Ukiweka sumu kwenye chakula changu, hata kama sumu hiyo inaua ndani ya dakika 1, sifi. Sababu hii hapa

Ukiweka sumu kwenye chakula changu, hata kama sumu hiyo inaua ndani ya dakika 1, sifi. Sababu hii hapa

Kama hujui unapata wapi nguvu ya kuongelea kitu usichojua maana yake huoni unakua kichekesho?
😁😁
Kichekesho ni mimi ninaeongelea au wewe unaetumia biblia ambayo ni kitu ambacho hakitambuliki kwenye maandiko?
 
Tahadhari:
Kama umeokoka, usinywe sumu kwa makusudi. Utakuwa unamjaribu Mungu na hapo unaweza kufa mara moja! Mungu atakulinda iwapo utakula au kunywa kitu chenye sumu bila wewe kujua.

Luka 4:12
Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”
Unajitekenya halafu unacheka mwenyewe.
 
Mtu aliyeokoka wala hawazi issue ya kifo maana ni njia ya kwenda mapumzikoni.
Unaenda kupumzika? Umeisha waleta watu wangapi kwa Yesu? Umeishaenda kwa mataifa yote kuhubiri Injili kama Yesu alivyoagiza? Kama bado, unaenda kupumzika nini ndugu? Fanya kazi ya Bwana. Usimruhusu shetani ayakatize maisha yako. Mavuno ni mengi watenda kazi ni wachache.
 
Sasa unajidanganya utaishi milele hapa duniani? yaani unajizima data hujui kufa ni kupumzika mlokole wewe.... kweli unajitekenya mwenyewe halafu unacheka. Hakuna shetani wa kukatisha maisha ya mtu kama Mungu hajaamua
 
Ndiyo. Kifo kipo tu lakini mimi nakataa kufa kwa sumu kabla ya wakati wangu.
Zaburi 90:10
Siku zetu za kuishi ni miaka sabini, au miaka themanini ikiwa tuna nguvu.

Kama wewe unakubali mtu aukatishe uhai wako kabla ya umri huo, sawa. Kaa tayari kufa. Lakini mimi siko tayari sumu iniue kabla ya wakati huo, maana kazi aliyonipa Yesu bado sijaimaliza!
Nini kinakufanya ukae na kuwaza kufa kwa sumu??? kwa nini huwazi kufa kwa kuangukiwa na nyumba unayolala? acha kuwaza kifo... utaokota makopo soon
 
Wafilipi : 1 : 21 - Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.
Sawa kabisaaaa. mwambieni mlokole wetu asiwaze kitu ambacho NI LAZIMA KITATOKEA hata iweje.
 
Sasa unajidanganya utaishi milele hapa duniani?
Nani kasema ataishi milele duniani? Nimesema miaka yetu ni 70 au 80 tukiwa na nguvu, hivyo lazima tuizime kwa Jina la Yesu, mishale yote ya moto kutoka kwa shetani anayetafuta kuyakatiza maisha yetu. Maandiko yanatuambia tukeshe kwakuwa mshtaki wetu Ibilisi anazunguka kama simba akitafuta mtu wa kummeza.
yaani unajizima data hujui kufa ni kupumzika mlokole wewe....
Watu wanapumzika baada ya kufanya kazi. Kazi aliyonipa Yesu ni kubwa sana, sidhani hata robo yake kama nimeitimiza, Wewe unataka nikapumzike nini. Wewe kama umeishatimiza agizo kuu la Yesu, sawa, nenda kapumzike.
Hakuna shetani wa kukatisha maisha ya mtu kama Mungu hajaamua
Hujasoma Luka 4:29?
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini. Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.

Hapo walitaka kukatisha uhai wake lakini Yesu hakukubali kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika.
Mungu ametupa silaha na mamlaka ya kumpinga shetani. Usipovaa silaha hizo na kumpinga shetani anaweza kuyakatiza maisha yako. Ukiwa mzembe kuomba, kama husomi Neno, kama imani yako ni haba, utazama ndugu. Watu wanaokufa sio kwamba wote Mungu ameamua. Maandiko yanasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Umenipata?
 
Nini kinakufanya ukae na kuwaza kufa kwa sumu???
Ukisoma uzi tafakari kwanza lengo la uzi kabla ya kukurupuka ku-comment. Lengo langu ni kuwatahadharisha watu kwamba wakifanikiwa kikazi, kibiashara nk watambue kuwa kuna watu wasiofurahia mafanikio yao. Watu hao ndio wanaoweza kuwawekea sumu ili wafe. Bila wokovu, ukiwekewa sumu utakufa tu. Lakini ukiwa na Yesu sumu haifanyi kazi kwa Jina la Yesu. Hivyo wakitaka kuwa salama watubu na kumwamini Yesu ili ishara hiyo ifuatane nao. Sio kwamba nawaza kufa.
 
Ndugu yangu, kumbuka kila wakati, katika dunia hii sio wote wanaofurahia mafanikio yako ya kimaisha, ya kikazi au ya kibiashara. Kwa sababu hiyo yamkini kuna watu wanapanga mbinu za kukuangamiza. Na wengine wanaweza kukuchukia tu hata kama huna pesa au cheo, wakatafuta njia ya kukuondoa duniani.

