Ukizaa na mume wa mtu, jukumu la kulea mtoto ni lako mwenyewe!

Umeongea Ukweli mtupu Taikon ,hakika hukoseagi kwenye maandiko Ungekuwa Le Mutuz ningesema Mzee wa Facts hakuna kupindisha maneno kitu black and white.
 
Ni wanaume wangapi humu ikitokea kapata mtoto nje ya ndoa atamwambia huyo mwanamke JUKUMU LA KULEA HUYO MTOTO NI LAKO? Yaani utamtelekeza mwanao?
mwnyw nmeshangaa aisee,
Michango ya hivi inastahili kutolewa na wavulana wanaobalehe,

Huwez kua mwanaume unaejitambua unajisifia kutelekeza damu yako, no matter what happened.
 
Someni TAARIFA YA SERIKALI NA. 134 ya tarehe 09/05/2014 TAFSIRI YA SHERIA YA MTOTO [SURA YA 13] TOLEO LA MWAKA, 2014, Sehemu ya 10. Inahusu haki ya mtoto kupata mali.
 
Punguza ujuaji dogo unapomwagia ndani unategemea nini? tunza damu yako
 
Huyu dogo ni mpumbavu sana nisha wahi kumushauri sio kila kitu lazima aandike , imagine mtu mzima una ndoa yako unaenda kulala na binti vichochoroni huko baadae unamwachia mwenzako mzigo , ni mpumbavu tu anae weza kula , kulala bila kuwaza damu yake inateseka mahali flani
 
Mbona sasa kwa huu uandishi wako unaonekana wewe uliye na experience na maisha hakuna unalolijua kuhusu maisha yenyewe.

Mleta uzi kasema wazi kuwa wanawake muwakalie mbali wanaume waliopo katika ndoa yaani wasijihusishe na wanaume za watu kimapenzi waishie salamu tu baasi.

Sasa wewe unakuja kumponda kuwa hayupo sahihi, haya sasa wewe uliye sahihi hebu tuambie vema unampango gani na watoto wa watu wa kike?!

Je unawasapoti wazae na wanaume za watu na kama hausapoti mbona umekuja kumkataza mleta uzi asikemee uovu wa kuzaa na wanaume za watu.
 
Wewe hufai kuwa mwanaume chagua jinsia tofauti,uanaume ni majukumu
 
Sahii kabisa,
Sio ujanja kutelekeza damu yako
Mwanaume lazima uwajibike kwa starehe zako
 
Wewe ndio sufuri kabisa. Watoto wengi wa kike wanaingizwa mkenge kwa kudanganywa kuwa mwanaume aliezaa nae hana mke wengi wanakuja kujua badae.

Halafu hizi ndoa zina mambo mengi wengi wanaenda nje kutafuta faraja matokeo yake mwansume anapenda kweli mchepuko mpka anaamua kuzaa nae. Kwanini usitunze damu yako?
 
Tafsiri yake ukiwachepuko pambana mume wa mtu akumegee chako mapema
Nimesema huo kama mfano tu, wa kuwa mara nyingi wanawake tunakuwa wahanga kwa kujitakia. Unatoka na mume wa mtu na unajua. Anakuletea hela analala kwako unaona kama vile hampendi mke wake
unajiachia unabeba mimba kwa akili zako timamu halafu leo hii uende kwa mke mkubwa udai urithi inaingia akilini.Basi wawe wanajiongeza waombe mitaji wafanye japo biashara ili walee hao watoto . Lkn hakuna wanataka hela za mtelezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalenda ya uzazi Mungu kaiweka kwa mwanamke. Hivyo anapaswa kujijua na kuchukua tahadhari kuepuka mimba zisizo tarajiwa.

Utamlaani Mwanaume kukutelekeza lakini itakuwa kama dua la kuku lisilompata mwewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…