Ukimsaidia Mbongo jambo au fedha, kila tatizo atataka umsaidie tena. Hii ni ishara ya Low IQ

Ukimsaidia Mbongo jambo au fedha, kila tatizo atataka umsaidie tena. Hii ni ishara ya Low IQ

Emotional intelligence ni tatizo kubwa kwa watanganyika wengi.

Kuna single maza nilimlipia kodi ya nyumba ndio ikawa nongwa, kila siku ananiomba hela ya kula, mara mtoto wangu anaumwa kalazwaaa..... MANINAAA!!

Nilimfuta na kumBROKU.

Cc: Lamomy Mbaga Jr Kalpana Extrovert
Wizo mvua zimeanza ushabadili jinsia 😹

Kwahiyo uliwahi kumuweka kimada single maza? 😹😹
 
Nachukia sana hiki kitu. Nina mama yangu mdogo, niliwahi kuna na binti yake kwangu akisubiri kwenda degree. Kwa kuwa anasaidia kazi za nyumbani ikibidi nimpeleke computer course. Alipochaguliwa nikampa hela ya kuanzia chuo wakati anasubiri boom

Nikawa kama nimechokoza nyuki. Baada ya week tu mama yake huyu hapa mwanangu nisaidie na hiki na kile. Akaniona kama mimi ni Backresa. Mimi ni katika watu walionyooka, nikamwambia sio wewe tu mwenye shida kwenye ukoo. Mama yangu mwenyewe sijamnunulia kitenge toka mwaka umeanza. Uwe na shukurani.

Baada ya hapo sikuwahi kupokea simu yake. Huwa akipiga naitazama tu.

Baba yangu mdogo hivyo hivyo mwanaye kushindwa kupata matokeo ada hajalipa. Nikasema pesa kitu gani, nikalipa laki 4....daah wakaona kama nina hela za kuchezea. Akanitumia na number ya Luku kabisa niwe namlipa umeme. Nikampotezea mazima huu mwaka wa 5.

Kuzaliwa familia za masikini ni kero sana
 
Ni ajabu sana mkuu kwa maana katika hali ya kawaida, yule aliyetafutiwa ndiye aliyepaswa kumpa 10% aliyemtafutia kama shukrani..
Exactly na mjini ndio ipo hivyo.

lakini kuna watu wana hiyo entitlement haswa kwenye familia. Mtu anaacha kazi na anaanza kusumbua ndugu zake wamtafutie

Ni ajabu lakini wapo
 
Zaidi ni pale ndugu ambao maisha yao ni magumu wanazaa watoto wengi wakitegemea ndugu zao wenye pesa watawasomeshea au kuwaletea chakula. Wao wanakuwa hawana mpngo na wao. Hii kitu kwa familia inaumiza sana.
UPUMBAVU ni wewe mwenye pesa, kuwasaidia,....
 
Mm binafsi kuna Mafundi 2, niliwapa kazi ya finishing kwangu, mmoja Rangi, mwingine kitchen cabinets. Tukalipana vzuri tu. Tukaachana kwa wema. Ila sasa, kila mara, hawa mafundi hawaishi kunipiga mizinga. Eti ooh! Boss leo nalala na njaa, okoa jahazi. Mara naumwa, sijaweza kwenda kazini mwezi sasa. Wameshanipiga vibomu hadi sahivi, hata simu zao spokei kabisa. Na usipopokea simu, unakutana na miscall 6 hadi 10 kama vile baba mwenye nyumba anakudai kodi yake ya miezi kadhaa uliyorundika bila kulipa.

Mi nadhani, virungu, havikatazwi, lakini isizidi mara 2. Ikizidi hapo unakuwa kero.
 
