Ukraine waamua kuachia mji wa Severodonetsk baada ya kichapo kikali

Vikosi vya Ukraine vilivyoko Severodonetsk vimetakiwa kuondoka, kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa eneo hilo.

Mji huo ndio kitovu cha uvamizi wa Urusi huku Moscow ikijaribu kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.

"Kusalia katika nafasi ambazo zimeshambuliwa kwa miezi mingi haina maana," gavana wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai alisema.

Vikosi vya Urusi vimepiga hatua katika siku za hivi karibuni na vinakaribia kuzunguka jiji hilo, na mji wake pacha wa Lysychansk.

"Wamepokea maagizo ya kurejea kwenye nafasi mpya... na kutoka huko waendelee na shughuli zao," Bw Haidai aliambia televisheni ya Ukraine.

"Hakuna maana ya kukaa katika nafasi ambazo zimeharibiwa kwa miezi kadhaa kwa sababu ya kubaki," alisema.

Miundombinu yote ya jiji imeharibiwa kabisa, Bw Haidai aliongeza, na zaidi ya 90% ya nyumba zikiwa zimepigwa makombora na 80% kuharibiwa vibaya.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ulioanza mnamo Februari, umekuwa ukilenga Severodonetsk na mji wake pacha wa Lysychansk kwa wiki kadhaa.

Ni nafasi za mwisho zilizosalia za Kiukreni katika eneo la Luhansk, moja ya mikoa miwili inayounda Donbas ya mashariki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amedai kwa uwongo kwamba wazungumzaji wa Kirusi katika Donbas wamekuwa wahanga wa mauaji ya halaiki - mojawapo ya sababu kuu anazotumia kuivamia Ukraine.

Siku ya Alhamisi, vikosi vya Urusi vilichukua udhibiti wa maeneo zaidi kusini mwa Severodonetsk na Lysychansk, na kuzua hofu kwamba vikosi vya Ukraine vitazingirwa huko hivi karibuni
Habari kama hizi zinanogesha sana usiku wangu😃😃😃
 
Ndo ile basi tu hata NATO wanajua, hata Zelensky kwa Sasa ashajua Kwamba kuipiga Russia Ni swala gumu. Vita washashindwa.
Marekani ameahidi kuwapa mifumo mizito ya kurusha makombora masafa matefu Minne (4) Aina ya HIMMARS. Cha ajabu Russia inayo mifumo ya mfano huu kwa maelfu . Eti leo Ukraine inajitapa itaitumia mifumo hiyo kuitoa Russia katika occupied regions za Ukraine. Hi ni aibu na home kubwa
 
Urusi sasa kutwaa miji magofu isiyo na shughuli zozote za kiuchumi sababu kabomoa miundombinu, mashule, mahospitali, makazi ya watu, kalipua reli, viwanja vya ndege nk

Hajateka mji kateka magofu kuteka mji unakuwa na watu, viwanda na shughuli za kiuchumi zikiendelea

Mrusi anateka dead cities
Cry [emoji22][emoji22]

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Kinachotekwa ni ARDHI; vilivyo juu yake kama majengo na miundombinu, vitajengwa Kama vilivyokuwa vimejengwa awali hata na kuzidi.
Raslimali iliyoko chini ya ardhi, kama madini na gesi, vitabaki kuwa chini ya aliyeiteka.
GO Vladmir Putin; PUT THEM IN.
[emoji123][emoji123][emoji123][emoji419][emoji28][emoji28]
 
Hiyo mikoa imemchukua miez miwili sasa kuimiliki chini ya vikosi hafifu vya Ukraine ,alafu pia mikoa hiyo iliyo ndani ya donbas ni magofu tupu hakuna watu ,Ukraine wameona ngoja wakajipange ,mbona kawaida tuu kwani Russia si walikimbia pia hapo mwanzo,mwez ujao utasikia Ukraine kakomboa tena
Cry [emoji22][emoji22]

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mrusi anavutwa tu na NATO...Putin anajua hawawezi NATO hata kidogo..lakini labda wanatafuta njia nzuri la kumuangusha..maana wakitumia mabomu ya masafa marefu,,wanajua yule kichaa anaweza kufyatua ata nuklia kwa panic...Naona upande wa vikwazo vya kiuchumi kama wamemshindwa..ila kwa mahaba yangu pUtin atachapika
Akili huna [emoji706][emoji706]
 
