Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Mimi Hadi leo Nina kovu nilipigwa na pembe nilipokua mdogo.
Kuna kipindi nilimpanda mgongoni ,aisee akaanza kutimua mbio kuelekea kwenye miba, niliokotwa Kama Yesu vile alivyokuwa katoka kusulubiwa!!mwili una vidonda balaa!!

Ila nilikua napenda pale vitoto vidogo vilivyokuwa vikiingia kwenye shimo la choo halafu unaenda kuviokoa.
Unafunga kitanzi halfu unaingiza shimoni huku ukimulika na tochi
Wakat anakuburuza walio pembeni walikuwa wanashangilia kumbe wewe mda huo unakinywea kikombe
 
Mbuzi watukutu ila nawapenda sana kuwafuga.

Enzi hizo tunawachunga tulikuwa tunawavalisha nguo, kaptula na shati, sketi nk [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]... yaani hata uwe na hasira ya dunia nzima utacheka hadi mbavu zikuume
 
Nimewavunja sana hao miguu, mbuzi na ng'ombe nimechunga sana.
Bora ufuge kondoo kuliko hao vicheche.

Wakishazoea kulisha shamba fulani, ukiwa njiani unawaswaga wanatimua mbio hata kama ni umbali wa kilometa 3 mbele. Inabidi ukimbizane nao na lazima utakuta wameshaharibu tu.

Raha ya kufuga hao ni nyama, baba alikuwa akichinja kila wiki mbuzi.

Nb: ukitaka kuwa mfugaji wa hutu "tushenzi" basi uwe na eneo kubwa vinginevyo kila siku utaitwa kwa mwenyekiti au mtendaji kujibu mashitaka ya kuharibu mazao ya watu.[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]kesi nyingi vijijini kanda ya ziwa ni za mbuzi kuharibu mazao
 
Aiseee nimecheka hadi mbavu zinauma.
Binafsi hawa wanyama nimewachunga sana toka nikiwa mdogo Kama miaka 14 hv.
Aiseee asikwambie mtu Mbuzi ni shidaaa.
Mm Baba yetu Alikuwa na mbuzi kama 130 hv Ila cha moto nilikiona yaan wanakera, wanamakusudi hawa viumbe, wana nongwa unahitahiji uvumilivu wa 5G kuwafuga maaana niliishia kumvunja kiuno mbuzi mmoja ambaye alikuwa kiranja wa wenzake kunisumbua. Ni Hadith ndefu sitak hata kukumbuka Ila wanaowafuga hawa viumbe wawajengewe sanamu la heshima aisee.
Na ww mtoa mada ubarikiwe umeona mbali sana japo kuna watu humu hawatak kuelewa wanadhani umetumia code [emoji1787][emoji1787][emoji1787]maana kuna mbuzi watu wao ni shida zaidi [emoji1787][emoji1787]
 
Ila mikoa mingine noma Mbuzi 50 walipikutika mwezi mmoja, yani mbuzi anapatwa na kichaa, ukimpasua unakuta hadi irizi,

Pia kuna watu noma, waroho ata mbuzi kajifia hadi anaanza kuaribika ila wanakula tu....

Dah umenikumbusha. Miaka kama mitatu nyuma nilijaribu kufuga mbuzi kijiji kimoja cha waha kule chato kwa mwendazake. Mbuzi walikuwa wanauawa kwa sumu balaa! Nilichanganya na makundi ya wengine ila wakawa wanakufa wa kwangu pekee! Nilivyochunguza nikaambiwa jamii ya pale (ni ya kimasikini) ina wivu sana na haitaki maendeleo ya wageni. Nikaambiwa "hata wewe mwenyewe ukizubaa utatembea"!

Ukiwagawia mzoga wa mbuzi wachinje wanagombea nyama balaa, haijalishi mbuzi alidhoofika kiasi gani.

Kilichonishangaza zaidi wengi wao wanakula hata kitoto cha mbuzi kilichokufa wakati wa kuzaliwa! Yaani kaulimbiu yao nyama ni nyama!

Waha Mungu anawaona! Sijui huko Kigoma kwenyewe ndo hali ipoje, maana ile sample ilinistaajabisha
 
Back
Top Bottom