Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Mkuu,siamini kama ni kweli, labda uwe ulifanya kosa moja,la kuanzisha biashara bila soko.
Au vinginevyo,uwe na uelewa mdogo kuhusu masoko.
Kuna mdau mmoja kasema hutompata mtu atakaekushirikisha mafanikio. Soko likiwepo anataka akupige akulize,na usijue soko.
Kama wewe mwenyewe unaweza, au una watu,jaribu kutafuta connection kwenye makampuni yanayouza nchi za nje. Napojua ni Dubai(kwa mjibu wa watu wa nchi jirani wanaopeleka palachichi na viazi mvilingo huko).
Tatizo kubwa,palachichi nchini humu ni nyingi na watumiaji ni wengi.
Kama umelima una shamba,fatilia. Zamani walikuwa wakisafirisha kwa ndege,ila kwa sasa wanatumia meri. Na hakika ni bandari ya Dar. Kama unaweza pata mzigo wa uhakika si tani moja,mbiki tatu, unawauzia wenye export certificates na masoko yao,kikubwa tu ukidhi vigezo.
 
Ni kwamba watu wapo kwenye ukoloni wa kitapeli. Watu wana dili zao,uishi,ufe,haiwahusu.
Unadhani wenye kutoa vibali hizo changamoto hawazijui? Nani akwambie?
Hata kwa mkopo,viwanda vya huko zinatumiwa kufanyia nini? Umeuza kwa hasara,lakini ikishageuzwa kitu kingine inakuja huku inauzwa bei mbaya. Hivyo viwanda vikijengwa huku,wakulima si watakuwa na soko la uhakika?
Huku mafuta ya nazi,utakuta hayana bei,na hayahitajiki kivile. Lakini acha yawekwe kwenye chupa af, yaandikwe kuwa yanatibu nini na nini,na bei yake uone.
 
Bodi ya Mazao Mchanganyiko huijui?
 
Walituambia Green Gold. Alimanusura nilime. Kuna zao moja hilo hubahatishi
 
Issue hapa sio parachichi
Miti inatakiwa kwa ajili ya kuboresha hewa....
Ujinga badala tuendeleze ya mbao ambayo ni hela...
Tunapanda matunda pumbu
 
Mashamba yapo kwa sh? Heka moja.
Parachichi hazivumnwi nna kupakiwa kwenye Fuso hapo tu tayari walishapata hasara huwa kuna tray za kuwekea
 
Jipe moyo tu mzee baba ila nikwambie ukweli tu kwamba kilimo cha kibongo walanguzi na madalali ndio wanaopiga hela ๐Ÿ˜‚
 
Parachichi ni zao ambalo halitupwi. Cozi likioza unatengeza mafuta, takataka zake unatengeza mbolea. Mbegu yake unatengeza unga. Hao waliotupa walizingua
 
Nililima heka 50 hizo Hass Ovacado mafinga nilipoangalia gharama msimu wa kwanza nikajikuta nimepata mil 14 ndg zangu hela niliyokua nimeweka pale nilitamani kulia mchozi...ovacado ni shida kubwa sana bora ulime mihogo
Hilo nimeligundua mapema sana, kuna mtu alinishawishi nikanunua heka 3 njombe hapo๐Ÿ˜‚ hesabu kwa alizompigia mama watoto kwamba baada ya kuvuna mche mmoja unaweza pata hadi laki 7 nikaona biashara sindio hii sasa.

Nimefyeka miti na kusafisha shamba nikapanda heka 2 kwanza. Siku naenda kuangalia hilo shamba na mazao. Nakuta almost 10% ya miche imekufa ๐Ÿ˜‚ sababu wanasema sijui mvua zilipiga madini yakawa washed away ba blaah blaah kwahio nirudishie tena 10% ya hio miche.

Nikiangalia gharama nilizotumia ndani ya miezi michache hadi kufikia hapo dah nikaona kabisa upkeeping cost za shamba na kile kilichotarajiwa after 3 years ni mbingu na ardhi.

Nimeamua niachane nalo tu hilo shamba. Hamna namna ntaendelea kupoteza hela kule๐Ÿ˜‚
 
Wewe ni motivational speaker. Unafanya jambo sasa bila kuwa na strategy, unasubiri baadae ndo ujue utafanya nn
 
Hio miaka 7-10 aliyelima mahindi yuko wapi?!
 
mi nimeuza heka zangu 3 baada ya kuona maji yatazidi unga in 3 years๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Kwenye nyanya hapo mi ni shuhuda,nilinunia nyanya ikakaa siku 28 bila kuharibika, na haipo kwenye fridge
Hio nyanya inasinyaa tu ila haiharibiki ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Mkuu umeandika ukweli mtupu, Tatizo la hapa Tanzania wanasiasa wanadanganya sana wananchi
Wengi wa hao waongo ndio madalali
1. Atakutafutia shamba
2. Atakutafutia vibarua
3. Atakutafutia trekta na majembe
4. Atakutafutia mbegu
5. Atakutafutia dawa na mabomba
6. Atakutafutia wavunaji
7. Atakutafutia walinzi
8. Ataongea na watendaji โ€˜wakulindeโ€™
9. Kisha atauza yeye, atakupa kipande kidogo tuncha income
10. Ma kila step hapo juu anakua anapiga kidogo kidogo

Ogopa uwekezaji na Wana siasa na watu wenye nafasi za kidalali
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
Kilimo kwa hapa Tanzania ni U.T.I ya mgongo, (siyo uti wa mgongo.).
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
Duh tutafika kweli.?
Au ndo tutafika tukiwa tumechoka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