Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Tukitumia lunar calendar ambayo Waisraeli wa Zamani waliyoitumia Kwa ajili ya kuhesabu siku na mwezi na mwaka, utakuja kugundua Sabato waliyopumzika haikuwa Jumamosi, inabadilikq kutokana na mwandamo wa mwezi kwa kalenda iliyopo.
Kalenda hii ilianzishwa na Papa Gregory ndo wasabato wanaitumia kujustify kuwa Sabato ni Jumamosi na kutumia Maandiko ya Kardinal Gibbons ila ukweli upo kwenye lunar calendar.
Ukiniambia Wayahudi wa Sasa wanapumzika Jumamosi nitakuambia wale ni Ashkenazim , Kuna uwezekano mkubwa hawana asili ya Kiebrania .
Soma biblia Luka 23:50 na kuendelea, soma Kwa makini. Biblia inasema yesu alifufuka cku ya kwanza ya juma.
 
Hakukuwa na Kanisa Katoliki kabla ya kuzaliwa Yesu. Dini iliyokuwepo kabla ya Yesu ni hii ambayo sasa inaitwa Judaism, hii wakati huo ilitwa dini ya Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.
umeninukuu vibaya nimekwambia kabla na baada ya kuzaliwa kwa YESU ilikuwepo roma ya kipagani yaan roman empire ambayo ilitawala dunia nzima .....lkn saiv ipo ya roma kidini ambayo ilihusika na kuua wakristo mamilion na mamilion wasio na hatia ktk karne ya 16, 17 na 18....na hv punde romani hii hii ya kidini itatawala tena dunia....
 
Yesu ni paska yetu mpya. Anachukua nafasi ya mwanakondoo. Kwa kuchinjwa kwakwe amelipa once and for all. Tunasherekea paska mpya ya Yesu. Nyie endeleeni na ya wayahudi
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Moja wapo ya sifa ya dini ni Universality. Sasa dini Ipo kwa Wapare, wajita , wakerewe na wajaluo tuu , hiyo ni prima facie evidence kuwa Kuna tatizo. Wao waendelee kucheza maparedi Yao kwenye makanisa Yao na kuzishika amri za kale za kiyahudi ambazo kimsingi ni Mila zaidi zilizopo kwenye agano la kale ambazo Yesu alizi ove rule Haina shida lakini wasiumize kichwa kwa Imani isiyowahusu
 
Kwanini YESU ana makanisa mengi hivi? Imeshindikana kabisa kukawa na viongozi wa kuwaonganisha wakristo wakawa kitu kimoja? Wakimwabudu MUNGU mmoja katika njia moja halali?

Tunajifahamu binadamu tukiwa na kila kitu tunanyanyuka na kiburi hutuvaa na kuyatamani mamlaka. Mbinguni hali itakuwaje iwapo hapa duniani pasipo na kila kitu kuwa kitu kimoja haiwezekani?
 
Kuna wakati, nilipokuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha 6, ikiwa ni pamoja na masomo ya biblia, nilialikwa kwenye mkutano wa wasabato. Nilienda huko nikiwa sijui kuwa ningepewa nafasi ya kuongea.

Cha ajabu, nikawekwa kama mtu wa kujibu maswali waliyokuwa wakiyaelekeza kwa Kanisa Katoliki. Nilijibu, kwa kadiri Roho alivyoniongoza.

Wote wakawa kimya kabisa. Nilishangaa mwishowe kufuatwa na viongozi wao kuwa eti wananiomba nijiunge nao na kisha niwe mchungaji wa Kanisa lao. Nilishangaa sana, nikawauliza kuwa tangu mwanzo wamelituhumu Kanisa Katoliki kuwa limepotoka, inakuwaje tena mimi Mkatoliki naweza kuwa kiongozi wao? Hawakuwa na jibu.

