Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Umenikumbusha miaka fulan nilipokuwa nikienda kijijini kwa babu kusalimia, kuna ng'ombe,mbuzi na panda wa kubebea mizigo.

Nilikua napenda sana kwenda kuchunga, yaani kila atakayekuwa ni zamu yake lazima niende nae, sasa mkiwafungulia kwenda kuchunga inabidi tuwatoe huku tunawakimbiza maana mashamba yapo karibu, yaani ukichunga mbuzi unatakiwa kuwa makini sana ni dk chache wanapotea.

Pale kwa babu kulikua na mbuzi wawili walafi hao ndo huwa wanaanzisha msafara wa kukimbilia shambani, pale tushachinja mbuzi nyingi tu ambazo tulikuwa tunapiga na jiwe kwa bahat mbaya linatua sehem mbaya mbuzi anataka kufa tunachinja

Mbuzi wanauzi sana
 

😀😀😀 na usiombe huyo mbuzi awe na ndevu ni BALAA
 
Mbuzi wasumbufu sana kama unahasira za karibu unaweza kumtwaga jiwe akafa

Mbuzi wakati wa masika sio wasumbufu sana ila wakati wa kiangazi/jua kali wanasumbua sana.
Kwetu kipindi cha masika ndio wasumbufu sana maana wanakuwa kwenye limitation(chini ya ulinzi) machungani na ndipo kipindi penye majani mabichi mazuri ikiwemo mazao.

kipindi cha Kiangazi wanakuwa wanachia maana tunakuwa hatuwalimit, tunawaachia wajichungie kwa kudhurura watakavyo ila ikifika jioni tunaenda kuwapokea(kuwatafuta kwa wale wakorofi kama Mabeberu ambao wanakuwa wanachanganyikana na makundi mengine ya mbuzi), pia mara nyingine huzoea hiyo hali na ikifika jioni wanarudi wenyewe nyumbani.
 
Wakiwa watatu wamefungwa kamba shughuli yake sio ya kitoto , wawili wanaweza amua kukaza unavuta wao wanakurudisha nyuma , alaf mmoja wa tatu yeye anakuvuta kuekekea kwenye mazao , ukute hapo na wewe kuna demu kakuvuruga akili , kuua ni kugusa tuu😁
 
Kama kuna shamba wamelizoea ukiwafungulia tuu ni mwendo wa Usain bolt , kila sku utakuwa unakimbia relay😁
 
Mbuzi wanachangamsha watoto nyumbani [emoji16]
Tuliletewa jike na mwanae kumbe yule mama alikuwa na mimba akazaa dume tukakampa jina Champion, tulikuwa tunacheza naye sana baba akaamua kumuhasi/asi (hapo sijui lipi sahihi) jamaa alivyokuwa akawa na kiburi na dharau sio ya kawaida majani ya jana hali, hataki kufungwa kamba hivyo mama na dada yake wanafungwa yeye yupo pembeni yao na kulikuwa na mti umepinda vizuri kwamba alikuwa anaweza kuupanda hivyo yeye aliupanda akala majani, majani ya jana wakala mama na dada champion. Tusipomuona inabidi tumuite na anaitika kabisa Mee halafu anakuja mbio Kama mtoto anavyoitwa na akija hata Kama kakuudhi inabidi utabasamu lasivyo anakupiga pembe [emoji3][emoji3][emoji3], baadae akawa ukisahau jiko wazi anaingia anakula chakula chochote atakachokikuta ispokuwa nyama na samaki tu. Baadae akawa kero mtaani anaingia nyumbani kwa watu akikuta wanakula na yeye anataka Kula wakimnyima anapindua meza, hawakuchinjwa wote wala kuuzwa maana watoto tulikataa yote, na mwisho mzee aliwagawa baada ya watoto wote kuondoka nyumba, hadi Sasa bado tunamuongelea champion ambaye mdogo wangu aliinama kumfunga kamba kwa hasira jamaa akarudi nyuma Kama hatua saba hivi akaja speed akampiga kichwa mdogo wangu akaanza kuvuja damu puani na mdomoni Mungu NI mwema dogo alipona, visa NI vingi ila niishie hapa maana mmenikumbusha mbali.
 
Kondoo nawafuga ni wapumbavu sana, wanapenda kukaa kimakundi, mmoja asipoona wenzie atalia na masauti yao mabaya.

