Ukweli mchungu: Kama unaishi Tanzania halafu wewe ni maskini huna akili timamu

Huu uzi kaandika chief Godlove[emoji3][emoji3]
 
Ningekuwa kaka yake ninafukuza kabisa
Akili yako ni ndogo kijana soma mada ulioandikwa alafu jibu Kwa kutulia usisupport kila kitu sababu kimewekwa kuegemea upande fulani, panua ubongo
 
Tumia watu wakufanyie kazi; hapa natafuta vijana 5000 nchi nzima wawe wanatembeza kahawa iliyopikwa kwenye birika, hasa hiki kipindi cha mvua na baridi; yeyote mwenye sifa, tuma maombi upate ajira.​
 
Please uzi huu naomba ukae jukwaani angalau kwa mwaka mmoja . Vijana wanalia njaa huku wamezungukwa na vyakula, waamke wale.

Hili ndilo hitimisho langu na ndio ukweli wenyewe.

Najua maskini watanijia juu wakitamani kuniua kwa kuwaambia ukweli.

Lengo sio kuwaumiza mioyo , lengo ni kuwaamsha. Tokeni usingizini mkapate mali.

Sizungumzii kuwa matajiri, nazungumzia ustawi wa maisha ya kawaida. Kumiliki Nyumba, biashara, gari au hata shamba.

Nchi hii yenye hifadhi za wanyama nyingi, mapori tengefu mengi, bahari imelala kutoka Kaskazini Mashariki mpaka kusini Mashariki mwa nchi, misitu mingi, ardhi yenye rutuba haina hesabu.

Ina maana shetani amefunga akili zako usiione fursa angalau moja kati ya mamilioni ya fursa?
Unasubiri serikali ikupeleke kwa nguvu Makete ukalime Viazi?

Unasubiri serikali ikupeleke kwa nguvu kwenye migodi na mialo ya dhahabu ukachimbe?

Kama huna ustawi katika maisha yako jua tu kuwa shetani ameharibu akili zako kwa ufupi amekufanya usiwe na akili timamu.

Amka.
Wengine watasema tatizo mtaji. Serious?

Nimeona watu wengi sasa wana pesa, mtaji wao wa kwanza ulikuwa nguvu na uthubutu.
Nenda kwenye migodi, mtaji wako ni nguvu tu, acha ulevi na uzinzi utafanikiwa.
Hapo utakuta una tumilioni ishirini kwa akaunti , asubuhi umekunywa tusupu twa makongoro basi unajiona bosi .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Nchi hii yenye hifadhi za wanyama nyingi, mapori tengefu mengi, bahari imelala kutoka Kaskazini Mashariki mpaka kusini Mashariki mwa nchi, misitu mingi, ardhi yenye rutuba haina hesabu.
Umesoma alichokiandika hapa huyu zwazwa? Hicho ndicho nilichochukia mtu anakaa anaandika vitu hata havielewi ili kupata attention ni ujinga, sasa ukimwambia aifafanue hio aya ataishia kutoa tu mimacho
 
Ningekuwa kaka yake ninafukuza kabisa
Wakat nasoma kipindi kile miaka ya 2000 Hela ilikuwa ngumu balaa kuipata,nilipiga sana vibarua mashambani na kubeba zege kwenye majengo yaliyokuwa yakijengwa na jkt! Sikumbuki km baba amenilipia ada mara ngap o level.. Godoro nimelijua nilipoenda form five!

Nilivyomaliza chuo nikarudia kijjn kwa bibi ,sikuwa na pesa ila maeneo yalikuwepo ,nikasema ngoja nishike jembe nikaandaa shamba nikaenda Kwa jirani kuomba mbolea! Niliwastaajabisha watu jinsi nilivyovuma mahindi,njugu,karanga!

Kijana analalamika mtaji Hana wakat anamiliki Sumsang Galaxy kali na anayo PC anatumia kuchekia Porno tu!
 
Nimeamua kusoma wadau wamejibu Nini kabla sijaamua kusoma huu Uzi.
 
Wakat nasoma kipindi kile miaka ya 2000 Hela ilikuwa ngumu balaa kuipata,nilipiga sana vibarua mashambani na kubeba zege kwenye majengo yaliyokuwa yakijengwa na jkt! Sikumbuki km baba amenilipia ada mara ngap o level.. Godoro nimelijua nilipoenda form five!

Nilivyomaliza chuo nikarudia kijjn kwa bibi ,sikuwa na pesa ila maeneo yalikuwepo ,nikasema ngoja nishike jembe nikaandaa shamba nikaenda Kwa jirani kuomba mbolea! Niliwastaajabisha watu jinsi nilivyovuma mahindi,njugu,karanga!

Kijana analalamika mtaji Hana wakat anamiliki Sumsang Galaxy kali na anayo PC anatumia kuchekia Porno tu!
Ni hatari nchi hii. Hiyo simu ni sawa na shamba eka mbili pale Kisarawe.

Hiyo PC ni mtaji wa kupandia mihogo heka mbili
 
Wakat nasoma kipindi kile miaka ya 2000 Hela ilikuwa ngumu balaa kuipata,nilipiga sana vibarua mashambani na kubeba zege kwenye majengo yaliyokuwa yakijengwa na jkt! Sikumbuki km baba amenilipia ada mara ngap o level.. Godoro nimelijua nilipoenda form five!

Nilivyomaliza chuo nikarudia kijjn kwa bibi ,sikuwa na pesa ila maeneo yalikuwepo ,nikasema ngoja nishike jembe nikaandaa shamba nikaenda Kwa jirani kuomba mbolea! Niliwastaajabisha watu jinsi nilivyovuma mahindi,njugu,karanga!

Kijana analalamika mtaji Hana wakat anamiliki Sumsang Galaxy kali na anayo PC anatumia kuchekia Porno tu!
Kwa hio hadithi yako inakifundisha nini? Unajua kuna watu wakikuwekea story zao unajua unaweza ukaishia kukenua tu mdomo, watu wanahustle watu wanapambana nini kubeba zege sijui kulima na uchafu gani kwa Bibi yako mamaezako ushawahi kufanya kazi masaa 18/19 bila kupumzika mwezi mzima hadi unahisi kufakufa? Kazi ambayo ukipewa wewe huvuki siku 3 una-float unaumwa mafua km kuku mwenye mdondo
 
Back
Top Bottom