Nilivyomaliza masomo yangu ya shahada ya pili, nilipofika Dar, nikaalikwa na jamaa mmoja, aliwahi kuwa mtu mkubwa kwenye ngazi ya kitaifa kwenye Serikali. Yeye ni muislam. Nikaitikia mwaliko, nikaenda. Kufika huko nikashangaa walikuwa wamejaa wasomi wa dini ya Kiislam. Pekee yangu nilitengewe kiti, huku wao wote wakiwa wameketi kwenye majamvi. Nikaanza kuulizwa mambo ya Ukristo. Sikuwa nimejipanga kwa hilo. Lakini kwa utulivu niliwajibu kadiri nilivyoweza, hata wakaishiwa swali lolote.

Nilitafakari sana kwa nini niliitwa mimi, lakini baadaye nilikuja kutambua kuwa kuna ndugu zangu, nao walikuwa wasomi wazuri kwenye elimu ya Dunia, lakini hawakuwa vizuri sana kwenye mafundisho ya kiimani. Na kuna watu walitaka kuwabadilisha wale ndugu zangu kwenda uislam, na ikaelezwa kwamba kikwazo ilikuwa mimi. Hivyo wakinibadilisha mimi, basi wale wengine watanifuata.

Nashukuru mpaka leo wote tupo katika imani yetu.

Na neno la mwisho nililowaambia wale wasomi wa dini ya Kiislam ni kwamba sisi katika Ukristo tunaamini sana katika neema. Na neema hiyo inaweza kumwangukia yeyote, na ukashangaa aliyekuwa imamu au hata mpagani, siku nyingine anaweza kuja kuwa mkristo, tena kukuzidi hata wewe uliyedhania unaujua zaidi ukristo, akawa mwalimu wako.

Kwa hiyo usighadhabike Kanisa likinenewa vibaya. Kristo pamoja na ukuu wote, na mamlaka yote, alidhalilishwa, alitukanwa, alipigwa, alivuliwa nguo, alitemewa mate, hakuhangaika na waliomtendea hayo. Alipofufuka neno lake la kwanza lilikuwa Shalom, yaani muwe na amani, nimekamilisha, msiwe na mashaka. Mkristo unatakiwa kuyaiga maisha ya Kristo. Hatushindani katika kumjua au kumwabudu Mungu. Hata anayetusi, ujue Mungu ameruhusu, asipotaka, hawezi hata kuupanua mdomo wake.
Mkuu kuna member humu juzi alisema Mungu ni shetani.!!!?
 
Unadhani ni msabato.

Lakini siku hizi wachambuzi wa biblia ni wengi kama wachambuzi wa soka na wanatokea kwenye madhehebu na dini zote.

Btw dini zina wafuasi wengi kwasababu kuu mbili tu:
• hofu ya kifo,
• tumaini la uzima wa milele.

Ukishaweza ku cope na hayo mawili hutakuwa na shida.

Taasisi za kidini yaani madhehebu au makanisa ni oganaizesheni za kiuchumi na kijamii za wakati uliopita ambazo zimefanikiwa kudumu hadi leo kwa sababu ya kuwaogofya wanadamu kwa upande mmoja na kuwapa matumaini yasiyothibitika kupitia hali asilia ya binadamu tunayooita imani.

Jinsi ambavyo watu wanazidi kuerevuka ndivyo ambavyo hizi taasisi zitadhoofika na kupotea.

Dalili mojawapo ni huo mnyukano unaouona kati ya madhehebu za kikiristo kama wasabato dhidi ya wakatoliki,
wapentekoste dhidi ya waluteri , na pia mvutano kati ya dini kubwa hasa uislamu dhidi ya ukristo.

Dalili nyingine ni mfumuko wa madhehebu na dini zisizo na kichwa wala miguu zinazoashiria kuwa wengi sasa wanaelewa kuwa imani na ibada ni uchochoro tu wa kujitafutia mali!
 
Hata hao wasabato still hata hio jumamosi wanayoifata ni kalenda ya wakatoliki.
Hii kalenda ya SAsa ilianzishwa na Wakatoliki miaka elf 2 iliyopita hata kabla ya uwepo wa usabato duniani ambao ulianzishwa mwaka 1890 na Hellen G White na Mwenzake
The Seventh-day Adventist Church had its roots in the Millerite movement of the 1830s to the 1840s, during the period of the Second Great Awakening, and was officially founded in 1863. Prominent figures in the early church included Hiram Edson, Ellen G. White, her husband James Springer White, Joseph Bates, and J. N.

