Wafanyabiashara wakubwa huwa hawabishani na serikali,ukiona mfanyabiashara anabishana na serikali jua huyo ni kichwa maji
Kijana tayari alikuwa na misala mizito akaona aingie kwenye siasa ionekane kakamatwa kisa siasa. Vyombo vya usalama vya Tanzania huwa vinamchunguza sana mtu kabla ya kumkamata ingawa wakati mwingine kuna maafisa huzingua kwa kuweka weledi pembeni.
Una uhakika?? 99.9% ya kesi zote huko mahakamani upelelezi haujakamilika na watu wanasota rumande na ndiyo sababu kuu ya msongamano magerezani.Vyombo vya usalama vya Tanzania huwa vinamchunguza sana mtu kabla ya kumkamata.
Mkuu kama PCCB na TRA wakiamua kunyooka kama rula matajiri watabaki wachache sana mjini. Ni busra tu zinatumika. Wabongo kutokuwa na madoa ni ngumu sana.Ukijiona una madoa sio msafi usithubutu kuichokoza serikali hauwezi ukawa salama
Itv na radio one zilipokua kimbelembele kwa chadema, walikua wanampelekea mengi Kodi alizokwepa, ndiyo maana baada ya magu kutangazwa mshindi,mengi alikua mtu wa kwanza kufika Lumumba kupiga picha na magu akiwa na cheti cha ushindiSure, Mbaya zaidi huwezi kua msafi kwenyw biashara, wakikutafuta watakupata tuu.
Sasa kuna watu kama Hushpuppi wao nia yao nzima ya kupata pesa ni ili wawatambie.Ukifanikiwa punguza kelele kula kimya kimya. Watu wasijue chimbuko la pesa zako. Dogo mmoja wa twitter huko (x) alikuwa na maneno ya shombo sana kwa watu sahv wamemfelisha ananyea debe .
Hushpupi pesa zote alizopata asingekuwa na kelele yasingemkuta maswahibu yaliyompata
BTW,mhaya gani?kwani hajawahi kuisema hata kidogo? mbona huwa anajisema ni CDM kindaki ndaki japo nilisomaga kipindi cha nyuma sijui ni kwa yule mkamaria alisema tajir ni kipenyo
Inasemekana alichokoza siasa makusudi ili awekwe ndani kukimbia madeni...Sir Jeff kilichomponza ni Siasa. Alijisahau akajua yupo kwenye ulimwengu wake wa Forex. Ajifunze kwa Jack Ma, Serikali ya China ilichomfanya alipotaka kuja na Ant Group IPO, kwaajili ya Digital Currency yake na kuanza kuidharau serikali.
hapo kwenye vyombo vya usalama kuchunguza mkuu umedanganya hao huwa wanasubiri kutumwa tu hawana loloteKijana tayari alikuwa na misala mizito akaona aingie kwenye siasa ionekane kakamatwa kisa siasa. Vyombo vya usalama vya Tanzania huwa vinamchunguza sana mtu kabla ya kumkamata ingawa wakati mwingine kuna maafisa huzingua kwa kuweka weledi pembeni.
Polisi utawaona hawafanyi kazi kama hawakutafutihapo kwenye vyombo vya usalama kuchunguza mkuu umedanganya hao huwa wanasubiri kutumwa tu hawana lolote
SahihiNazani hapa bongo ukiamua kufanya biashara, Achana na siasa au harakati.
Hakika Mkuu watu kama Hushpuppi ni ngumu kuwatuliza labda prison pekee.Sasa kuna watu kama Hushpuppi wao nia yao nzima ya kupata pesa ni ili wawatambie.
Ukimwambia mtu kama huyo atafute pesa halafu akae kimya asiwaoneshe kuwa kapata pesa, unakuwa umeondoa sababu yake kubwa ya kupata pesa.
Yani yeye anaona kuwa na pesa halafu asijioneshe anaona ni sawa na kutokuwa na pesa.
Ili ajue ana pesa kweli ni lazima ajioneshe, awatambie.
Halafu pia, kule kujionesha ni sehemu ya kuvutia watu ili aweze kupiga pesa zaidi.
Zike saa za Hushpuppi za bei mbaya alikuwa anavuka nazo mipaka kama sehemu ya money laundering. Sasa akiwa anajulikana huyu Hushpuppi anavaa saa za gharama, anapata urahisi wa kuvuka nipaka bila kuulizwa, kwa sababu anajulikana mitandaoni.
Ni kama habari ya "biashara matangazo" halafu wewe unamwambia mfanyabiashara afanye biashara kimyakimya bila matangazi.
Kabisa Dada yeyoyoooMungu akikupa mapema
muonbe akupe na hekima ya kuziendesha hizo pesa
ontario hata kabla ya siasa alikua anatukana sana watu kwamba nyinyi maskini na blah blah za kijinga
sawa wewe Mungu kakupa kwann unaita wengine maskini??
kwanza anapenda showoff kama mtoto wa form 2
mi nakumbuka sakata flani alikuala ela ya jamaa jamaa akasafiri kuja kumfata alivyokua ana mjibu yaani dharau plus ushubwada wa kupuuzi kweli kweli
kuna vijamaa vina sifa za kijinga maishani kama huyo jeff ila tu havijapata ela
huyo jeff ujinga umemjaa ubongo wa mbele
na huo utajiri gani wa kufunga semi moja ya mbao??
ni hela za kawaida sema tu hana utulivu
waongee kina Benji fernandes
Ni nani huyo msaada plzπ π π kuuumbe sema ana mbwembwe sana yule jamaa
Yule ni mwenzetu wasiojulikana, usije ukamzoea zoea kienyeji.mbona yule tajir wa kihaya anajipost yeye na mali zake plus michambo mingi kwa watu lakini hajakutwa na jambo?,,,