Zanzibar waliojiondoa katika muungano kwa katiba ya 2010 hukusema lolote na hata sasa huoni kama ni tatizo.Mkandara;9406994]Tukiendekeza fikra hizi hapa hapatakuwa na Muungano kabisa na mtakuja nambia maana nashukuru Mungu kanijaalia kuona mbali.
Haya ungeyasema wakati JK na Karume wanaruhusu katiba ya znz kuwa juu ya JMT tungekuelewa. Leo muungano ushavunjwa kwa kuanza na katiba, halafu unatisha watu kuwa nchi itasambaratika. Mbona haijasambaratika wakati katiba inavunjwa.Mkandara: Na hizi mbinu za UKAWA ni kupingana na CCM tu, kwa sababu wanakisia CCM wanalao jambo na kwa nini wanaibembeleza Zanzibar kumbei vijana hawa hawaelewi uzito na nini hasa maana ya Muungano wa nchi.
Watazame Ukraine na Urusi kinavyowaka, Watazame kilichofuatia Ethiopia na Eritrea na majuzi Egypt. Hii yote inatokana na wanasiasa wachache kuchochea moto wa Kisiasa hasa kwa kutumia katiba ya nchi
Hebu eleza vita itatokeaje, maana sioni vita labda mwenzetu unaiona.Hakuna hatari kubwa ya kuvunja muungano nahata kusababisha vita ikiwa swala la Muungano litakuwa sehemu ya Katiba kwa sababu katiba huundwa baada ya kupatikana NCHI ama TAIFA. hivyo mwongozo huo unasimamia haki za wananchi wake, unaweka shera dhidi ya wahalifu, wahaini, miiko na maadili sii kwa viongozi tu hadi wananchi kulingana na mila na tamaduni zao
Una maana katika makundi CCM nayo ni kundi na inapaswa kutetewa kama makundi ya akina mama na walemavu.Kilichonichosha zaidi ni pale wajumbe wengi wa UKAWA wanapofikiri kwamba dhamana walopewa ni kutoa mawazo yao japo wamechaguliwa toka ktk vikundi vya kijamii. Hawajui kama wapo pale kutetea haki za vikundio vyao, kusimamia mawazo ya wengi toka ktk makundi yao bali wanachojua wao ni MAWAZO BINAFSI yaani kila mtu aseme anavyoona yeye
Muungano wetu na Marekani una historia iliyolingana? Katiba za Marekani na Tanzania zimeandikwa katika muundo sawa.Mkandara: mbona Muungano wa Marekani una miaka zaidi ya 200 na wameendelea kutushinda sisi kwa kila kitu..Hadi sasa hivi sijaona hoja ya maana kabisa zaidi ya wajumbe wote kupingana kwa jina la chama.
Marekani ina kiti kimoja UN. Canada ina kiti kimoja UN.Mkandara: Hivi kweli tunaweza kuwa na shirikisho lakini kiti kimoja UN, ama itabidi kila nchi iwe na kitu chake kama ilivyo Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Na hata kama tutakuwa na kiti kimoja hawaoni kama kitakachofuatia ni madai ya kila nchi kuwa na kiti UN maana tayari nchi hizo zina shirikisho tu? na wasivyo elewa umuhimu wa Muungano wanazungumzia mifano ya EU kama mfano bora! nani kawaambia muungano wetu ni sawa na ule wa EU ama tukiwa na shirikisho kama hilo tutakuwa wamoja zaidi..
ZNZ wanatuchukia kwa sheria za uhamiaji, ukaazi na ajira. Hilo hulizungumzii unachoona ni tatizo ni pale Tanganyika inapotajwa. Wanajamvi wangekuelewa kwanza kwa kukemea uchafu wa znz halafu ueleze point.Na sijui kama hawa watu wamewahi kutembelea nchi za EU hasa zilizoendelea na uchumi mzuri wajue jinsi gani wananchi wanavyobaguana na kuchukiana na wageni kufuatia sheria tu ya Uhamiaji toka nchi jirani ambao zamani hawakuwa na fursa hiyo. Ati wananchi wengi wanaunga mkono shirikisho! wananchi hao ni kina nani kama sii kina Jussa na Hizbu yao! mimi sikubaliani kwa mengi na utawala wa CCM lakini ktk hili sintowaunga mkono UKAWA hata kwa mijeledi!
