Sean Paul
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 1,330
- 3,289
Wewe dogo unajifanya mjuaji sana wa haya mambo wakati ukweli huujui. Na unapenda ligi za kidini ukitetea ukristo wako wakati huna elimu and so unakosa moral authority to establish this type of discussions.Labda hii watu hawajui. Leo si tunazungumzia dini zetu, let's go.
Kuna tofauti ya watu walioandikwa kwenye Biblia na Koran, hilo kwanza ulijue. Ibrahim unayemsoma kwenye Biblia si Ibrahim unayemsoma kwenye Koran.
Ibrahim wa kwenye Biblia baba yake anaitwa Terah ila wa kwenye Koran anaitwa Azar. Kasome Quran 6:74.
Kwenye Biblia wana Yesu, kwenye Koran wana Issa. Huyu Issa hakusulubiwa msalabani, ila Yesu alisulubiwa. Ndugu zangu, hawa ni watu wawili tofauti.
Kuna MUNGU (Almighty GOD) kwenye Biblia na kuna Allah kwenye Koran
So watu wa huku ni tofauti na wa kule. Kwa Biblia, Ishmael anajulikana kama mtoto wa kijakazi, ila kwa Kuran ni tofauti.
So mkikaa na kuzungumza, cha kwanza jueni mnawazungumzia watu wa sehemu tofautitifauti.
Mfalme Suleiman wa Bible alikuwa holy na baadaye akaanguka dhambini ila wa kwenye Kuran alikuwa anaongea mpaka na majini. So mkiwa mnawasoma watu wa kwenye Bible, msije kufikiri ni watu walewale wa kwenye Kuran, sio hivyo.
Musa wa kwenye Biblia alipewa Amri 10 za MUNGU, Musa wa kwenye Koran hakupewa amri 10 zozote.
Biblia inamtambua Samson kama jamaa aliyebarikiwa nguvu na uwezo wa kupambana na udhaifu wake ni kukata nywele zake, ila hakuna kisa cha namna hiyo kwenye Quran.
Biblia imeorodhesha mitume na manabii wengi wakitoka katika chimbuko la wayahudi, wakati Quran haiwazungumzii wayahudi katika chimbuko la unabii.
Ndio maana ukimsoma mtu wa huku, unaona tofauti kubwa na mtu wa kule.
Kuran imemtambua Adam kama mtume, ila kwa Biblia imemtambua kama mtu wa kawaida tu, mtu aliyeumbwa mwanzoni kabisa.
So mlifahamu hilo, sio mnakaa kwenye vijiwe vya kahawa mnabishana weeee meaningwhile watu mnaowazungumzia ni tofauti.
Historia ya Matukio ikitofautiana basi jua kabisa hao ni watu tofauti kabisa.
Hivyo ni vyema kila mtu abaki na anachokiamini, muda au siku ya kiama ndio ukweli utadhihirika nani alikuwa sahihi na nani alikuwa muongo.
Naomba nikujibu point yako ya kwanza ya Ibrahim.
Kiarabu kina wenyewe sio mnatafsiri mnavyotaka nyinyi. Hiyo aya ya Surat An'aam (6:74) Quran imetumia neno Abi kudenote baba (kama ambavyo wewe umetafsiri)......lakini katika ufasaha wa lugha, Abi haitumiki tu kudenote baba mzazi. Hata baba mdogo/mkubwa inatumika pia yaani uncles au mababu zako waliotangulia (ancestors). Nitakupa ushahidi juu ya hili:-
1. Ukisoma Quran 2:133 wakati Yaqub (Jacob) umemjia umauti akawauliza wanawe watamwabudu nani baada ya kufa kwake? Wakamjibu tutamwabudu Mungu wa baba zako Ibrahim, Ismael na Isihaka. Hapa Ismael naye kaitwa Abi wakati si baba yake mzazi.
2. Kwanza baba yake Ibrahim hakuwa mwabudu sanamu. Ukisoma Quran 14:41 Ibra anaomba yeye na baba yake na waumini wengine waingizwe peponi. So hii ni evidence aliyetajwa pale 6:74 si baba yake mzazi.
Baba yake Ibrahim kwa mujibu wa Uislam anaitwa Tarah, kasome kitabu cha Ibn Katheer, kinaitwa Al bidaya wa Nahaya volume 1 page 139.
Pia nenda usome Tafsiri ya Quran ya Tabari by Ibn Jarir volume 7 page 158 na Historia ya Tabari volume 1 pg 119.
Dogo, ukija huku ujipange sio unakurupuka kama mlevi wa wanzuki. Hivi hujiulizi, yaani makosa uje kiyaona wewe leo wa karne hii ya dot com, huko nyuma hakukuwa na watu wanatafakari mambo haya? Hawakupata majibu?
Ni bora uulize kuliko kuconclude usichokijua.
WHEN YOU ARE NOT SURE, GUESS POSITIVELY.
Sean.