Ndio inawezekana kuwepo watu wawili tofauti kabisa wenye jina linalofanana... Kitu kinachofanya watu hawa wawili kusemekana kuwa ni mtu mmoja ni kufanana kwa matukio au historia yao... Ila wasipofanana tu matukio basi hao sio mtu mmoja... Mfano Yesu na Issa ni watu wawili tofauti kabisa kwa sababu historia zao hazifanani.
Hujasoma Maelezo yangu ukayaelewa? kayasome..
Kuna Mtu anayeitwa Petro..
Unajua Kuwa Petro,Peter halikuwa Jina lake na wala hakuwahi kuitwa Hivyo???
jina lake Halisi lilikuwa ni Simon ila Yesu alimuita Mwamba kwa Kiaram " cephas"
Mpaka wanakufa hicho kizazi hakukuwa na Mtu anayeitwa Petro mwanafunzi wa Yeshua..
Kwa mujibu wa Biblia baba yake na Yusuph mke wa Maria ni nani??
Kwa Mujibu wa Biblia Baba yake na Mke wa Musa ni nani?
tuanze na hayo kwanza mengine yatafuata
Yesu ni tafsiri tu ya kiswahili
Jina "Yesu" ni tafsiri ya Kiswahili ya jina la Kigiriki "Ἰησοῦς" (Iēsous), ambalo lenyewe ni tafsiri ya jina la Kiebrania "ישוע" (Yeshua) au "יְהוֹשֻׁעַ" (Yehoshua), linalomaanisha "Yahweh anaokoa" au "Yahweh ndiye wokovu."
Kama ilivyo kwa majina mengine ya kiebrania yaliyotafsiriwa kuja kiswahili kama Yohana, Musa, Petro na mengineyo. Kitu pekee kinachofanya jina hilo kudhiriisha huyo mtu ni mfanano wa historia na matukio yao
mkuu Tangu umezaliwa Umewahi kuona Jina la Mtu linatafsiriwa..
Kwa mfano hapo unaitwa Mhaya ukienda kongo utaitwa Nani???
vipi ukienda China??
Jina halina Tafsiri..
na hapo ndo walipo tuweza..
huwezk kushangaa Jina la Yakobo lina tafsiri Mbili tofauti
kuna Yakobo wa Jacob na Kuna Yakobo wa James Bado hushangai?
Jina linaloandikwa kwa Kiebrania kwa Maandishi sawa Ila tafsiri Tofauti...
Kama Yeshua ina tafsiri Kwanini Jina la yoshua Bin Nun hakuitea Yesu Bin Nuni?
Hajiri kipindi anaolewa alikuwa bado kijakazi, na hata hakupata haki zote kama mke. Hata mtoto wake hakufanywa mwana mkuu machoni pa Ibrahim badala yake Mke wake Sarah baada ya kuzaa ndio isaka akafanywa mtoto mkuu machoni pa baba.
mkuu Jitahidi Kusoma sana
Maana nilipokuandikia mwanzo ulielewa?
Kipindi cha zamani Mtumwa aliachiwa baada ya kukaa miaka kumi kwa bwana wake..
Ila Hajar alipotimiza miaka Kumi sarai hakuona haja ya kumuachia akaamua kumuozesha mumewe awe mke wa Ibrahimu..
Nimekupa Andiko la biblia Mkuu kasome maana zamani Ukikaa na mtumwa "Kijakazi" utaruhusiwa kukaa naye miaka saba tu, Baada ya hapo utamuachia..
Kama hutataka kumuachia Bhasi Muoe..
Na ndo kilichofanyika..
Kutoka 21:2
"Ukimnunua mtumwa, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure."
Sasa Turudi kwa hajari alitumika miaka mingapi Ilkuwa Kumi maana yake ni kwamba alikuwa Huru na ndo maana akaweza kuruhusiwa kuolewa na Ibrahimu ambaye ni bwana wake..
Mwanzo 16:3
"Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe."
Nafikiri Sasa Umeelewa.