Ukiweka sumu kwenye chakula changu, hata kama sumu hiyo inaua ndani ya dakika 1, sifi. Sababu hii hapa

Ukiweka sumu kwenye chakula changu, hata kama sumu hiyo inaua ndani ya dakika 1, sifi. Sababu hii hapa

Ndugu yangu, kumbuka kila wakati, katika dunia hii sio wote wanaofurahia mafanikio yako ya kimaisha, ya kikazi au ya kibiashara. Kwa sababu hiyo yamkini kuna watu wanapanga mbinu za kukuangamiza. Na wengine wanaweza kukuchukia tu hata kama huna pesa au cheo, wakatafuta njia ya kukuondoa duniani.

Njia inayotumiwa na waovu kukatisha maisha ya watu kimya kimya ni kuweka sumu kwenye chakula au kinywaji. Unaponaje sasa katika hali hii? Utakuwa unatembea na daktari wa kupima maji na chakula chako kabla hujala? Na je, daktari akipitiwa akasema chakula hakina sumu kumbe sumu ipo, utaponaje?

Nakupa siri ya ushindi! Ukiokoka, ukawekewa sumu kwenye chakula – sumu hiyo haitakudhuru kabisa.
Marko 16:17-18
Na ishara hizi zitafuatana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.

Hiyo ndiyo sababu kwanini siwezi kufa ukiniwekea sumu kwenye chakula.
Kuokoka ni jambo lenye faida sana. Ndio maana shetani anatumia mbinu nyingi kuwadanganya na kuwashawishi watu wasiokoke - eti kuokoka ni ujinga! Ujinga?! Shetani anajua, watu wakiokoka wataishi maisha yenye heri hapa duniani na mbinguni. Kataa uongo wa shetani, kwa Jina la Yesu.

Ukweli ndio huo, mimi nimeokoka. Hivyo ukiniwekea sumu kwenye chakula changu ili nife, utasubiri sana! 🙂
Ww mtoto mdogo yako nepi
 
Hivi kuoka maana yake nini ukiwa bado unaishi kwenye hii dunia iliyojaa laana kwakweli hii maana ya kuokoka huwa inanitatiza sana hivi unawezaje kujiakikishia kuwa umeokoka.

sisi ni raia wa mbinguni tunaishi duniani kwa muda mfupi.

sisi sio wa ulimwengu huu. Ndio maana inabidi tulindwe na Mungu Baba kwa sababu tu tu wageni na wapitaji.

Yohana 17 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁵ Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
¹⁶ Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.


Tunalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya Imani, 1Pet 1:3. Imani iliyo katika Kristo Yesu Bwana wetu.


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Hivi kuokoka maana yake nini ukiwa bado unaishi kwenye hii dunia iliyojaa laana kwakweli hii maana ya kuokoka huwa inanitatiza sana hivi unawezaje kujiakikishia kuwa umeokoka.
 
Watanzania tupo nyuma yake

Hakuna mtu mzito km mzalendo hao wewe unazungumzia mzito fisadi labda
 
Ndugu yangu, kumbuka kila wakati, katika dunia hii sio wote wanaofurahia mafanikio yako ya kimaisha, ya kikazi au ya kibiashara. Kwa sababu hiyo yamkini kuna watu wanapanga mbinu za kukuangamiza. Na wengine wanaweza kukuchukia tu hata kama huna pesa au cheo, wakatafuta njia ya kukuondoa duniani.

Njia inayotumiwa na waovu kukatisha maisha ya watu kimya kimya ni kuweka sumu kwenye chakula au kinywaji. Unaponaje sasa katika hali hii? Utakuwa unatembea na daktari wa kupima maji na chakula chako kabla hujala? Na je, daktari akipitiwa akasema chakula hakina sumu kumbe sumu ipo, utaponaje?

Nakupa siri ya ushindi! Ukiokoka, ukawekewa sumu kwenye chakula – sumu hiyo haitakudhuru kabisa.
Marko 16:17-18
Na ishara hizi zitafuatana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.

Hiyo ndiyo sababu kwanini siwezi kufa ukiniwekea sumu kwenye chakula.
Kuokoka ni jambo lenye faida sana. Ndio maana shetani anatumia mbinu nyingi kuwadanganya na kuwashawishi watu wasiokoke - eti kuokoka ni ujinga! Ujinga?! Shetani anajua, watu wakiokoka wataishi maisha yenye heri hapa duniani na mbinguni. Kataa uongo wa shetani, kwa Jina la Yesu.

Ukweli ndio huo, mimi nimeokoka. Hivyo ukiniwekea sumu kwenye chakula changu ili nife, utasubiri sana! 🙂
Imeandikwa " Usimjaribu Bwana Mungu wako". Utakuja kufa kama mende wewe, sumu siyo jambo la utani. Siyo kula tu! hata kulamba tu usijaribu utakuja kuwa marehemu katika muda usioutegemea.
 
Mkuu,
hivi unaifahamu POLONIUM 238?
Kama unaishangaa Polonium, basi hujaisikia Botox(Botulinum Toxin)
Hiyo sumu, Lethal Dose: ~1–2 nanograms per kg (theoretically, a few grams could kill every human on Earth).

Lakini majina ya sumu zote hizo yako chini ya Jina la Yesu

Wafilipi 2:9-11

Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana[Yesu], na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri kwamba Yesu ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba Mwenyezi.
 
mental health patients
This is strange! How come mental health patients are pulling you in until you open their posts and comment? Isije ikawa wewe ndo akili zako zimetiwa giza kama Maandiko yanenavyo:
2 Wakorintho 4:4
Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu.
 
Unacheza wewe, unazijua sumu na mode of action zake? Yani hivyo vijistari vya kukariri vizuie botulinum toxin, arsenic, cyanide, strychnine nk kufanya kazi yake? Hizi imani zingine ni ugonjwa tu wa kufisha
 
Umeandika as if walokole hawatakiwi kufa. Kifo kipo tuu ... uwe tayari kufa kwa njia yoyote kama muda umefika hiyo sumu itakuua tu. Mtu aliyeokoka wala hawazi issue ya kifo maana ni njia ya kwenda mapumzikoni. Okoka upya
kweli tupu!!!👿 " mtu aliyeokoka hawazi kufa..."
 
Back
Top Bottom