Ukitaka kujua ofisi unayotaka kufanya kazi, wafanyakazi wana hali gani, wewe tazama parking. Baaasi

Acha ushamba utakufa masikini nausije kupost unanuka umasikini. Warren Buffet anatembea kwa miguu kwenda kwa mishe zake na ni tajiri 1 acha ushamba
Ndugu uelewa wako mdogo.
Sijaleta mada kutoa ushauri wa kiuchumi au kuonyesha assets zangu
Just nilikuwa natoa picha mbili za ofisi mbili tofauti zinazoonyesha hali ya maisha ya watumishi wake
 
Nazungumzia picha za ofisi mbili ndani ya jamhuri ya Tanzania zenye hali tofauti ya maisha kwa wafanyakazi wake. Sitoi ushauri wa maisha kwamba Jenga lodge, nyumba, bar au gari.
 
Mimi ninako kaist ila nakapaki nje ya ofisi kwenye kijiwe cha kahawa, sipendi bosi wangu aione.
 
Kazini kwetu hakuna Gari kata nzima analo diwani tu, yalobaki ni huwa yanapita tu maana kuna barabara kuu ya Mkoa.

Vituo vyote vya Afya, Shule zote za Msingi na Sekondari mpaka office za serkali.

#Tunaomba pole au tuache kazi...?
 
Kuna pahala nilifanya kazi...watu wote wana magari .lakini hakuna anayepaki gari ofisini...........
Parking ipo kubwa ila tupu.....ukiona gari jua ni mteja....au mgeni.......
 
Kwenye kampuni za wachina utakuta gari moja tu ya meneja.wengine mtakuja na boda
 
Hizo zinaitwa ofisi sukuma siku..
 
Ni mtazamo wako tu mkuu.......wengine wanasomesha ,wanahudumia wazazi ,wanajenga ,wameinvest kwenye bizness.
 
Kuna chama cha ushirika kagera KCU 1990. Pale ukienda utakuta magari mawili au matatu parking tena ya milioni kumi, ndani furnitures zimechoka Cpu cijui pentium hipi , photocopy machine wanatumia copy writter Ila wanakula maisha BOT wakasome.
Hapo KCU napaelewa sana wale wazee acha kabisa wanazuga Ili wasishtukiwe
 
Kuna kampuni flani nilipata kazi mfanyakazi mwenzangu nilikotoka akaniambia ukifika kule ukiona parking ya magari mengi ya wafanyakazi tena wa chini usije shangaa.
Kweli nikafika huku yaani ukiwa na RAV4 ni usafiri tu wa kawaida
Asubuhi ukija kazini unaweza kosa nafasi ya ku paki
Hapa mtu kukuliza je gari yako ni ya aina gani hata kama hajui una gari ni jambo la kawaida
Ni sawa na kwa sasa mtu akuambie aise nipe namba yako ya simu tuwasiliane ni swali la kawaida tu anajua lazima unayo.
Ila tu ndugu zangu niwaambie mtu kuwa na gari sio kipimo halisi cha utajiri au mafanikio ya mtu maana mwingine kainunua kwa mkopo anaishi kwa tabu sana kwa ku bomu na familia inaishi kwa tabu sana.
Ila pamoja na yote ndugu zangu kwa dunia ya sasa gari sasa sio luxury ni necessity kama vile simu ya mkononi ila tuache utani gari uzuri wake linaficha umasikini jamani.
 
ASANTE BABA MWENYEGARI. Shukurani hizi zinatoka kwangu Baba mwenyenyumba wako.
 
Haya mambo ndiyo yanasababisha watu waingie mikopo migumu ya magari .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…