Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

"Habari za asubuhi" , "Mmeamkaje" n.k ni salamu zenye maana sana na kumaanisha kuliko hizi za shikamoo... tatizo wabongo mtaani wajinga wajinga ukimuambia mtu mzima "Habari ya leo", anasema umemdharau...
Kabisa! kuna dada aligoma kuniuzia dawa dukani kwake kisa nimemsalimia "za sahizi" akaanza kupayuka we si ni sawa na mtoto wangu tu sijui hivi mara vile anashirikisha hadi wateja wengine nikamwambia uhitaji wangu akasema hauzi hiyo dawa nikasema ok...nikaendelea kwingine.
 
Shida iko hapo expert wangu,watasema sasa hivi amejiona amekuwa hasalimii watu
 
Kabisa! kuna dada aligoma kuniuzia dawa dukani kwake kisa nimemsalimia "za sahizi" akaanza kupayuka we si ni sawa na mtoto wangu tu sijui hivi mara vile anashirikisha hadi wateja wengine nikamwambia uhitaji wangu akasema hauzi hiyo dawa nikasema ok...nikaendelea kwingine.
Huyo naye kavuka mipaka,anachukulia shikamoo kama pumzi ya uhai
 
Ni sahihi kabisa,yani hapo mtihani sehemu mbili unaweza kuamkiwa na wakubwa kwako,nawe waweza amkia wadogo kwako,,ni shidaaa!
huwa nashangaa sana, kuna wakati huwa nasalimiwa shikamoo na majimama na majibaba makubwa yamenizidi umri inabidi niitikie tu marahaba! Kwa sasa nimekuja na salamu zisizobagua umri, nazo ni jambo afande, jambo mtoto, jambo binti, jambo kijana, jambo baba/mama, habari za saa hizi, kwema?
 
Kabisa! kuna dada aligoma kuniuzia dawa dukani kwake kisa nimemsalimia "za sahizi" akaanza kupayuka we si ni sawa na mtoto wangu tu sijui hivi mara vile anashirikisha hadi wateja wengine nikamwambia uhitaji wangu akasema hauzi hiyo dawa nikasema ok...nikaendelea kwingine.
Shikamoo ifutwe..
Huwa sielewi maana yake..
Kuna shikamoo nyingine unaitoa lakini kwa mvutano sana na mkwaruzano wa mawazo ndani ya nafsi yako..

Kwa sisi wa kiume kuna wale wamama hawataki kuzeeka unakuta kajiachia kama binti aisee inakuwa ngumu sana kutoa shikamoo..
 
Itakua Kuna jinsi ULIVYO toa salamu ungeitoa kwa unyenyekevu MKUBWA kabisa yaan usionyeshe kama ulimdharau or ume mu insult.

Kama umemwammbia MAMBO VP? MAMA WA KUKUZAA ATAONA KAMA UME MU INSULT
 
Uchebe huo😂😂

20250527_132524.jpg
 
View attachment 3347358

Hiyo namba ndio mwaka wangu wa kuzaliwa,ulivyokuwa na hamu ya kujua Etugrul Bey ana miaka mingapi utapiga hesabu bila aibu ujue nina miaka mingapi,usijichoshe hii may nimetimiza miaka 46,je kuna mwenye shida na hilo?

Nakumbuka nikiwa Chuoni kuna mtu wa Library kipindi hicho alikuwa kwenye 40's akasema ukiwa na umri huu ni mtihani,unaweza usisalimie watu kwa kuwaona mnalingana au ukajikuta unawasalimia wadogo zako kwa umri

Aisee sasa namuelewa sana,kwanza namshukuru Allah nimejaaliwa mvi za kutosha tu,ishu ni kwamba huwa sometime nashindwa kuwaamkia watu nisio wajua kwakuwa naona kama nipo sawa nao tu,lakini sometime najishtukia naona kama nilipaswa kuwaamkia

Hii salamu ya Shikamoo sio poa kwasababu inamtaka mdogo amsalimie mkubwa,lau tungekuwa na salamu flani hivi ambayo haibagui mkubwa na mdogo ingekuwa poa sana, kwa mfano salamu ya "habari za asubuhi au mchana au jioni" haina mfumo wa mkubwa au mdogo

Najua watoto wa elfu mbili hamuelewi hili kama ambavyo nami sikumuelewa yule jamaa wa kule library kule Chuoni,sasa nimemuelewa,nanyi pia mtakuja kumuelewa Etugrul Bey siku moja when u turn 40's

Kama kuna mtu ambaye anamjua alieanzisha hii salamu aniambie,kwani namhitaji huyu mtu anipe maelezo ya kina ilikuwaje wameturithisha hii salamu.

Ni hayo tu!
Unazaliwa tupo makazini! Kweli JF kiboko
 
Shikamoo ifutwe..
Huwa sielewi maana yake..
Kuna shikamoo nyingine unaitoa lakini kwa mvutano sana na mkwaruzano wa mawazo ndani ya nafsi yako..

Kwa sisi wa kiume kuna wale wamama hawataki kuzeeka unakuta kajiachia kama binti aisee inakuwa ngumu sana kutoa shikamoo..
Yani nakuelewa sana expert wangu
 
Itakua Kuna jinsi ULIVYO toa salamu ungeitoa kwa unyenyekevu MKUBWA kabisa yaan usionyeshe kama ulimdharau or ume mu insult.

Kama umemwammbia MAMBO VP? MAMA WA KUKUZAA ATAONA KAMA UME MU INSULT
Yawezekana lakini salamu niliitoa kwa heshima zote na hakuwa mtu mzima wa kunizaa sijui tu ndo alivyo au mood ilikuwa mbovu sikuhiyo.
 
Back
Top Bottom