Ukitaka kuuza gari ya Ulaya/Marekani ni changamoto sana

Ukitaka kuuza gari ya Ulaya/Marekani ni changamoto sana

Ishu sio tu gari ya Japan, hapa Tanzania ukiwa na gari yoyote ambayo sio TOYOTA (hata kama ni ya Japan mfano Honda, Mazda, Nissan nk) utapata tabu sana kuiuza! Sijui toyota walitukamata wapi masikio kudhani kwamba gari zao ndio bora kuliko zote?
Ni zaidi ya miaka 50 iliyopita enzi za Nyerere serikali ya Tanzania iliingia mikataba mingi na serikali ya Japan kwenye miradi mbalimbali ikiwemo kampuni ya Toyota hii ndiyo kampuni ya Kwanza kufanya biashara na serikali yetu kwenye ishu za magari.
Kampuni ya Toyota bado inaendelea kufanya biashara na Tanzania mpaka Leo,watu wanazaliwa wanakuta magari ya Toyota yapo serikali na maduka ya spare parts yapo mtaani ndiyo maana ilikuwa rahisi Kwa wananchi kununua Toyota tofauti na magari mengine..
 
Ni kweli mkuu.
Amazon kwa 20ml hata kama ni mbovu labda
Kule kupatana ziko Amazon mpk za kwny mil 17 huko na nilishaikaguaga moja na ilikua poa kabisa.Tatizo la wabongo ni 1 tu wanapenda kuangalia upuuzi wa No.,ikishakua no.A au B etc hio Gari Hata iwe Kali vipi jiandae kuiuza kwa hasara tu.
 
Ila kwa gari za mchina ninazofahamu, aiseeee hayupo nyuma kwenye tech.

Halafu mchina haweki maengine makubwaaaaa au maturbo kwenye gari zake.

Gari zake zina engines za kawaida ila zinakuwa na tech za maana. Hivyo overall inakuwa na performance nzuri.
Anazi underpower sana gari zake so hazina speed
 
Kule kupatana ziko Amazon mpk za kwny mil 17 huko na nilishaikaguaga moja na ilikua poa kabisa.Tatizo la wabongo ni 1 tu wanapenda kuangalia upuuzi wa No.,ikishakua no.A au B etc hio Gari Hata iwe Kali vipi jiandae kuiuza kwa hasara tu.
Kuna gari ngumu kama landcruiser hata ikiwa A na imetunzwa mimi na beba, ikiwa injini na body vinesimama huwa sijali najua siri za hizi chuma za kale
 
Ishu sio tu gari ya Japan, hapa Tanzania ukiwa na gari yoyote ambayo sio TOYOTA (hata kama ni ya Japan mfano Honda, Mazda, Nissan nk) utapata tabu sana kuiuza! Sijui toyota walitukamata wapi masikio kudhani kwamba gari zao ndio bora kuliko zote?
haya ni matokeo chanya ya kile kipindi cha wanyama ITV.
Kweli marketing inanguvu sana. Mpaka kizazi kimerithishana.
 
Back
Top Bottom