Ukitaka hela za haraka fungua kanisa kuna majinga mengi; kinachoendelea Kawe kwa Mwamposa kinasikitisha

Huu ni utapeli na uhujumu uchumi wa wazi kabisa unaolindwa na serikali ya ccm.
Mkuu haya mambo bora uyasikie ukiwa mbali tuu. Kwa wakazi wa kawe ni ngumu mno kuuamini ikiwa ndugu mwamposa ni kiumbe wa kawaida. Ilifikia mahali waiting zinaokotwa kwenye maeneo yake.

Baada ya kuona kero hiyo,alichofanya ni kuweka walinzi wa sura jkt kuzuia watu kuwepo eneo hilo muda ambao sio wa ibada. Ni kwamba watu wsnatoka mikoani hoi taabani na wanakua hawana mahali pa kufikia.

Wakazi wa kawe wenye nyumba zenye vibaraza wanawalipisha watu 2000 per night, watu wanalala kama wanyama.

Ccm imeharibu sana hiki kizazi.
 
Mwamposa anawazuia watu kuelekea katika njia ya Mungu. Yeye kashapotea na bado anazuia watu wasimuendee Mungu.

Hakika Mwamposa ni kiumbe muovu sana na atabeba dhambi za watu wote aliowapoteza pasi na wao waliopotea kupunguziwa chochote katika dhambi zao.
 
Hosea 4:6 kwenye Biblia, ambapo maandiko yanasema "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa"
 
MUNGU anasema katika ufunuo wake wa mwisho kuja kwetu sisi wanaadamu .

Quran 9:34
"Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat'ili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu."
Mwamposa ni miongoni mwa "mwanazuoni wa kikristo" (aka Kuhani) ambaye anakula mali za watu kwa batili na anawazuia wakristo wasimmjue Mungu...anajilimbikizia mali na dhahabu na wala hazitumii katika njia ya Mungu (kusaidia Mayatima,Masikini,wagonjwa,wafungwa,Wajane n.k)...ila anazitumia kwa manufaa yake kujenga mahoteli ,kujinunulia magari ya kifahari,kuhonga wanawake n.k

Quran 9:35
" Siku zitapo tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwa mkilimbika."
 
Unadhani ni rahisi hivyo? Kasome kitabu chake cha NGUVU YA KUONA ndio utajua ilivyo mtiti kuanzisha huduma hiyo
Wewe uliyekwishasoma unasubiri nini na wewe kuanzisha?
 
Wajinga ndiyo waliwao. Mkuu endelea kumtajirisha Mwamposa
 
Unawacheka waumini wa Mwamposa wakati kanisani kwenu RC mna maji ya baraka yamechotwa kwenye choo cha kanisa 💩🤣💩🤣 WaTz wapumbavu sana mnajifanya wajuaji kumbe kichwani kumejaa takataka.
Hata maji ya kutawadha msikitini kwenu yako pembeni ya choo
 
Mbona kwenye mikutano ya kiserikali hawajai hivi?
 
Uwongo tu
 
... anaweza kubaki na magongo kwa muonekano wa nje, ilkhali kwa ndani AMEISHAYATUPA! ... FOR THOSE REALLY BLESSED THEY GET IT SPIRITUALLY AND INTERNALLY!
Hapo sasa ndipo penye UTAPELI wenyewe. Yaani upone kwa ndani huku bado inatembelea clutches. You are highly hypnotised by Mwamposa, poor soul
 
Huwezi wapanga wale watu woteeeeeee hapo kama unaweza anzisha huduma Yako uone kilicho mtoa kanga manyoya shingoni 😁
Mazezeta wengi sana wala hawahitaji kupangwa sana. Nawaonea huruma sana ninapokuta wanavuka pale daraja la Kawe asubuhi wakitaka kurudi makwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…