Ukweli mchungu: Kikwete family ni Royal Family watatutawala milele

Subiri utaelewa Tu ni suala la muda Tu
 
Safi sana 👍 nafurahi nikimuona mtu anajiamini kama wewe ! Wanasemaga As you think so shall you be !! All the best and good luck !!
 
Waliteleza kidogo wakamkabidhi nchi JPM, cha moto walikiona ila hawatakaa wafanye tena kosa walilolifanya kumpa JPM nchi. Ndio maana wanawaandaa watoto wao kwenye nafasi za uwaziri ndio mapresident wajao.
Na mwamba yule angetusua,hizo falme zote angezisambaratisha

Ova
 
Hii si sawa! Sema bila malecela Nape angalikuwa anaendesha Bodaboda
Bila JK, Nape angekuwa anaendesha bodaboda.
Usisahau Nape alinyimwa hata sponsorship katika chuo cha diplomasia wakati JK akiwa ni Waziri wa Foreign Affairs, pale alipoambiwa asigombee uenyekiti wa UVCCM amwachie Nchimbi. Aliyesevu ngoma ni malecella. Ladwa ndiye alitoa fedha. Nape bisha
 
Acha nchi iliwe watuachie mifupa na miba tufyonze.
 
Mkuu somesha watoto na wajukuu acha kulalama na kulia wivu, ndio suluhisho la kumkomboa mtu kutoka katika umaskini.
Kusomesha sio kuelimisha.
Maana ya/lengo la elimu sio kutajirisha.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kutoka kwenye umasikini na kuwa tajiri kupindukia.
Viongozi wa Tanzania hawajafika hapo kwa kusoma sana na kuelimika.
Viongozi wa Tanzania hawatumii elimu yao katika kujikomboa kutoka umasikini,bali katika kujilimbikizia utajiri kwa njia zisizo halali.
Lengo la uongozi si kujikomboa kutoka katika umasikini. Lengo la uongozi ni kuwaletea watu maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…