Ukiangalia jinsi Rais Ruto alivyopokelewa kwa heshima Marekani utashangaa

Huu ni ukweli mchungu sana
 
Sijaona sababu zozote za msingi za Ruto kuheshimika duniani. Na wala huwezi kumpata katika list ya maraisi wanaoheshimika
Hujaelewa somo, swali si Ruto anaheshimika sana duniani au haheshimiki.

Swali ni mbona Ruto anaonekana kuheshimika sana duniani kuliko Samia.

Ndiyo swali alilouliza mtoa mada katika sentensi ya kwanza kabisa ya thread.

Mbona unaacha kujibu swali lililoulizwa halafu unatunga swali tofauti ambalo halijaulizwa unajiuliza na kujijibu mwenyewe?
 
Nimekupa mpaka namba za GDP hapa, umekimbia kujadili uchumi kwa namba kulinganisha Kenya na Tanzania.
Kenya ni ya saba kwa GDP hapa Africa kama hiki ndio kigezo cha kumheshimisha basi maraisi wa taifa la 1-6 kwa GDP kubwa Africa wanaheshimika zaidi duniani kuliko Ruto

Pili, ameingia madarakani ameikuta Kenya ikiwa hapo hapo angeipandisha tungesema kidogo kafanya kazi
 
Swali la mtoa mada lilikuwa hili.

"Rais samia kwanini pamoja na ziara zote huko hapewi kipaumbele kama Ruto?"

Analinganisha Tanzania na Kenya, si ligi za dunia.

Sasa katika hizo nchi sita zilizoipita Kenya kwa GDP Tanzania ipo?
 
Kipaumbele gani unachozungumzia cha kupewa state visit?
Actually Samia alipewa kipaumbele kuongoza mazungumzo ya climate change Misri kwenye COP-27 Sharm el-Sheikh, kwa sababu mwanamke watu wakaona atapewa attention.

Akashindwa kuliongelea suala lile kwa ufanisi sio tu Misri, bali hata alivyorudi Tanzania kwenye press conference alishindwa ku highlight hiyo kazi.

Mpaka leo Watanzania wengi bado hawajui Samia aliongoza mazungumzo hayo kwa niaba ya nchi za Africa. Kashindwa hata kutangza hiyo habari tu aonekane na yeye aliongoza kitu fulani.

Wenzetu Wazambia ambao hata hawakuwa viongozi katika mazungumzo hayo wakapiga billions of dollars.

Watu wa kimataifa wakamdharau Samia.

Samia kafeli mtihani.
 
Wewe jamaa ni muafrika kweli... Na unakili sana.. maana unafikiria kabla ya kuzungumza..

Mmarekani Hana jema.. anampeti bwana ruto ili alegee mwisho wa siku afunguo milango ya chumbani..
 
Nakubali ...
 
Hujajibu swali.

Samia kampita Ruto kwenye performance gani? Kwa kipimo gani?

Kutojibu swali nako utasingizia typing error?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…