DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Unaweza ukawa na mada nzuri yenye motivation ila uwasilishaji wako ukaspoil mada yote....Please uzi huu naomba ukae jukwaani angalau kwa mwaka mmoja . Vijana wanalia njaa huku wamezungukwa na vyakula, waamke wale.
Hili ndilo hitimisho langu na ndio ukweli wenyewe.
Najua maskini watanijia juu wakitamani kuniua kwa kuwaambia ukweli.
Lengo sio kuwaumiza mioyo , lengo ni kuwaamsha. Tokeni usingizini mkapate mali.
Sizungumzii kuwa matajiri, nazungumzia ustawi wa maisha ya kawaida. Kumiliki Nyumba, biashara, gari au hata shamba.
Nchi hii yenye hifadhi za wanyama nyingi, mapori tengefu mengi, bahari imelala kutoka Kaskazini Mashariki mpaka kusini Mashariki mwa nchi, misitu mingi, ardhi yenye rutuba haina hesabu.
Ina maana shetani amefunga akili zako usiione fursa angalau moja kati ya mamilioni ya fursa?
Unasubiri serikali ikupeleke kwa nguvu Makete ukalime Viazi?
Unasubiri serikali ikupeleke kwa nguvu kwenye migodi na mialo ya dhahabu ukachimbe?
Kama huna ustawi katika maisha yako jua tu kuwa shetani ameharibu akili zako kwa ufupi amekufanya usiwe na akili timamu.
Amka.
Wengine watasema tatizo mtaji. Serious?
Nimeona watu wengi sasa wana pesa, mtaji wao wa kwanza ulikuwa nguvu na uthubutu.
Nenda kwenye migodi, mtaji wako ni nguvu tu, acha ulevi na uzinzi utafanikiwa.
Umezungumzia Nchi kuwa na hifadhi za wanyama na hifadhi tengefu...
Unataka wazifanyie nini wakati Hifadhini Raia Hawaruhusiwi? We unaishi wapi? Hata kuwinda panya tu Serengeti ni kosa linaloweza kukufunga Miaka 100 jela...
Unazungumzia kuhusu Mashamba yenye Rutuba? Asilimia 100 ya mashamba hayo ni mali ya Serikali, ulitaka vijana wakayachukue ili waingie Mgogoro na Serikali (Bado hatujasahau yule mtu aliouziwa pori tengefu)..
Unazungumzia kilimo cha Viazi Makete....
Unajua Kijana alioko Dar mpaka Makete nauli ni Bei gani?
Unajua Mbegu za viazi ni kiasi gani?
Unajua kukodi shamba ni kiasi gani?
Unajua mbolea na pembejeo nyingine ni kiasi gani?
Unajua kutafuta Labour wa kupalillia na kutunza hayo mashamba ni kiasi gani?
Unasema watu waende Migodini umewahi kufanikiwa kwenda Migodini?
Au ni story ulizosimuliwa mtaani?..
WAKATI MWINGINE SHIRIKISHA AKILI KABLA YA KUANDIKA MADA AMBAYO WEWE MWENYEW U AIONA NI 🚮🚮🚮