Ukiweka sumu kwenye chakula changu, hata kama sumu hiyo inaua ndani ya dakika 1, sifi. Sababu hii hapa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ndugu yangu, kumbuka kila wakati, katika dunia hii sio wote wanaofurahia mafanikio yako ya kimaisha, ya kikazi au ya kibiashara. Kwa sababu hiyo yamkini kuna watu wanapanga mbinu za kukuangamiza. Na wengine wanaweza kukuchukia tu hata kama huna pesa au cheo, wakatafuta njia ya kukuondoa duniani.

Njia inayotumiwa na waovu kukatisha maisha ya watu kimya kimya ni kuweka sumu kwenye chakula au kinywaji. Unaponaje sasa katika hali hii? Utakuwa unatembea na daktari wa kupima maji na chakula chako kabla hujala? Na je, daktari akipitiwa akasema chakula hakina sumu kumbe sumu ipo, utaponaje?

Nakupa siri ya ushindi! Ukiokoka, ukawekewa sumu kwenye chakula – sumu hiyo haitakudhuru kabisa.
Marko 16:17-18
Na ishara hizi zitafuatana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.

Hiyo ndiyo sababu kwanini siwezi kufa ukiniwekea sumu kwenye chakula.
Kuokoka ni jambo lenye faida sana. Ndio maana shetani anatumia mbinu nyingi kuwadanganya na kuwashawishi watu wasiokoke - eti kuokoka ni ujinga! Ujinga?! Shetani anajua, watu wakiokoka wataishi maisha yenye heri hapa duniani na mbinguni. Kataa uongo wa shetani, kwa Jina la Yesu.

Ukweli ndio huo, mimi nimeokoka. Hivyo ukiniwekea sumu kwenye chakula changu ili nife, utasubiri sana! 🙂
 
Tahadhari:
Kama umeokoka, usinywe sumu kwa makusudi. Utakuwa unamjaribu Mungu na hapo unaweza kufa mara moja! Mungu atakulinda iwapo utakula au kunywa kitu chenye sumu bila wewe kujua.

Luka 4:12
Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”
 
Umeandika as if walokole hawatakiwi kufa. Kifo kipo tuu ... uwe tayari kufa kwa njia yoyote kama muda umefika hiyo sumu itakuua tu. Mtu aliyeokoka wala hawazi issue ya kifo maana ni njia ya kwenda mapumzikoni. Okoka upya
 
Ukiokoka unapata sio tu tiketi ya kwenda mbinguni; bali pia ulinzi na neema ya Mungu. Wanaoishi ndani ya Kristo wanalindwa kwa namna ya ajabu.

Katika Matendo ya Mitume 28, tunaona jinsi Paulo alivyong’atwa na nyoka mwenye sumu kali, lakini hakupatwa na madhara yoyote. Watu walidhani atakufa mara moja, lakini alibaki salama. Huo ni mfano wa ulinzi wa Mungu kwa waaminio.
 
Umeandika as if walokole hawatakiwi kufa. Kifo kipo tuu ... uwe tayari kufa kwa njia yoyote kama muda umefika hiyo sumu itakuua tu. Mtu aliyeokoka wala hawazi issue ya kifo maana ni njia ya kwenda mapumzikoni. Okoka upya
Wafilipi : 1 : 21 - Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
 
Umeandika as if walokole hawatakiwi kufa. Kifo kipo tuu
Ndiyo. Kifo kipo tu lakini mimi nakataa kufa kwa sumu kabla ya wakati wangu.
Zaburi 90:10
Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, au miaka themanini ikiwa tuna nguvu.

Kama wewe unakubali mtu aukatishe uhai wako kabla ya umri huo, sawa. Kaa tayari kufa. Lakini mimi siko tayari sumu iniue kabla ya wakati huo, maana kazi aliyonipa Yesu bado sijaimaliza!
 
Hivi kuoka maana yake nini ukiwa bado unaishi kwenye hii dunia iliyojaa laana kwakweli hii maana ya kuokoka huwa inanitatiza sana hivi unawezaje kujiakikishia kuwa umeokoka.
 
Solution ya yote ni kufanya tahajudi kwa masaa 24 bila kuchoka, hapo roho wa MUNGU, ndio atakuongoza na kukuepusha na mabaya yote. Hakuna cha dini yoyote, wala ulokole unaoweza kukuokoa. Sababu MUNGU ni upendo na wala hana dini yoyote.
 
Kufa ni faida kama kazi uliyopewa umeimaliza. Hujui kwamba kazi yako itapimwa ndio upate thawabu. Wewe umeishamtumikia Mungu kama Paulo kiasi cha kuweza kusema kufa ni faida?
Mkuu, nimeisindikizia tu comment ya mkuu hapo kwa hicho kifungu kama rejea.
 
Back
Top Bottom