Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Mzazi aliuliza walimu huyo kijana alifanya kosa gani?Awali ya yote napenda kuushukuru uongozi wa Jamii Forum kwa kuendelea kuruhusu kufichua maovu yanayoendelea kutendeka katika jamii zetu.
Kuna ukatili wa watoto (wanafunzi unaoendelea katika shule ya binafsi (Experancia) iliyoko wilaya ya Sengerema.
1. Watoto wanapatiwa adhabu zenye kuwazidi uwezo ikiwa ni pamoja na bakora maeneo yasiyo sahihi na zenye kuwazidi uwezo kulingana na umri wao.
2. Watoto wa kike kuingiliwa na Mkurugenzi wa shule husika kwa zamu na baada ya hapo kuwapatia vidonge vya kuzuia ujauzito (P2), na inasemekana kwa bahati mbaya kuna mwanafunzi aliwahi ingiliwa na kusababishiwa ujauzito na baada ya hapo zikafanyika jitihada za kuutoa huo ujauzito 😭💔.
Ninaomba uongozi wa Jamii forum tuwasaidie watoto wetu jamani, dunia sio mbaya ila Binadamu tumegeuka wabaya kuliko hata wanyama wenyewe😭😭. Dunia imekuwa sio mahala salama tena.
Dkt. Gwajima D tusaidie kuwaokoa watoto wetu.
Hizi ni picha zilizotumwa na mzazi baada ya kwenda kumsalimu mwanae na kukuta khali isiyo ya kawaida kwa watoto.
View attachment 3125656View attachment 3125657View attachment 3125658View attachment 3125659
Isijekuwa mnasagiana kunguni na kuwekeana mizengwe ya kibiashara hapa.
Mwanafunzi akilambwa mboko, siwezi simama moja kwa moja na kulaumu, lazima niuchimbue undani wa kisababishi kwanza.
Mbona hatujaona foleni ya picha ya pamoja ya waathirika walalamikaji kama jambo hilo linatendeka kwa wanafunzi wengi/wote.
Na kwa nini uoneshe mgongo bila sura yake kama jambo hilo ni la kiuonevu?
Je kama picha ni ya kuokoteza ili itumike kutengenezea fitina hapa?
Toa maelezo ya kina pamoja na picha zenye kueleweka ili tuweze kulipima jambo hili.