Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Usipoteze muda kubishana na mjinga. Kiimani unatakiwa kumwombea.
Paulo aliyekuwa kiongozi mkuu wa kulihujumu Kanisa la Kristo alikuja kuwa mtume wa Kristo aliyefanya kazi kubwa sana. Hata huyo unayemsema, usishangae siku nyingine akasimama mbele yako akikuhubira mafundishobya kweli kuliko hayo ya upotofu anayoyatoa sasa.
Ila kama wewe unayumba kwa sababu ya kutolijua neno la Mungu, jibidishe kuyajua maandiko:
Kwa ufupi kabisa, rejea hapa:
1) kwa nini Kristo aliuawa?
JIBU: Kwa sababu ya kutotii sheria.
2) Sheria gani
JIBU: Sheria ya Musa, yaani kumbukumbu la torati.
3) Sheria gani ilikuwa kuu kuliko zote kwenye kumbukumbu la torati?
JIBU: Sheria ya sabato
Yesu kutozingatia mafundisho ya mafarisayo kuhusiana na sabato, ndiyo mwanzo wa chuki za mafarisayo na makuhani dhidi ya Kristo. Tena wakasema wazi kuwa, kama angekuwa mwana wa Mungu angeitii Sabato. Naye akawaambia wazi kuwa yeye ni mkuu kuliko sabato. Yeye ni bwana wa Sabato. Kwa nini uiabudu siku ya Sabato badala ya kumwabudu yeye aliye bwana wa Sabato?
Kwa hiyo Kristo aliuawa kwa kutoitii sheria. Kwa kutoitii sheria za kumbukumbu la torati, ambako sheria kuu ni utii wa sabato. Kwa sababu kutokutii sabato lisingekuwa kosa kubwa la kuhukumiwa kifo na Pilato kiongozi mwakilishi wa mfalme wa Roma, wakamtengenezea kesi ya kubumba ya uchochezi kuwa anawachochea watu wasilipe kodi kwa mfalme Kaizari wa Roma.
Paulo anasema wazi Kristo alihukumiwa kwa sababu ya kutoitii sheria, akayashinda mauti. Baada ya ushindi wa Kristo yaani kuyashinda mauti, sisi tulioshinda na kufufuka na Kristo, tukirudi kuitumikia sheria, basi kifo cha Kristo ni bure.
Mkristo hustahili kuiabudu sabato, au kuiabudu siku, mwabudu Bwana wa Sabato katika kweli na haki.