Ni nyie mnao amini Zanzibar hawataki Muungano wakati tunayaona Bungeni ni kina Jussa na rasimu nzima imeandikwa kwa kuchukua mawazo ya kina Jussa. Mara zote ktk maandishi yangu nimekuwa nikitenganisha kundi la Maalim Seif/Jussa na lile la Wazanzibarkwa sababu nawajua tofauti zao. Wewe usojua ndio unachanganya madawa sana.Zanzibar waliojiondoa katika muungano kwa katiba ya 2010 hukusema lolote na hata sasa huoni kama ni tatizo.
Nyerere alisema kama wznz hawataki muungano hatawapiga mabomu. Wewe unasemaje, wapigwe?
Ni wewe uliyesema takwimu za Warioba zina matatizo kwasababu wznz walitaka mkataba(kumbu kumbu zipo JF) vipi leo useme msimamo wa wznz wengi ni serikali 2.
Wewe mgumu sana kuelewa mkuu wangu. Purto Rico kuna tatizo gani? wao sio state ya Marekani hadi sasa, ni kama koloni tu au territory kama ilivyo Yukon kwa Canada, Falkland kwa UK. Hivyo huwezi kuifananisha na Zanzibar ambayo ni state ilounda mungano wetu. Kifupi Zanzibar kwa Marekani inakuwa ktk zile states 13 za mwanzo kuunda USA acha hata hizo 37 zilizofuatia.Muungano wetu na Marekani una historia iliyolingana? Katiba za Marekani na Tanzania zimeandikwa katika muundo sawa.
Kama Marekani hawana tatizo ya Puerto Rico yametokeaje?
Kwavile Marekani waliandika katiba ya wananchi, na sisi tunaandika kwa vyama, hivi huoni kuna tofauti ya miungano hiyo miwili? Je, unadhani ni sawa kulinganisha chungwa na Fenesi kwasababu tu yote yanaitwa Matunda
U
Mkuu wewe unataka majibu gani kama sii yale unayotaka kuyasikia. Unauliza swali wakti majibu unayo ama unataka kufahamishwa?..
Sasa ikiwa leo sales tax haitoki Znz kuchangia mfuko wa Taifa, unataka kusema maadam hakuna mchango huo ktk serikali 2, basi hawawezi kulipa tena hata kama Katiba mpya inasema wanatakiwa ila kwa mserikali 3.
Pili, Unaposema Znz asilimia 2/3 ya bajeti yake inatoka Bara hiyo bara wewe umeipata wapi ikiwa wewe unaidai Tanganyika ambayo haipo?
Wewe umetaka kujua bara tutaweza vipi kulivua koti la Muungano na nimekueleza kwa kirefu na yote yana maana kwa undani wake. Unapojenga Bandari Znz kwa fedha ya Jamhuri inaondoa koti kwa sababu itakuwa kwa mara ya kwanza serikali ya Jamhuri imejenga miundombinu Znz. Na kama umefuatilia ilani ya JK ktk kuadhimisha sikukuu ya Muungano kawaahid Znz kuwajengea miradi mikubwa ambayo hadi sasa kelele nyingi zimeondoka. Wazanzibar wengi wamerudi ktk kuikubali serikali 2 na sii kama ilivyokuwa awali.
Kuhusu Bajeti, nachoweza sema mimi pato lolote lililopo ktk mfuko wa Taifa ni pato letu sote bara na visiwani hivyo mipango yoyote ya maendeleo ktk mfuko huo lazima uzihusishe nchi mbili na sii kugawana madaraka ya Urais na Umakamu. Wananchi wanataka kuona maendeleo na sii Hamad kapewa cheo gani ama Znz imekuwa na bendera gani..
Hivyo hata kama 2/3 ya bajeti ya Znz Inatoka bara (Serikali ya Muungano), ndivyo hata serikali za Marekani, Canada na Uingereza hutegemea fedha toka mfuko wa Muungano (serikali kuu) kuendesha shughuli za nchi zao. Mfano:- State ya New York (Nchi) hutegemea fedha za Federal Government kukamilisha bajeti yao ya kila mwaka. . Tazama Ontario yetu Federal budget 2014: Ottawa turning its back on Ontario, Wynne says | National Post Hakuna dhambi.
