Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

"Mimi tangia zamani huwa nasalimia hivi"

"Habari ya uzima " hii salamu nilianza kuitumia chuoni baada ya kupata rafiki mlokole.

Kwanza inapendwa Sana hii salamu Sana na ukimsaimia MTU anakuona upo na maadili kwake
 
Hakuna kitu ambacho sipendi kama kusalimiwa shikamoo yaani sipendi.
Na mimi pia huwa sisalimii kabisa watu hiyo salamu.
Hadi nione kabisa mtu kazeeka kabisa kajichokea anaenda kuwa babu au bibi yaani kifupi kasha jikubali kuwa ni mzee ndio nasalimia.
 
View attachment 3347358

Hiyo namba ndio mwaka wangu wa kuzaliwa,ulivyokuwa na hamu ya kujua Etugrul Bey ana miaka mingapi utapiga hesabu bila aibu ujue nina miaka mingapi,usijichoshe hii may nimetimiza miaka 46,je kuna mwenye shida na hilo?

Nakumbuka nikiwa Chuoni kuna mtu wa Library kipindi hicho alikuwa kwenye 40's akasema ukiwa na umri huu ni mtihani,unaweza usisalimie watu kwa kuwaona mnalingana au ukajikuta unawasalimia wadogo zako kwa umri

Aisee sasa namuelewa sana,kwanza namshukuru Allah nimejaaliwa mvi za kutosha tu,ishu ni kwamba huwa sometime nashindwa kuwaamkia watu nisio wajua kwakuwa naona kama nipo sawa nao tu,lakini sometime najishtukia naona kama nilipaswa kuwaamkia

Hii salamu ya Shikamoo sio poa kwasababu inamtaka mdogo amsalimie mkubwa,lau tungekuwa na salamu flani hivi ambayo haibagui mkubwa na mdogo ingekuwa poa sana, kwa mfano salamu ya "habari za asubuhi au mchana au jioni" haina mfumo wa mkubwa au mdogo

Najua watoto wa elfu mbili hamuelewi hili kama ambavyo nami sikumuelewa yule jamaa wa kule library kule Chuoni,sasa nimemuelewa,nanyi pia mtakuja kumuelewa Etugrul Bey siku moja when u turn 40's

Kama kuna mtu ambaye anamjua alieanzisha hii salamu aniambie,kwani namhitaji huyu mtu anipe maelezo ya kina ilikuwaje wameturithisha hii salamu.

Ni hayo tu!
Salamu ya habari ni nzuri zaidi kwa mtu usiemjua, hiyo shkamo salimia wakubwa unaowajua wenye umli sawa na mzazi wako, lakini mnaokutaka just say to hello, hi, habari, za saa hivi full stop. Me watoto angu wote kusalimia shkamo ndo walishashindwaga kitambo, labda mzazi, bibi, babu, aunty, uncle that ok
 
Hahaha hii inanikuta mimi kuna mda nawasalimia wadogo zangu kabisa siku hizi watu wanakua haraka sana hasa wanawake hahahaha kuna profesa mmoja nikimuamkia shikamoo haitikii na madam flani ivi alikua mwalimu wangu wa kozi hahah
 
Nasalimia kwa unyenyekevu sjui so far naonekana na heshima sana kumbe kawaida tuu 😂
Haaahaa 😆 ☺️ kuna siku Kuna ka brother kangu kana MWILI mdogo mdogo sikuwai kuonana nako tangia nikiwa mdogo.

Siku moja nikawa nimeenda kinyerezi nikamkuta kavaa jezi yake yupo na brother angu mmoja nikasalimia habari za leo kajamaa kakagoma kakasema nikape shikamoo tukalumbana nikakasalimia kwa shingo upande.

Baadae ndio brother mwingine AKAJA aka ni introduce kwake ni brother mkubwa na ana wadhifa kubwa tuu mpaka NIKAONA AIBU Ila Kuna watu Wana miili midogo midogo mpaka wanaweza kunyimwa kiti ugenini 🤓
 
Kuna kipindi niliamkia sana makinda huko kanda ya ziwa. Siku moja mama mmoja akasema kijana wangu nakuona unaamkia sana wadogo zako hata kama unataka kuoa usukumani usifanye hivyo. Nisilikia aibu sana tangu siku hiyo hadi leo salamu yangu kubwa ni habari.

Na nikikutana na mtu simuelewi naanza kwa kuchangamsha maongezi bila salam. Isitoshe wengi siku hizi hawaipendi.
 
Back
Top Bottom