Kama Kanisa la SDA lilianzishwa 1863, na madhehebu yote mengine hawapo sahihi, tuamini kwamba kwa karibia miaka 2,000 kabla SDA halijaanza, wote walikuwa wanamwabudu shetani?

Na hao hapo juu walianzisha SDA baada kufukuzwa kutoka kwenye Kanisa la Wabaptist baada ya wakuu wa Kanisa kuona kulikuwa na mafundisho ya uwongo kuhusu mwisho wa Dunia. Waliwafundisha waumini wao kuwa mwisho wa Dunia ungekuwa 22 October, mwaka 1844.
 
The Seventh-day Adventist Church had its roots in the Millerite movement of the 1830s to the 1840s, during the period of the Second Great Awakening, and was officially founded in 1863. Prominent figures in the early church included Hiram Edson, Ellen G. White, her husband James Springer White, Joseph Bates, and J. N.

Kama Kanisa la SDA lilianzishwa 1863, na madhehebu yote mengine hawapo sahihi, tuamini kwamba kwa karibia miaka 2,000 kabla SDA halijaanza, wote walikuwa wanamwabudu shetani?

Na hao hapo juu walianzisha SDA baada kufukuzwa kutoka kwenye Kanisa la Wabaptist baada ya wakuu wa Kanisa kuona kulikuwa na mafundisho ya uwongo kuhusu mwisho wa Dunia. Waliwafundisha waumini wao kuwa mwisho wa Dunia ungekuwa 22 October, mwaka 1844.
Yesu ni MKUU kuliko sabato na yeye ndie Bwana wa sabato.
Amefufuka leo ndio chimbuko la Ukristo
 
Wakatoliki ndio walizipa majina hizi siku hazipo kwenye Biblia. Na ndizo hadi kesho utumiwa Dunia nzima kisiasa, kiuchumi na kijamii pia
Kuna namna waeza tupa ushahid juu ya hili? Pia kama ni hivyo inamaana sote tunaabud cku ambazo ni mapokeo ya wanadam? Kama ndivyo je kuna mweny haki wa kumwambia mwenzake sabato ni cku flan?
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
JE WAKATOLIKI TUNAABUDU MSALABA?
Kabla sijajibu swali la Msingi naomba nitoe utangulizi kidogo

Kwa hulka yake binadamu ni kiumbe ambaye ana tabia ya ku imagine karibu kila kitu ambacho anakiwaza au kukisikia na huwa anajaribu kutengeneza picha Fulani ya kitu hicho, kwa mfano mtu anaposikia jina la mtu Fulani ambaye hajawahi kumuona…… kwanza kabisa atatengeneza picha Fulani labda huyo jamaa ni mrefu, Mnene na kadhalika, na siku akimuona utamsikia akisema ‘aaaaa kumbe yupo hivi mimi nilifikiri yupo vile’

Hii ni hulka ya binadamu yeyote yule na hata kuhusu Mungu tunayehubiriwa na kwa kuwa hatujawahi kumona , nina hakika kila mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu yupo anapata picha Fulani ya Jinsi Mungu alivyo, na hiyo picha ni Tofauti kwa kila binadamu, picha hapa simaanishi uwezo wa Mungu kwa kuwa uwezo wa Mungu tunaweeza kuu feel ( hisi)kutokana na mambo ambayo anayatenda kwenye Maisha yetu ya kila siku.

Au pia mtu akisikia jina au habari za mji fulani kwa mfano SONGEA, kwa yule ambaye hajawahi kufika songea ni lazima atapata picha Fulani kichwani mwake, Kwmba ni Lazima kutakuwa na barabara za Vumbi kila sehemu, kuna wanaume weupe tu kama Mapunda N.K sasa siku akifika songea na kukuta kuna Rami barabara na mitaa yote ‘’ aaaaa Kumbe ndiyo kulivyo’Mimi nilifikiri papo vile.aaa kumbe kuna wanaume Weusi N.K

Sasa hizo picha zote kwa namna yoyote ile hazichukui Nafasi ya hivyo vitu kwa uhalisia wake, Miji, au watu husika, Ingawa zinawakilisha vitu hivyo kwa binadamu husika. Na hata picha za mnato kwa mfano hazichukui Nafasi ya mtu husika, kwani mtu husika anabaki kama alivyo na picha yake inabakia kama kiwakilishi tu cha muhusika.