Wazanzibar nimeishi nao na naishi nao hawana tofauti na Watanzania wengine tena naweza sema sisi Watanganyika tuna roho mbaya zaidi yao. Wao wanashirikiana sana lakini sisi kama mifisi kazi yetu ni kuviziana. Leo Chadema na CCM ni maadui wakubwa na sidhani kama wanaweza kaa meza moja.
Leo hii wewe Nguruvi3 mambo yakikuchanganyikia tu utawaona wakipanga msitari na mabakuli yao lakini ziondoke hutamuona hata ndugu yako. Shida shida yako.. Hii habari ya matusi na kadhalika sisi wenyewe tunatukanana kama jambo la kawaida kabisa. Dharau ya makabila ipo hadi keshio. Wahindi na Waarabu wote wanatudharau lakini kina nani wanaoheshimmiwa bara kama sii Wahindi na Waarabu tena wa Bara.
Katiba yao ya mwaka 2010 ni maridjhiano baina ya CCM na CUF kabla ya uchaguzi wa mwaka huo na maridhiano hayo yalivunja uhusiano baina ya CUF na Chadema. Ni mchezo wa kisiasa ambao CUF waliingizwa Mkenmge na CCM. Nguvu hii ya CCM kuweza kutoa mamlaka makubwa kwa Znz pasipo kupitia bunge la Taifa, pasipo ridhaa ya wananchi ndi nguvu tunayiotakiwa kuiondoa. Ni katiba mpya tu inayoweza kuidhoofisha CCM kt mamlaka yake sii serikali 2 ama 3.
Mkuu nashukuru nawe umeliona hilo.Kiukweli mkuu hujibu swali...
Sidhani kama hili swali la serikali 2 zitasaidiaje Tanganyika kuvua koti la muungano linajibiwa kwa sentensi 20. Unachojitahidi kueleza wewe ni kwa nini huoni umuhimu wa serikali 3.
Lakini ni kwa vipi serikali 2 zitatatua tatizo, kiukweli hata hujagusia kabisaa...
Kauli ya kutumiwa na watu wa nchi za magharibi imetumiwa na Paul Makonda, gazeti la habari leo na sasa Nape NnauyeWAGAWE UWATAWALE
Mwanzo kabisa wa bandiko tumeeleza jinsi ambavyo mbinu zitatumika kuwagawa UKAWA.
Hii ni baada ya hoja za gharama, jeshi kushindwa.
Hizo ndizo zilizokuwa silaha za CCM walizotegemea zingeweza kuangamiza hoja za S3.
UKAWA walichukua muda mrefu kuanza mikutano. Katika muda huo CCM wamekuwa wakivuta kasi ili watoke bungeni na kuanza ksambaza hoja zao za upotoshaji.
Moja ya upotoshaji inayoonekana kutumiwa ni UKAWA kupewa fedha na mataifa ya magharibi.
Hoja hiyo ilioonekana kama laini kwasababu imetumika kila wakati serikali inapokosa hoja za kushawishi wananchi.Hoja hiyo imekuwa unafungamanishwa na amani na utulivu.
Kwamba, kupingana na serikali ya CCM ni kuvuruga amani na utulivu. Huo nao ni wimbo uliozooeleka.
Kwa bahati mbaya baadhi ya watu huvutika kirahisi na hoja ya amani na utulivu.
Hoja hiyo inapofungaminishwa na mataifa ya magharibi, huwatisha watu bila sababu yoyote.
Sasa hivi kuna mifano kwamba Tanzania itageuka kuwa somali, Ukraine au Russia.
Wananchi wanaoangalia TV wanaamini hasa wakiona nchi za magharibi zikiwa katika mvutano kama kule Ukraine,ndipo CCM wanapotumia mwanya kuwachanganya wananchi wasiobahatika kuwa na uelewa wa mambo hayo.
Hakuna mapambano hata kama muungano utavunjika leo.
Ni hisia tu zinapandwa kwasababu hazipo sababu za maana za kuthibitisha kuwa kutatokea vurugu.
ZNZ ni nchi na imejitambua hivyo, nani ataweza kwenda kuishambulia.
