Kilimbatzz
JF-Expert Member
- Feb 11, 2023
- 9,134
- 14,593
🤔🤔🤔🤔🤔Wengi wana uwezo wa kuujua ukweli lakini sio wote wanaopenda kuufata.
Kwa mfano
Kwenye circle ya kimahusiano, mwanamke anaweza kutongozwa na wanaume tofauti tofauti.
Katika hao anaweza akamuona mwanaume ambaye anajua kabisa mwanaume huyu ni husband material.
Mwanaume ambaye ana ambitions za kimaisha (husler) anayeweza kujenga naye maisha.
Lakini mwanamke akaamua kuachana naye kwasababu ya vitu vidogo tu kama muonekano (marafiki zake watamuonaje) au ni mtu fulani hivi ambaye hajichanganyi kwenye viwanja vya starehe ambapo huko anaweza kuvimbiana na marafiki zake (showoffs)
Halafu akaenda kujenga mahusiano na mwanaume mwingine ambaye anafahamu kabisa kuwa huyu si muoaji, ila kwakua ni cheki bob anapiga pamba kali na kuvaa ma chain ya silver anaona sasa huyu ndio atanifaa.