Leo hii hatuwezi kuchukua picha ya mchazeji kama Fiston Mayele na kusema huyu ndiyo Mayele halisi.
SASA NAENDELEA NA SWALI NA MAJIBU YA MSINGI.
Jibu la Msingi ni HAPANA. Nitaeleza ni kwanini nasema wakatoliki hatuabuu sanamu, na labda tujiulize kwanza maswali yafuatayo ;
1.Je Mungu anachukia Kila sanamu ?
Jibu lake ni kwamba HAPANA, Mungu hachukii kila sanamu kwani hata yeye mwenyewe katika nafasi mbalimbali aliwahi kuagiza matumizi ya sanamu, nitakupeni mifano michache katika mingi, Katika agano la Kale tunaona kwamba Mungu alimuagiza Musa akatengeneze sanamu na kuziweka mahali ambapo Mungu atakuwa anazungumza naye na kumpa maagizo mbalimbali, tunasoma hilo katika kitabu cha kutoka 25 :10-22.

Pia kama mnakumbuka wakati wana waisrael walipokuwa Jangwani na baada ya kumnung ‘unikia Mungu,naye aliwaadhibu kwa kuwaletea nyoka wenye sumu waliwauma na watu wengi walikufa. Lakini baada ya Musa kuwaombea mshamaha kwa Mungu Naye Mungu alimuagiza atengeneze Nyoka wa shaba na kumtundika juu ya mti, na kila aliyeng’atwa na wale nyoka wenye sumu alipokwenda kumtazama yule nyoka wa shaba alipona baada ya kufanya hivyo( Hesabu 21 :4-9) sasa hapo tunaweza kujifunza kwamba aliyekuwa anaponya watu siyo ile Sanamu ya nyoka badala yake ni Mungu mwenyewe alikuwa anawaponya.

2.Je ni sanamu gani /zipi zinamchukiza Mungu
Mungu anachukia kila aina ya Sanamu ambayo inachukua nafasi yake, hapo namaanisha kila aina ya sanamu inayoabudiwa kama ndiyo Mungu mwenyewe , hiyo inamchukiza Mungu, Kwani Mungu yupo peke yake na kila kitu kinachochukua nafasi yake kuwa ndio Mungu anakichukia,kama mnakumbuka katika kitabu cha kutoka tunasoma kwamba wakati Musa alipokuwa mlimani sinai kupokea Amri za Mungu, alikaa huko kwa muda mrefu sana na waisrael imani ikawatoka, kiasi kwamba wakaamua kujitengenezea sanamu na kusema kwamba hiyo sanamu ya Ngo’mbe ndiyo Mungu wao aliyewatoa Misri na ndiye atakayewaongoza huko waendako.

Hivyo hii sanamu ni Lazima imchukize Mungu kwa kuwa inachukua nafasi ya Mungu, na siyo kwamba anawakilisha uwepo wa Mungu wa Kweli.Nenda kasome kitabu cha kutoka sur aya 32, isome yote.

3.Pia Mungu anakataza sanamu na kuziabudu na kuzitumikia, hapo ni sawa na kusema sanamu zimechukua nafasi ya Mungu. Hivyo sanamu zinakatazwa kama zinaabudiwa na kutukuzwa na kutumikiwa kama walivyofanya waisrael kama yule ndama, walimfanya kuwa ndiyo Mungu wao na walikuwa tayari kumuabudu na kumtumikia. Kwa kushindilia hoja hii soma kitabu cha kumbukumbu la Torati 4 :15 – 20)

4.Wakatoliki hatifanyi nini ?

Wakatoliki hatuabudu sanamu na kwa kuwa hakuna siku wala mahala ambapo tumewahi kufanya wala kusema hizi sanamu ndiyo Mungu wetu na kwamba tunaziabudu au tutaziabudu na kuzitii na kuzitumikia, hatujawahi kufanya hivyo na sidhani kama itatokea.