Na mapamabano yataanza kwa kisingizio gani hasa. Hizi ni propaganda za kuwatisha wananchi.
Hata hivyo UKAWA wasidharau propaganda za CCM.
Kwa mfano, CCM imeanza kutumia vijana wake kwenda kusambaza uongo.
Msome Paul Makonda hapa uone jinsi vijana wanavyotumika vibaya katika taifa hili....https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/647862-nje-ya-bunge-hakuna-katiba-ya-wananchi.html
Halafu soma habari hii ya gazeti la habari leo
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/24753-ukawa-waanza-mivutano
Utakachoona ni kuwa hoja ya Makonda ya kuvuruga amani na usalama na kutumiwa na mataifa ya magharibi ndiyo ile ile iliyotumiwa na habari leo.
Tofauti ni kuwa habari leo wameitumia kuwavuruga UKAWA kwa kusema kuna pesa zinatumwa kutoka mataifa ya magharibi na zimeliwa na baadhi ya vongozi.
Hoja hiyo inatueleza mambo makubwa mawili
1. Kwamba, kuna darasa ambalo mhariri wa habari leo na Paul Makondawamehudhuria na kuondoka na somo moja.
2. Kuwa mbinu za kuwagawa UKAWA sasa zipo kazini.
UKAWA lazima waelewe kuwa njia ya kupigania wanahciokitaka haitakuwa rahisi na ina wasaliti.
Wapo watakaolipwa ili kufanikisha mipango ya CCM.
Hapa ndipo ninashawishika na hoja ya Mchambuzi kuwa kauli ya rais Kikwete ya UKAWA wapo likizo na watarudi haikutoka bila sababu.
Tayari Kikwete anajua na ana vyombo vya dola, mbinu wanazosuka huenda zimefikia hatua nzuri hata kumfanya atambe hivyo.
UKAWA lazima wachukue tahadhari zote vinginevyo mpango wa kuwavuruga utatimia muda si mrefu.
Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Ukawa ni kikundi cha wachumia tumbo ambacho kinategemea fedha za wasioitakia mema Tanzania kuvuruga amani iliyopo.
Mkuu wangu wewe unashindwa kuliona tatizo kwa sababu mnatazama KERO badala ya Mapungufu yaliyomo ktk mfumo tulokuwa nao wa kiutawala. Ni mfumo wa kiutawala ndio unaweza leta maendeleo ama kutoyaleta kwani hoja kubwa ya Wazanzibar ni MAENDELEO ktk visiwa vyake na ndipo kero zilipokuja baada ya wao kutopewa kipaumbele kwa miaka 30, japo nyie kizazi kipya mnadai miaka 50 serikali 2 imeshindwa kuondoa kero.Kiukweli mkuu hujibu swali...
Sidhani kama hili swali la serikali 2 zitasaidiaje Tanganyika kuvua koti la muungano linajibiwa kwa sentensi 20. Unachojitahidi kueleza wewe ni kwa nini huoni umuhimu wa serikali 3.
Lakini ni kwa vipi serikali 2 zitatatua tatizo, kiukweli hata hujagusia kabisaa...
Mkuu Nguruvi3,
Mbona umejazana kuutetea UKAWA huku ukijua ni muungano BATILI kisheria?
Si ndio hao hao waliodiriki kumtukana Baba wa Taifa juu ya Muungano wa Tanzania ambao kwa maoni yao ni BATILI? Mbona na wao pia wanafanya yale yale?
Wametoka Bungeni wakilalamika kutukanwa lakini Prof Lipumba alisikika akiwaita walio na mawazo tofauti na ya kwake "Interahamwe!"
Sasa ya nini kulalamika wakati wewe nawe unafanya yale yale?
Nionyeshe mahala nilipoandika kwamba mimi Mkandara nawaunga mkono CCM na S2. Mkuu vipi lakini uko sawa kweli au ushabiki huu unakuipelekesha!Mkuu Mkandara
Naona umeiga kona tena.
Wewe umesema unawaunga mkono CCM kwa S2 na bandiko la hapo juu ukasema kilichopo ni mapungufu wala siyo kero.
Kila unapoongelea mapungufu a.k.a kero mara zote unafumba macho na kudhani tatizo ni znz tu. Huongelei adha za Mtanganyika.
