Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Ni mtihani kweli, unaweza kumsalimia mtu habar za saa hizi akakushushua kwa kukuona hustahili kumuamkia hivyo anataka shikamoo. Kuna wengine nao wanakuamkia shikamoo huku unawaona hawastahili kukupa shikamoo, ni wakubwa. Ishu nyingine inakuja kwenye kutongoza, unataka kutongoza demu mara anakusalimia shikamoo wakati we ulitaka akusalimie mambo vipi? Confidence ya kutongoza inashuka kwa kuona huyo demu ni mdogo sana kwako
Ni sahihi kabisa,yani hapo mtihani sehemu mbili unaweza kuamkiwa na wakubwa kwako,nawe waweza amkia wadogo kwako,,ni shidaaa!
 
Mimi huwa nasema pole na kazi ili kukwepa kutoa shkamoo 😁 hasara ni pale kuna vibinti virembo kabisa navyo vinanipa shkamoo🥲
Haaahaa 😆 ☺️ SHIKAMOO ya Binti naiitikia na mbususu / papuchi unaiomba vizuri TU.

Wanawake wa dasalama,pwani ,Tanga hawapendi uwasalimie SHIKAMOO wanaona kama unawazeeshaa 😁 😆 Hawa wasalimie salamaleko au habari ama mambo vipi..
 
View attachment 3347358

Hiyo namba ndio mwaka wangu wa kuzaliwa,ulivyokuwa na hamu ya kujua Etugrul Bey ana miaka mingapi utapiga hesabu bila aibu ujue nina miaka mingapi,usijichoshe hii may nimetimiza miaka 46,je kuna mwenye shida na hilo?

Nakumbuka nikiwa Chuoni kuna mtu wa Library kipindi hicho alikuwa kwenye 40's akasema ukiwa na umri huu ni mtihani,unaweza usisalimie watu kwa kuwaona mnalingana au ukajikuta unawasalimia wadogo zako kwa umri

Aisee sasa namuelewa sana,kwanza namshukuru Allah nimejaaliwa mvi za kutosha tu,ishu ni kwamba huwa sometime nashindwa kuwaamkia watu nisio wajua kwakuwa naona kama nipo sawa nao tu,lakini sometime najishtukia naona kama nilipaswa kuwaamkia

Hii salamu ya Shikamoo sio poa kwasababu inamtaka mdogo amsalimie mkubwa,lau tungekuwa na salamu flani hivi ambayo haibagui mkubwa na mdogo ingekuwa poa sana, kwa mfano salamu ya "habari za asubuhi au mchana au jioni" haina mfumo wa mkubwa au mdogo

Najua watoto wa elfu mbili hamuelewi hili kama ambavyo nami sikumuelewa yule jamaa wa kule library kule Chuoni,sasa nimemuelewa,nanyi pia mtakuja kumuelewa Etugrul Bey siku moja when u turn 40's

Kama kuna mtu ambaye anamjua alieanzisha hii salamu aniambie,kwani namhitaji huyu mtu anipe maelezo ya kina ilikuwaje wameturithisha hii salamu.

Ni hayo tu!
Hii inachanganya sana aisee,sisi kinyakyusa Haina mkubwa salamu, ugonile, ugonile full stop!
 
Haaahaa 😆 ☺️ SHIKAMOO ya Binti naiitikia na mbususu / papuchi unaiomba vizuri TU.

Wanawake wa dasalama,pwani ,Tanga hawapendi uwasalimie SHIKAMOO wanaona kama unawazeeshaa 😁 😆 Hawa wasalimie salamaleko au habari ama mambo vipi..
Dah sasa hivi unaweza salimia hata mtoto ,nasikia vitoto vya daslamu vinaumuka haraka🤔
 
Naungana na wewe aisee kama mtu sijamsoma bado napiga tu "habari" wakati anajibu namzingatia kuona amenizidi au vipi nimgongee hilo shikamoo lake...
Changamoto sana kuna wazee wa draft watu wazima kabisa niliwahi kuwasalimia wakaniuliza "unataka kutunyima nini" aah ndo nikafunga na vioo kabisa nikaacha hata kuwasalimia.
 
Back
Top Bottom