Njia inayotumiwa na waovu kukatisha maisha ya watu kimya kimya ni kuweka sumu kwenye chakula au kinywaji. Unaponaje sasa katika hali hii? Utakuwa unatembea na daktari wa kupima maji na chakula chako kabla hujala? Na je, daktari akipitiwa akasema chakula hakina sumu kumbe sumu ipo, utaponaje?

Nakupa siri ya ushindi! Ukiokoka, ukawekewa sumu kwenye chakula – sumu hiyo haitakudhuru kabisa.
Marko 16:17-18
Na ishara hizi zitafuatana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.

Hiyo ndiyo sababu kwanini siwezi kufa ukiniwekea sumu kwenye chakula.
Kuokoka ni jambo lenye faida sana. Ndio maana shetani anatumia mbinu nyingi kuwadanganya na kuwashawishi watu wasiokoke - eti kuokoka ni ujinga! Ujinga?! Shetani anajua, watu wakiokoka wataishi maisha yenye heri hapa duniani na mbinguni. Kataa uongo wa shetani, kwa Jina la Yesu.

Ukweli ndio huo, mimi nimeokoka. Hivyo ukiniwekea sumu kwenye chakula changu ili nife, utasubiri sana! 🙂
Siku hizi ukitaka kuwa mlokole ni lazima ujitoe ufahamu kwanza kama Komandoo Mashimo😀
 
Ufungwe bomu tuone km kweli mkuu..!!
Nikikubali kufungwa bomu ili wewe uone km kweli ntakuwa namjaribu Mungu. Mungu hapendi tumjaribu.

Lakini wewe ukinifunga bomu ili unimalize kabla saa yangu haijawadia, hilo bomu linaweza lisilipuke. Kumbuka Petro alivyofungwa gerezani. Minyororo ilikatika na lango la chuma lilifunguka lenyewe, Petro akaenda zake. Askari waliokuwa wanamlinda hawakujua hata ametoka saa ngapi. Soma Matendo 12:6-10. Mungu ni mkuu sana. Hakuna jambo asiloweza kufanya.
 
Kichekesho ni mimi ninaeongelea au wewe unaetumia biblia ambayo ni kitu ambacho hakitambuliki kwenye maandiko?
Itoshe tu kusema hujui unachokisema
Kaa chini jifunze acha ujinga,
Biblia ni mkusanyiko wa Vitabu
Neno Biblia kiasili ni la kigiriki likimaanisha Vitabu au Scrolls,

Mjumuisho huo wa Vitabu au maandiko matakatifu unajumuisha,
Historia,unabii,Mashairi na Hekima
Mwanzo kabla Biblia haijakuasanywa na kuwekwa kwenye mjumuisho mmoja ilikua kila scrolls inajitegemea yaani kila kipande kipo sehemu yake mpaka pale maendeleo ya kukusanya document yalipokuja ndio ikapatikana idea ya kuweka kwa pamoja Ili iwe rahisi kupata rejea,

Sasa wewe ndugu yangu Lucha unavyosema Biblia haitambuliki na maandiko unakua una maana gani wakati Ndio maandiko yenyewe?
😁😁
 
Ndugu yangu, kumbuka kila wakati, katika dunia hii sio wote wanaofurahia mafanikio yako ya kimaisha, ya kikazi au ya kibiashara. Kwa sababu hiyo yamkini kuna watu wanapanga mbinu za kukuangamiza. Na wengine wanaweza kukuchukia tu hata kama huna pesa au cheo, wakatafuta njia ya kukuondoa duniani.

Njia inayotumiwa na waovu kukatisha maisha ya watu kimya kimya ni kuweka sumu kwenye chakula au kinywaji. Unaponaje sasa katika hali hii? Utakuwa unatembea na daktari wa kupima maji na chakula chako kabla hujala? Na je, daktari akipitiwa akasema chakula hakina sumu kumbe sumu ipo, utaponaje?

Nakupa siri ya ushindi! Ukiokoka, ukawekewa sumu kwenye chakula – sumu hiyo haitakudhuru kabisa.
Marko 16:17-18
Na ishara hizi zitafuatana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.

Hiyo ndiyo sababu kwanini siwezi kufa ukiniwekea sumu kwenye chakula.
Kuokoka ni jambo lenye faida sana. Ndio maana shetani anatumia mbinu nyingi kuwadanganya na kuwashawishi watu wasiokoke - eti kuokoka ni ujinga! Ujinga?! Shetani anajua, watu wakiokoka wataishi maisha yenye heri hapa duniani na mbinguni. Kataa uongo wa shetani, kwa Jina la Yesu.

Ukweli ndio huo, mimi nimeokoka. Hivyo ukiniwekea sumu kwenye chakula changu ili nife, utasubiri sana! 🙂
Ila walokole huwa mnajifariji sana lakn kila siku tunawazika
 
Back
Top Bottom