Umesema mfumo wa sasa haukutoa kipaumbele kwa znz kwa miaka 30.
Kwamba, pesa za kukopa zinatumika na Tanganyika tu.
Maswali hayo unashindwa kuyajibu au kuyatolea ufafanuzi kwasababu hujaweza, hujaweza kueleza ni vipi tunaweza kuwa na muungano wa S2 ambao mchangiaji pekee ni Tanganyika halafu tukaweza kugawana mapato, misaada na mikopo kwa uwiano sawa bila pesa hizo kuwa za Tanganyika kwa muungano wa koti.
Jibu la haraka ni kuwa muundo wa S2 hautoi jibu.
Unachoogopa kusema ni kuwa S3 itawajibisha znz ambayo wewe unadhani inapaswa kupokea tuu bila kutoa.
Mkandara na CCM na serikali yao wanaamini kwa dhati kabisa kuwa ni sawa Mtanganyika alipe kodi, achukue misaada na mikopo na nusu awape wznz kwasbabu wao ni bora
Ndiyo maana Mkandara anasema kuvunja muungano ni kugawana umasikini.
Mkandara deni la taifa la sasa la ndani na nje znz haihusiki. Vipi uongelee kupokea tu na siyo kutoa.
Matokeo yake znz wanakopa michele Kenya halafu bili wanaleta Tanzania.
Wanasajili meli zingine za kihuni wanachukua pesa, ada za shirika la kimataifa analipa Mtanganyika.
Hii free ride ndiyo Mkandara anaita Kipaumbele.
Nakuhakikishia kuwa umasikini wa Tanganyika utabaki ule ule hata muungano ukivunjika.
Hatuna umasikini wa kugawana na znz kwasababu hadi sasa sisi ni masikini tunawowalea znz kwa kodi zetu.
Hatuwezi kukubali kubeba zigo la samadi na kupe huku wakiendelea kupiga kelele kila siku tena zisizo na maana ili mradi tu wafungue vniywa.Hatuna umasikini wa kugawana na znz, Tanganyika ni taifa kubwa mbele ya znz.period.
Maelezo yako kama ya wana CCM wengine hawajibu hoja ya kwavipi tuvue koti.
Unachotaka kusema ni tuwape znz kipaumbele na si Tanga au Mtwara wanachongaia kodi na pato la taifa.
Tuwape kipaumbele kwa mchango gani?
Kwamba, walale na wake zao wakitumia umeme wa bure mkulima wa Mtimbira alipe kodi ya kuwapa kipaumbele!
tafadhali bwana.
Kama znz wanadhani wanaonewa, hakuna sababu ya wao kuendelea na uonevu. Njia nyeupee waondoke.
Huu muungano ni kwa ajili yao si yetu na wala hatuwahitaji.
Muda wa miaka 50 kupigizana kelele na watu hawa unatupotezea muda.
Hatutaki kunyonya ndama asiye na kiwele. Tunyonye znz kwa kitu gani hasa, Uchumi wake ni mdogo kuliko asilimia 90 ya wilaya za Tanganyika. Kwanini tusiende kwenye nundu tukae tunakamua ng'ombe asiye na kiwele.
Mkuu bado hujajibu swali la Tuko. Unakwepa sana kwa utetezi wa znz.
Ukweli ni kuwa znz ni kupe ambao sasa ni tatizo kwa ng'ombe. Ni ima wang'olewe au wakae mgongoni kwa adabu. Tumechoka kutumia muda wetu kujadili watui laki 5 na siyo milioni 41.
Inawezakana kabisa hatufahamu na kwa vile unafahamu muundo wa S2 tunaomba utusaidie kidogo pengine tutabadili mawazo.Yaonyesha wazi kwanza hamuufahamu kabisa muundo wa S2 kama msivyofahamu Uislaam hivyo kila mnachoandika ni vichekesho tu kama vile Mkristu akitaka hukumu ndoa ya Kiislaam (Na swala la mahakama ya Kadhi) kwa sababu mnataka waislaam nao wawe na mfumo kama wa Wakristu! Kwa upande mwingine mimi napingana na Mahakama ya kadhi kwa sababu naufahamu Uislaam!