Mm binafsi kuna Mafundi 2, niliwapa kazi ya finishing kwangu, mmoja Rangi, mwingine kitchen cabinets. Tukalipana vzuri tu. Tukaachana kwa wema. Ila sasa, kila mara, hawa mafundi hawaishi kunipiga mizinga. Eti ooh! Boss leo nalala na njaa, okoa jahazi. Mara naumwa, sijaweza kwenda kazini mwezi sasa. Wameshanipiga vibomu hadi sahivi, hata simu zao spokei kabisa. Na usipopokea simu, unakutana na miscall 6 hadi 10 kama vile baba mwenye nyumba anakudai kodi yake ya miezi kadhaa uliyorundika bila kulipa.

Mi nadhani, mixing haikatazwi, lakini isizidi mara 2. Ikizidi hapo unakuwa kero.
Mafundi wajanja ni wale wanaoomba uwaunganishie kazi kwa jamaa zako ili waendelee kuishi
 
Wizo mvua zimeanza ushabadili jinsia 😹

Kwahiyo uliwahi kumuweka kimada single maza? 😹😹
Wizo naona unataka kuanza kuitikisa mbunye yangu!!

Mimi ni demu mwenye roho njema, nasaidia wasiojiwezaa 😋😋😋
 
Watanzania wengi hawana elimu ya pesa akiongeza kipato kidogo anaongeza na matumizi mwisho shida zinabaki pale pale
Ni ngumu sana kumsaidia mtu ambaye hana elimu ya pesa
Kabisa maana wengi kipato kikiongezeka na matumz juu.
 
Hi!
Binadamu mwenye akili timamu au mwenye standard IQ anapaswa awe na aibu na utu.
Nilomsaidia brother mmoja kumnunulia simu baada ya kuona simu yake ina matatizo. Sasa anataka nimsaidie kununua kaunta book za watoto wake. Anapiga simu kama ugomvi.
Nilomsaidia mtu kupata kazi mahali kipindi akiwa apecha alolo. Mshahara pamoja na posho around 700k-900k.
Sasa amelijua jiji anaona pesa ndogo anataka kazi kwenye kampuni zingine, Cha ajabu anataka tena Mimi nimsumbukie kumtafutie tena kazi huko ili aaache pa sasa.
Mifano iko mingi sana.
Ukimsaidia tu mbongo huyo atakuwa mgeni wako na kama mwanamke atataka muwe wapenzi ili akuvune zaidi.
Sema ungekaa kimya tu yupo uku uku JF anaona post 😁😁
 
Kwakwel n kipengele... Kuna ndugu tena wa kike mdada mtu mzma mpka akanipa namba ya mwenye nyumba wake vile anavyosumbuliwa kodi nkaongea na faza house tukalsort nkamtumia kod ya miez 4 Toka apo sasa kila wikend anapga simu anataka 15000 akalewe aweke kichwa sawa mara na stress sana kaka angu leo sjui nakula nn Wabongo ss tabu tupu n bora wote kulia noki tu ukiombwa msaada na ww lia shida apo wote mtaish kwa aman
Ni taabu sana kuishi na watu wa hivyo.
 
Hi!
Binadamu mwenye akili timamu au mwenye standard IQ anapaswa awe na aibu na utu.
Nilomsaidia brother mmoja kumnunulia simu baada ya kuona simu yake ina matatizo. Sasa anataka nimsaidie kununua kaunta book za watoto wake. Anapiga simu kama ugomvi.
Nilomsaidia mtu kupata kazi mahali kipindi akiwa apecha alolo. Mshahara pamoja na posho around 700k-900k.
Sasa amelijua jiji anaona pesa ndogo anataka kazi kwenye kampuni zingine, Cha ajabu anataka tena Mimi nimsumbukie kumtafutie tena kazi huko ili aaache pa sasa.
Mifano iko mingi sana.
Ukimsaidia tu mbongo huyo atakuwa mgeni wako na kama mwanamke atataka muwe wapenzi ili akuvune zaidi.
Siyo wote acha ukumbaff hata Mheshimiwa mbeba maono Samia?!!!!
 
Mimi sina nidhamu ya pesa nawasumbua watu. Bali narejesha deni.

Mnachoongelea ni upuuzi kama huwez kumsaidia mtu kaa kimya. Mpige fix achana nae kuliko kuja kuripoka hapa
 
Back
Top Bottom