Tunaamini kwa Mungu Mmoja kama tunavyosali katika kanuni ya Imani yetu, na hakuna sanamu hata moja iliyowahi kupewa heshima kama hiyo.
NARUDIA TENA KWAMBA HATUFANYI KAMA WALIVYOFANYA WAISRAEL KULE JANGWANI KWA ILE SANAMU YA NDAMA.NDIYO KUSEMA HATUABUDU SANAMU.

5.Ijumaa kuu wakatoliki tunafanya nini ?
Katika Ibada ya ijumaa kuu kuna kipengele kinaitwa cha kuheshimu Msalaba.Mara nyingi huwa unatumika msamiati kuabudu msalaba.Lakini je kinachofanyika pale ni kitu gani hasa ? kwa mtu anayefuatilia vyema ibada hiyo atakumbuka kwamba kabla ya zoezi la kubusu msalaba halijaanza kiongozi wa ibada husema mara tatu maneno yafuatayo ‘’ HUU NI MTI WA MSALABA, AMBAO WOKOVU WA ULIMWENGU UMETUNDIKWA JUU YAKE’ na watu wote tunaitikia/ tunajibu ‘’ NJOONI, NJOONI, NJOOONI TUUABUDU’.
Sasa hapo kama kweli umeelewa tunachoabudu ninini ? mti wa msalaba au uokovu uliotundikwa juu yake ? Sasa wataalamu wa theologia wanatueleza kuwa tunaabudu wokovu juu ya msalaba, kwani kwa kufanya hivyo siyo kwa sababu ya ule msalaba, kwani kama kufa msalabani hata wakosaji wote katika jamii ya kiyahudi waliuawa kwa kutundikwa msalabani.

Hivyo basi tuna alikwa kuabudu wokovu uliotundikwa juu ya msalaba, na huo wokovu ninini basi ? Jibu ni YESU KRISTU na huyu Yesu Kristu ni nani ? katika katekisimu katoliki tunaambiwa kwamba Yesu Kristu ni Nafsi ya pili ya Mungu na ni Mungu sawa na Baba, hivyo kusema Yesu ni Mungu, na wokovu wetu ni Mungu ndiyo kusema TUNAMUABUDU MUNGU.

Na kwa wale ambao hawajawahi kuwa makini sehemu hii ya ibada ya ijumaa kuu nawaalika kuwa makini katika ibada ya mwaka huu na wale ambao wanasema kwamba ijumaa tunaabudu sanamu nao nawaalika wakafuatilie kipengele hiki vizuri. Ni hapo tu watapata majibu ya maswali yao na mashaka yao yatakwisha.

Na kuna wakati watani zetu huwa wanasema kwanini sisi wakatoliki tunaweka picha ya mtu katika misalaba yetu. Sisi huwa tunaweka picha ya Yesu katika misalaba yetu. Hao wanaouliza hivyo nao pia wanatumia misalaba lakini haina hiyo picha kwakuwa wanasema kwa kufanya hivyo watakuwa wanaabudu sanamu, lakini picha ya msalaba kwao siyo tatizo.

Hapo napenda kuwaeleza kwamba kuwa sisi wakatoliki tumeona kuwa na picha ya msalaba haitoshi kwani kitu muhimu ni kupata picha halisi ya Jinsi Yesu alivyokufa Msalabani, ndiyo maana tunaongeza na mtu pale msalabani.Kitu cha muhimu hapo ni msalaba wa Yesu na siyo tu msalaba PEKE YAKE .

Kwani msalaba ulioleta wokovu ni msalaba wa Yesu tu,kama suala lingekuwa ni msalaba tu kwani hata wale wanyanganyi waliuawa msalabani, na misalaba yao haikuleta wokovu kwa dunia.Ndiyo maana tunajazia na hiyo kitu ili kutoa picha halisi ya Yesu msalabani kusudi tunapoutazama msalaba wa Yesu tupate picha halisi ya kifo chake msalabani.