NATO wanaweza kumchapa Putin vizuri nayeye analijua hilo...ila je wataweza ku handle consequences za kumi attack russia kijeshi ikiwa ana nyuklia na huku akijua vita ya kawaida hawawezi..!?? Nafikiri NATO they have plan..ila sio kukurupuka na mihemko kumtwanga urudi..ndio maana ata mabobu wanayopewa Ukraine sio ya masafa marefu ya kufika urusi..kama urusi atakua arrogant na kuendelea kushambulia nchi mwanachama wa NATO..hapo ndipo Putin atakapovalishwa kijora.

Ikiwa vita ya tatu ya dunia..basi wahuni tutubu na kumrudia Mungu wetu Ili vile vikombe vya mvinyo vya ghadhabu ya bwana visitushukie...maana dhiki kuu itakuja
Narudia tena akili hauna [emoji706][emoji706]
 
Mijitu mingine bwana , yaani mmekaa kabisa mnaikebehi Russia, hivi mna akili kweli

Yaani mnashindwa kutambua nguvu ya Russia katika zama hizi kuwa sio nchi inayo paswa kubezwa hata kidogo bali ni taifa linalo paswa kuogopwa sana

Imagine taifa linapigana vita huku likiwa limewekewa vikwazo lukuki lakini Bado linatoa kichapo katika uwanja wa vita kama vile hakuna kikwazo chochote kile walicho wekewa bad Enough vita wanayo pigana wanae pigana nae ana pewa support ya silaha na Mataifa 28s lakini Bado Wana chapika .. still mnashindwa kutumia logic nakuiona Russia kuwa ni lidubwana la kuogopa badala yake mnaendelea kuibeza !? .. aiseee kweli Kuna watu akili hamna [emoji706][emoji706]
 
Sperm yenye speed ikijaribu kutoa maoni kwa mihemko na hasira
 
Vikosi vya Ukraine vilivyoko Severodonetsk vimetakiwa kuondoka, kwa mujibu wa afisa wa ngazi ya juu wa eneo hilo.

Mji huo ndio kitovu cha uvamizi wa Urusi huku Moscow ikijaribu kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.

"Kusalia katika nafasi ambazo zimeshambuliwa kwa miezi mingi haina maana," gavana wa mkoa wa Luhansk Serhiy Haidai alisema.

Vikosi vya Urusi vimepiga hatua katika siku za hivi karibuni na vinakaribia kuzunguka jiji hilo, na mji wake pacha wa Lysychansk.

"Wamepokea maagizo ya kurejea kwenye nafasi mpya... na kutoka huko waendelee na shughuli zao," Bw Haidai aliambia televisheni ya Ukraine.

"Hakuna maana ya kukaa katika nafasi ambazo zimeharibiwa kwa miezi kadhaa kwa sababu ya kubaki," alisema.

Miundombinu yote ya jiji imeharibiwa kabisa, Bw Haidai aliongeza, na zaidi ya 90% ya nyumba zikiwa zimepigwa makombora na 80% kuharibiwa vibaya.

Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ulioanza mnamo Februari, umekuwa ukilenga Severodonetsk na mji wake pacha wa Lysychansk kwa wiki kadhaa.

Ni nafasi za mwisho zilizosalia za Kiukreni katika eneo la Luhansk, moja ya mikoa miwili inayounda Donbas ya mashariki.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amedai kwa uwongo kwamba wazungumzaji wa Kirusi katika Donbas wamekuwa wahanga wa mauaji ya halaiki - mojawapo ya sababu kuu anazotumia kuivamia Ukraine.

Siku ya Alhamisi, vikosi vya Urusi vilichukua udhibiti wa maeneo zaidi kusini mwa Severodonetsk na Lysychansk, na kuzua hofu kwamba vikosi vya Ukraine vitazingirwa huko hivi karibuni
Muda utasema Kama wataamua ku retaliate au laa,maana Kama wameweza kuokoa maeneo mengine km Kharkiv,lviv n.k sidhanikm watauachia mji wa Sieverodonesk.
 
Back
Top Bottom