Ukitaka kuuza gari ya Ulaya/Marekani ni changamoto sana

Ukitaka kuuza gari ya Ulaya/Marekani ni changamoto sana

Kiufupi badala ya kununua Discovery au Toureg tafuta Prado
Badala ya kununua Ford Everest tafuta Surf au Fortuner
Badala ya kununua Ford Ranger au Amarok tafuta Hilux
Badala ya kununua Range Rover tafuta Land Cruiser VX

Utakuja kulia kama mfuko wako sio mnene.
 
Mchina ana gari gani ya chini ambayo wabongo wanatembelea zaidi ya Yutong,Howo, Faw, Shacman, Higer na tule tugari twa polisi kama Prado?

Mchina ana Pick Up fulani zinaitwa JMC Vigus

Halafu kuna Haval H9 bonge moja la SUV.

Hizi ndio watu wanazowanazo humu mtaani.

Katika hizo mbili nimekutana na JMC Vigus, aiseee hii gari ina umeme, mzungu anasubiri.
 
Tunaitwa Haval. Na Mchina katoa new model yake,kali haswa kwa muonekano na latest features. Anapambana hahika
Ila kwa gari za mchina ninazofahamu, aiseeee hayupo nyuma kwenye tech.

Halafu mchina haweki maengine makubwaaaaa au maturbo kwenye gari zake.

Gari zake zina engines za kawaida ila zinakuwa na tech za maana. Hivyo overall inakuwa na performance nzuri.
 
Ishu sio tu gari ya Japan, hapa Tanzania ukiwa na gari yoyote ambayo sio TOYOTA (hata kama ni ya Japan mfano Honda, Mazda, Nissan nk) utapata tabu sana kuiuza! Sijui toyota walitukamata wapi masikio kudhani kwamba gari zao ndio bora kuliko zote?
Honda ni moja kati ya gati reliable sana.

Kinachowapa watu kigugumizi ni upatikanaji wa spea.
 
Back
Top Bottom