Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Soko la uhakika ni la ndani tu
 

Kwa hiyo kahawa, mahindi, mpunga na viazi ni mazao ya chakula, sio mazao ya biashara, yani hayauziki!

Na parachichi ni zao la biashara, sio zao la chakula, kwa hiyo parachichi haliliki!

Unajua wale walimu wa primary wale walitukaririsha madudu mengi vichwani, tulikuwa hatujielewi na wao hawajielewi masikini ya Mungu!
 
Parachichi unazolima ni hizi za biashara?? mfano; Hass avocados, Fuerte avocados Au ni nyingine..maana hizo ni rahisi kufanya biashara maana zinaenda nje japo kuna parameters zake zinahitaji ufuatiliaji wa umakini.
Ila kama unalima parachichi kwa kulenga soko la hapa hapa ndani aiseeh ni hasara.
Hizo za biashara ulime kiutaalamu ukifuata international standards na kuzikatikia certificates kabisa kama GlobalGap certifices e.t.c mbona makampuni yatakufata menyew.
 
Mkuu unaweza ni connect na mkulima wa machungwa wa aina hiyo ya valencia?
 
Mkuu safi sana umezungumza vizur sana..hii biashara ya mazao unaijua vizur na nimfatiliaji.
 
Kilimo kina wenyewe. Ukitaka kufanikiwa kwenye Kilimo basi fanya partnership na mkulima mzoefu wewe ongeza mtaji wa mbolea kukodi mashamba zaidi na pembejeo kwa ujumla.wake alafu huyo mtaalamu mzoefu mwache aendeshe shamba hapo ndio utaona utamu wa kilimo, ila hiki kilimo chenu cha kupost picha whatsapp na twitter sehemu kubwa ni uongo uongo tu wa kwenye picha kwa groung ni different story.
 
Mkuu nilijiuliza hilo swali kwamba lazima parachichi zizae kwa pamoja mbona viumbe vingine vinazaliwa siku moja ila vina mature tofauti. Naomba hoo elimu ya kuzifundisha zizae mda naotaka.
Zangu ndio zipo hatua ya maua ya pili.
Nalimia njombe ba huku changamoto kubwa ni barafu na jua.
Je ukikomaa na soko la ndani tu je hailipi kweli kama wadau wanavyosema?
Mwaka huu nina project ya heka 20 na watu wana toa tahadhari nami siwezi puuza.
 
According to code of conduct from college desa, it state that " teach the syllabus, don't teach your ideas!".
Walaumu wakuza mitaala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…