo ambalo ni la urithi la dunia.Umeme unahitajika na mazingira yanahitajika.mazingira yakiharibika hasara ni kubwa zaidi''.
Kwa sasa Tanzania inayokadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 50,inazalisha kiasi cha megawati 1400 tu za umeme kiwango ambacho hakikidhi mahitaji ya nishati ya umeme ya nchi.
Mradi huu mkubwa wa umeme unatarajiwa kuzalisha kiasi cha megawati zaidi ya 2000 za umeme ili kuimarisha mahitaji halisi ya umeme.
Chanzo: BBC
Tupo hapa 2030 utasikia uzalishaji wa umeme upo chini ya kiwango kotokana na kupungua kwa maji sababu hasa ni ukame unaochangiwa na ...hapo utasikia ufagaji usio zingatia utanzaji wa mazingira ukataji miti hovyo na shughuli za kibinadamu kweny misitu ya asili hapa ndo utajua kuna viongozi waliopita kichwani palikuwa patupu..