Ni wabishi pale unapo wavuta wana kiburi hatari, ila ukishamjua kiongozi wa kundi basi hawana shida kuwa fuga.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ndo mana mitume karibia wengi walikua wakifuga mbuzi kabla ya kupewa utume ili waweze kuvumilia maudhi ya binadamu katika kulingania Dini
 
Huku kwetu kipindi cha kiangazi wanasumbua sana maana kuna migunga/accasia
 
Sisi uchagani tunafuga kwa kuwafungia ndani. Kuna kichanja cha nje na cha ndani. Sasa way back 2003 au 2004 kama sijasahau kuna mbuzi mmoja yeye haridhiki yani. Hata apewe majani vipi ataruka tu kwenda kujilia huko. Sasa akaruka zizi si akajiumiza kifuani. Aisee kesho yake mzee ananiita eti kwa nini mbuzi ameruka akajiumiza ulikua wapi? Nilipewa kipondo cha haja mpaka nikatoka vidonda miguuni. Ilibeba muda mimi kunsamehe mzee. Yani alitaka nisiende shule nichunge mbuzi wake au niwe nawakagua aisee?. Ilibibeba kumjua Yesu kujifunza kusamehe. Yani sijamsahau yule mbuzi moaka leo.
 
Wafugaji mje huku mtupe visa vya visirani vya mbuzi wa kienyeji
Nakumbuka vituko vyao vingi sana maana tuliwahi kuwa nao tulipokuwa kijijin wakati huo nikiwa mdogo

Mbuzi ni kama binadamu ambavyo wapo wenye tabia mbali mbali na mbuzi ni hvyo hvyo kuna vimalaya humo kwenye kundi la mbuzi,kuna wezi,kuna wambeya,pia kuna vihele hele

Mbuzi anatakiwa achungwe na watoto maana mtu mzima hzo jogging hutaziweza

Mbuzi vihele hele,nakumbuka tulikuwa na mbuzi wengi lakin ukichelewa kuwapeleka machungani kuna wale mbuzi wachache katika kundi watalia na kupiga kelele ili wazazi wawasikie ili wawaambie muwapeleke machungani

Mbuzi malaya,kuna vile vidume vidogo huwa vinatabia ya kupiga kelele ya kupanda jike usiku kucha na wakati hata vikipewa mbususu haviwezi kuifikia,pia wapo majike ambao wao kila mara utakuwa unawaona wanayapanda madume(ila baada ya kupata elimu niligundua kumbe huwa wanakuwa kwenye heat)

Mbuzi wezi,hawa huwa ni wajanja wajanja sana muda wote hawawazi kula nyasi wanataka kula vya kuiba mashambani,huwa na tabia ya kuwapiga pembe wenzao kama wakiwa karibu na mazao ili wakimbilie kwenye mazao,kipindi hicho nakumbuka tulikuwa tusipofunga vizur mlango wa banda basi usiku wanatoka,tulikuwa tukiwakamata tunawapanda kama farasi,na unapompanda inabid kuwa makin sana maana anakimbia sana na anakuwa na tabia ya kupita karibu na visiki au ukuta ili ujipige pale uumie,
bAada ya kuwajulia wakati wa kwenda kuwachunga ili wasisumbue sana tulikuwa tunaenda na kamba,wale wasumbufu tunawatia kamba
Nakumbuka nilkuwa nikiwapeleka machungani lazima nipoteze mbuzi,inabid niwarudishe nyumban ili nikamsake huyo/hao waliopotea

Katika story za wana jamaa mmoja aliwah niambia kuwa wao walikuwa wanawang'oa meno baadhi ya mbuzi wasumbufu,wakiwapeleka kunywa maji wanaanza kumshika mmoja mmoja wanamgonga na jiwe mpaka jino linatoka au wanamkamata wanamzamisha kichwa kwenye maji kwa muda ndo wanamtoa,hao waliokuwa wanatolewa meno itamchukua siku hata tatu atakuwa ametulia sana na hali majani sana kama siku zingine

TUlikuwa tusipowapatia maji ya kutosha,ile jioni wakati wa kuwarudisha walikuwa wakifika nyumban wanakuwa na fujo balaa watalazimisha mpaka waingie ndani,na wataangusha viti na kumwaga maji

Mbuzi sina hamu nao,nimechapwa sana enzi hzo kwasababu ya hawa wapuuzi pamoja na kwamba mimi nilikuwa mtoto mpole sana

wAlinifanya hata nisipate muda wa kucheza mpira hadi leo nikiambiwa nipige mpira naanguka tu mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…