Ukimsaidia Mbongo jambo au fedha, kila tatizo atataka umsaidie tena. Hii ni ishara ya Low IQ

Wizo mvua zimeanza ushabadili jinsia 😹

Kwahiyo uliwahi kumuweka kimada single maza? 😹😹
 
Nachukia sana hiki kitu. Nina mama yangu mdogo, niliwahi kuna na binti yake kwangu akisubiri kwenda degree. Kwa kuwa anasaidia kazi za nyumbani ikibidi nimpeleke computer course. Alipochaguliwa nikampa hela ya kuanzia chuo wakati anasubiri boom

Nikawa kama nimechokoza nyuki. Baada ya week tu mama yake huyu hapa mwanangu nisaidie na hiki na kile. Akaniona kama mimi ni Backresa. Mimi ni katika watu walionyooka, nikamwambia sio wewe tu mwenye shida kwenye ukoo. Mama yangu mwenyewe sijamnunulia kitenge toka mwaka umeanza. Uwe na shukurani.

Baada ya hapo sikuwahi kupokea simu yake. Huwa akipiga naitazama tu.

Baba yangu mdogo hivyo hivyo mwanaye kushindwa kupata matokeo ada hajalipa. Nikasema pesa kitu gani, nikalipa laki 4....daah wakaona kama nina hela za kuchezea. Akanitumia na number ya Luku kabisa niwe namlipa umeme. Nikampotezea mazima huu mwaka wa 5.

Kuzaliwa familia za masikini ni kero sana
 
Ni ajabu sana mkuu kwa maana katika hali ya kawaida, yule aliyetafutiwa ndiye aliyepaswa kumpa 10% aliyemtafutia kama shukrani..
Exactly na mjini ndio ipo hivyo.

lakini kuna watu wana hiyo entitlement haswa kwenye familia. Mtu anaacha kazi na anaanza kusumbua ndugu zake wamtafutie

Ni ajabu lakini wapo
 
Zaidi ni pale ndugu ambao maisha yao ni magumu wanazaa watoto wengi wakitegemea ndugu zao wenye pesa watawasomeshea au kuwaletea chakula. Wao wanakuwa hawana mpngo na wao. Hii kitu kwa familia inaumiza sana.
UPUMBAVU ni wewe mwenye pesa, kuwasaidia,....
 
Mm binafsi kuna Mafundi 2, niliwapa kazi ya finishing kwangu, mmoja Rangi, mwingine kitchen cabinets. Tukalipana vzuri tu. Tukaachana kwa wema. Ila sasa, kila mara, hawa mafundi hawaishi kunipiga mizinga. Eti ooh! Boss leo nalala na njaa, okoa jahazi. Mara naumwa, sijaweza kwenda kazini mwezi sasa. Wameshanipiga vibomu hadi sahivi, hata simu zao spokei kabisa. Na usipopokea simu, unakutana na miscall 6 hadi 10 kama vile baba mwenye nyumba anakudai kodi yake ya miezi kadhaa uliyorundika bila kulipa.

Mi nadhani, virungu, havikatazwi, lakini isizidi mara 2. Ikizidi hapo unakuwa kero.
 
Mafundi wajanja ni wale wanaoomba uwaunganishie kazi kwa jamaa zako ili waendelee kuishi
 
Wizo mvua zimeanza ushabadili jinsia 😹

Kwahiyo uliwahi kumuweka kimada single maza? 😹😹
Wizo naona unataka kuanza kuitikisa mbunye yangu!!

Mimi ni demu mwenye roho njema, nasaidia wasiojiwezaa πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
 
Watanzania wengi hawana elimu ya pesa akiongeza kipato kidogo anaongeza na matumizi mwisho shida zinabaki pale pale
Ni ngumu sana kumsaidia mtu ambaye hana elimu ya pesa
Kabisa maana wengi kipato kikiongezeka na matumz juu.
 
Sema ungekaa kimya tu yupo uku uku JF anaona post 😁😁
 
Ni taabu sana kuishi na watu wa hivyo.
 
Siyo wote acha ukumbaff hata Mheshimiwa mbeba maono Samia?!!!!
 
Mimi sina nidhamu ya pesa nawasumbua watu. Bali narejesha deni.

Mnachoongelea ni upuuzi kama huwez kumsaidia mtu kaa kimya. Mpige fix achana nae kuliko kuja kuripoka hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…