Mods sitaki mbadili title,
Ktk watu ambao huwa wanaanza na idea ya kitu, wanakitathimini, wanatafakari na kupata picha halisi kabla idea hiyo haijafanyiwa kazi na kuwa kitu, basi ni hawa watu wanaoitwa maingineer.
Fikiria daraja la kigamboni, fikiria daraja la ssalenda lile jipya linalopita baharini, fikiria reli ya mwendokasi kuna njia imepasuliwa kati kati ya mlima.
Hawa majamaa wanahamisha mpaka mito wanajenga daraja kisha wanaurudisha mto unaendelea kutililisha maji kama kawaida,
Hivi ktk hali ya kawaida mtu kama huyu akikufuata akakuambia hana ramani ya maisha unamsaidiaje?
Engineer yeyote akikufuata akakuambia hana mchongo wa kufanya na hajui afanye biashara gani mpige makofi.
Nawasilisha.