Bada ya kusema hayo basi naamini utakuwa ume imarika kiimani na hakuna mtu atakubabaisha juu ya hili suala la msalaba na masakramenti yote na tuwaeleweshe wale ambao hawaelewi kwa upendo na utulivu mantiki na liturujia nzima ya uwapo wa sanamu kwa wakatoliki
 
Huelewi chochote. Waulize wanaofahamu. Huelewi maana ya kuabudu.

Haya maneno huwa yanasemwa na baadhi ya wakristo waliokosa maarifa lakini huwezi kusikia kutoka kwa viongozi wenye elimu ya kutosha ya dini, hata kama siyo wakatoliki. Ila wale wakristo wa kusoma mstari mmoja wa biblia, bila hata kuelewa content, wanatoka na kuanza kupiga kelele kuwa Wakatoliki wanaabudu sanamu.

Wayahudu walipoitazama sanamu ya shaba walikuwa wanaiabudu?

Wayahudi walipokuwa wakisafiri na sanduku la amri za Mungu, walikuwa wanaliabudu?

Waisrael walipoyaweka makerubu kwenye hekalu lao walikuwa wanaabudu?

Wayahudi walipoibeba mifupa ya Yakobo, walikuwa wanaiabudu?
Nyinyi mnaabudu sanamu, hiyo ni dhambi na upagani
 
umeninukuu vibaya nimekwambia kabla na baada ya kuzaliwa kwa YESU ilikuwepo roma ya kipagani yaan roman empire ambayo ilitawala dunia nzima .....lkn saiv ipo ya roma kidini ambayo ilihusika na kuua wakristo mamilion na mamilion wasio na hatia ktk karne ya 16, 17 na 18....na hv punde romani hii hii ya kidini itatawala tena dunia....
Unaposema kutawala Dunia, una maana gani? Kushikilia vyombo vya dola na Serikali zote Duniani.

Mpaka sasa Kanisa Katoliki lipo mahali pote Duniani.

Catholic maana yake kitu kilichoenea Duniani kote. Pamoja na misukosuko mingi katika vipindi mbalimbali, ikiwa ninpamoja na kuwaua mitume wote (isipokuwa mtume Yohana aliyekufa kifo cha kawaida), Kanisa Katoliki lilizidi kuenea na linazidi kuenea.

Jana usiku, tumepokea wakristo wapya 7 toka familia za Kiislam, siyo kwa sababu ya kusimama barabarani na kuhubiri kwa kelele au kuutusi uislam, au kulitusi dhehebu lolote.

Wanaoutukana ukatoliki, waendelee lakini hawataleta athari yoyote. Yesu alimwambia Simon, 'wewe ni Petera (rock) na juu ya hiyo petera nitalijenga Kanisa langu, na wala milango ya jehanamu haitalishinda". Kama Kanisa Katoliki siyo la Kristo, kuna siku litapotea, lakini kama ni la Kristo, wazidi kutukana, lakini litazidi kustawi zaidi siku hadi siku hata kama kutakuwa masaibu ya namna gani.
 
Usidhani kanisa katoliki ni mapadre tu na maaskofu na masista.

Kanisa ni pamoja na wewe yaani kila aliyebatizwa na hivyo kila mmoja ana duty ya kulilinda kanisa.

Hivyo mjibu huyo muhubiri usisubiri askofu au padre.
Usipotoshe, imeandikwa alipo Askofu, Kanisa lipo!
 
Moja wapo ya sifa ya dini ni Universality. Sasa dini Ipo kwa Wapare, wajita , wakerewe na wajaluo tuu , hiyo ni prima facie evidence kuwa Kuna tatizo. Wao waendelee kucheza maparedi Yao kwenye makanisa Yao na kuzishika amri za kale za kiyahudi ambazo kimsingi ni Mila zaidi zilizopo kwenye agano la kale ambazo Yesu alizi ove rule Haina shida lakini wasiumize kichwa kwa Imani isiyowahusu
Wasichokijua, mtume Paulo anasema, "Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya".

Yale yale ya kuiabudu sabato badala ya Bwana wa Sabato.
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Kanisa Katoliki huwaga halina muda mchafu kama huo! Yaani ukahangaike kujibizana na mataahira wanaomwabudu Ellen G. White?
 
Back
Top Bottom