Ukimpata mwanamke anayekupenda usimletee masihara utakuja kumlilia siku akibadilika

Ukimpata mwanamke anayekupenda usimletee masihara utakuja kumlilia siku akibadilika

muda mwingne anaweza asiwe kweli bwanawake lakini mtu anapangwa mjini hapa jamani,ukimtafuta mtu ukamwambia 50k hii hapa fanya moja 2 na 3 aahh mtu anaigiza kabisa
Ata akiwa na rafiki tu ama mtu yeyote wanejuana wamewahi kushare situations anazopitia anafanya tu
 
Hy n sawa, lkn vp kama yeye anakupenda lkn ww humpendi.?
Hapo sasa, nakumbuka enzi hizi nikiwa bachela nikapita na single mother mmoja hivi, akaanza kuniganda Kila nikitaka kumwacha ananiganda analia na kuniambia usiniache nimekuzoea huruma ikaniponza, akapata ujauzito akaona ndiyo tiketi ya kumuoa, nikasema huyu hanijui vizuri. Pamoja na kufuatwa na wazazi wake, kaka zake lakini sikuwa tayari kuishi nae
Hy n sawa, lkn vp kama yeye anakupenda lkn ww humpendi.?
 
Moja ya vitu ambavyo tunavyo baadhi ya wanaume ni kuwachukulia poa wale wanawake wanoonyesha kutupenda kupitiliza, unakuta una mwanamke anakujali mnyeyekevu anakuheshimu alafu unamchukulia poa poa tu wengine tunawanyanyasa tukijua hawana kimbilio sababu ya kuvutiwa na sisi kimapenzi hivyo tunawachukulia kimasihara

My friend siku mwanamke akikuchoka huwa anakuchoka kweli kweli na akigeuza shingo huwa ni mazima kama kashakuvumilia vya kutosha ,akichoka manyanyaso huwa anachoka kweli, ukibahatika kumpata mwanamke mnyeyekevu msikivu anayekujali yaani onyesha kumjalizaidi na kumpenda my friend hawa wanawake wastaharabu wamebaki wachache sana, ukimpata jua umepata dhahabu ndani, wengi walishasombwa na maafuriko kipindi cha mwinyi kwa sasa hawapo wengi wamenaki wachache.

Nayaongea haya sababu kaka yangu kalazwa now siku ya pili presha imepanda, alipata mwanamke mzuri mpolee aliyempenda kupitiliza akamuowa kabisa, yule dada alikuwa anaupendo wa ajabu ukweni , anapendwa ukweni hadi leo, sababu ya tabia zake tu

Ila brother akawa anamchukulia poa anamnyanyasa ,anampiga kesi zikawa zinaletwa hom mara kwa mara , binti akawa anavumilia tu mwaka na miezi sita, sasa juzi bro karudi hom kakuta mkewe kabeba vitu vyake vyote kaondoka kutafutwa kwenye sim anapokea mwanaume anasema muhusika hayupo asisumbuliwe

Kaka kupata hizo habari nusu tumpoteze tumbo la kuhara lilimbana hapo hapo majirani ndio wamemkimbiza hospitali juzi, kufika Bp juu kakata kauli kaaza kuongea jioni ya jana, kachungulia kaburi yani

Saaa kumbe mwanamke alikuwa anampenda kwanini amnyanyase?
Mkuu yalinikuta, hadi nilihisi kufa nashukuru mabaalia waliniokoa na wakanifundisha hakuna kuingia mazima, saivi naangalia walioko kwenye mahusiano tu,
 
Pia wanawake mkipendwa na mwanaume ambaye hana hela, msichezee hiyo nafasi maana siku akizipata hautamuona tena hapo kwako na utatamani hata ajibu text yako ila hautapata hiyo nafasi ya kujibiwa.


Kwa kifupi kufanyiwa vibaya haina jinsia.... Hutokea kote tuu mbona.
Mwiba mkali sana 😁
 
😂😂😂😂 nina dogo hapa home baada ya kubembeleza saaan bby mama nikaona anielewi nikamwita dogo then kiutani tu nikamwagiza sumu ya panya ety.......!😂😂😂😂 haya mapenzicuseng***** kweli jaman. Ile karudi tu na sumu fahamu ndo zinarudi nikakumbuka nina masela wa tungi hapa kitaa nkamweleza tu dogo rudisha sumu njoo na mirinda nyeusi ya baridi baada ya kunywa hyo nikatoka out mm na wano ukawa mwendo wa vyombo tu. Saiv no love no stress na kati ya mapenzi na tungi bora nn nitakwambia bira tungi🤟
Ungedus Kudanja mmbwa ww...Kula kimea halisi.
 
Daahh najaribu kui magine huyo aliyekimbiwa na mkewe halafu kazimia na watu wote wanajua ..sijui aki recover uso wake atauficha wapi 😆😆😆

Usela usela kwenye mapenzi haufai
 
Hakika mkuu. Siku hizi wamejaa wale walioko kwa ajili ya kukukomoa. Akilala anawaza aje na gia gani kukuchomoa. Mapenzi ya siku hizi yamekuwa na hasara nyingi kuliko faida kwa wanaume.
📌📌
 
dunia ina zaidi ya watu billion 7 na zaidi ya nusu ni wanawake, mwanamke mmoja tu anatoa roho ya MTU. Bro wako ana matatizo ya afya ya akili si bure!
😀😀😀😀
 
Ebwana broo umesema neno hapo. Mwenyewe leo yamenikuta aiseh. Huy mwanamke nimekaa naye kweny mahusiano for more than two yrs almost five ila toka juzi naye kanipa kisogo nabembeleza lakn wap. Hapa nahsi moyo unanisuta, nafsi yenyewe inaniuma daaah kweli tukipedwa jaman tupendeke. Nakupenda saan p wangu
😀😀😀
 
Unasema alimpenda sana mumewe ila kaomdoka na simu anapokea mwanaume mwingine je huyo mwanume amempata siku hiyo hiyo alipoondoka au ulikuwa mpango kando kabla? All in all wanasema usibebe mayai yote kwenye kapu moja! Bro wako alimnyanyasa kama ulivyosema ila hakuwa anapendwa kama unavyohadithia.
😀😀😀 Haiwezekani mwanaume ampate siku 1 huyo Ni fisi aliyevaa manyoya ya bata
 
Mimi nimekuelewa zaidi ya wote. Ulichoandika ni ukweli mtupu. Hii huwa inatokeaga kwa wale wanawake wanaopenda sana kupitiliza, ukimkosea anakuomba yeye samahani, ukimwambia nakuacha atalia nusura ya kufa yaani yuko tayari kufanya jambo lolote ili asikupoteze. Ukitaka waendelee hivyo wapende yaani japo tu mdanganye, ila ukimtesa au akichoka akuacha lazima uumie,

Utajiuliza ni wapi alikohamishia mapenzi Yale na lazima ukonde vile jinga lako limegeuka janja.
True true huwa inaumiza sana
 
Back
Top Bottom