Ukimsaidia Mbongo jambo au fedha, kila tatizo atataka umsaidie tena. Hii ni ishara ya Low IQ

Ukimsaidia Mbongo jambo au fedha, kila tatizo atataka umsaidie tena. Hii ni ishara ya Low IQ

Hivi hamna jinsi ya kuweka hili somo darasani maana hakika umaskini wetu umeanzia hapa na hata ukijaribu kugusia hili UTAONA jinsi utachambwa mara mchoyo mara roho mbaya ila ukweli ni janga la taifa.
Hata ukiweka somo labda iwe home business ama economics lakini suala kubwa zaidi ni kila mtu kutambua kuwa nidhamu ya pesa imeegemea katika tabia za mtu

Na tabia zinaandaliwa toka nyumbani kwa hiyo lazma mtoto atengenezewe mazingira ya kujua kuwa, kitu chochote anachotaka nje ya basic necessities lazma azifanyie kazi

Anataka video games, mpe kazi afanye then apate. Zamani tuliambiwa ukifaulu ndio unapewa kitu flani so ilitengeneza mazingira ya kuwa kila unachokitaka, unatakiwa ukifanyie kazi... Huo ndio mwanzo wa kumfanya mtoto independent, responsible and disciplined
 
viongozi omba omba, kila siku bize na kapu na kauli mbiu ni deni stahimilivu, timu za mpira na nyumba za ibada vile vile ni mwendo wa kutembeza bakuli japo wana vyanzo vingine vingi vya mapato,....ulitegemea wananchi waweje?....watanzania ni omba omba kwa asili na sio WAWAJIBIKAJI kwenye matatizo yao kabisa ...
 
Uzungu sio ngozi, ni itikadi tu na namna ya kuendesha maisha. Ukiendesha maisha kibepari we ni mzungu. Mzungu anajua mipaka ya msaada na haogopi kusema hawezi. We uchukie usichukie utajua mwenyewe.
Umetisha sana mkuu.
 
Ni kweli kabisa, nimekutana na hii Hali sana. Mara nyingi nafanya Moja ikizidi ya pili bye bye.
 
Ule hata ukiubeba haubebeki. Imagine mtu akutafutie kazi na bado unaomba akutafutie nyingine yenye mshahara mzuri.

Hii ni ajabu
Ni ajabu sana mkuu kwa maana katika hali ya kawaida, yule aliyetafutiwa ndiye aliyepaswa kumpa 10% aliyemtafutia kama shukrani..
 
Back
Top Bottom