Ukweli mchungu: Maombi ya kujionesha, hata kama ni ya siku tisa (Novena), Mungu hayasikii

Kwahyo wewe ulitaka wafanyaje?
 
Soma Biblia kwa muktadha:
Yesu alipokuwa anaondoka mjini Yeriko...vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu anapitia hapo, walipaza sauti....

Yesu amekuambia leo kwamba atapita JF? If not, kwanini unapaza sauti ya sala yako hapa kama sio kujionesha?
 
Kipi kinakuwasha!? Kichwa au tundu la haja kubwa!?
Duh, na wewe unahitimisha Novena huku ulimi wako unanena yaliyopotoka? Hujui kwamba Mungu hawasikii wenye dhambi? Soma Yn 9:31
 
Acha dhihaka Binti utakufa vibaya

Tubu utasamehewa..acha dhihaka kwa watu wa Mungu.
 
Kuna muda hunaga hoja basi tu kujaza server
Mwanangu, pinga hizo hoja kwa hoja.
By the way, nani alikuambia server zinajaa? Inaonekana bado unaishi stone age. Siku hizi kuna mpaka cloud servers 😎
 
Acha dhihaka Binti utakufa vibaya

Tubu utasamehewa..acha dhihaka kwa watu wa Mungu.
Watu wa Mungu wanatenda aliyosema Mungu. Mungu amesema usijioneshe barabarani kuwa unasali, wewe unampinga Mungu na kujionesha mpaka mitandaoni, halafu unadai u mtu wa Mungu?
Lk 6:46-49
"Kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, lakini hamtendi nisemayo?"
 
Ikiwa ndio hivyo basi ninyi walokole mpo mbali sana na Mungu kwa sababu Ibada zenu ndizo zimejaa maonesho mengi na maspika ya kelele mitaani.
 
Ikiwa ndio hivyo basi ninyi walokole mpo mbali sana na Mungu kwa sababu Ibada zenu ndizo zimejaa maonesho mengi na maspika ya kelele mitaani.
Mada hii haibagui mtu wala dini yake. Inawahusu watu wote, hata walokole. Na wao wakiomba kwa kujionesha, maombi yao hayafiki kwa Mungu. Period
 
Mada hii haibagui mtu wala dini yake. Hata kama ni mlokole akiomba kwa kujionesha, maombi yake hayafiki kwa Mungu
Ndio hualisia wenu walokole lakini mnaona mkiwaponda RC mtapata mileage.
Ibada zenu za kilokole zimejaa unafiki mwingi na makelele.
Mnafiki wewe! Wewe ni nani mpaka umapangie Mungu mwenye nguvu maombi Gani ampokee!

Mathayo 7:1–5
1 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
2 Kwa maana kwa hukumu hiyo mhukumuyo, ninyi pia mtahukumiwa; na kipimo kilekile mtakachopimia, ndicho mtakachopimiwa.
3 Mbona waona kibanzi kilicho katika jicho la nduguyo, lakini huoni boriti lililo katika jicho lako mwenyewe?
4 Au wawezaje kumwambia nduguyo, 'Niruhusu nitoe kibanzi kilicho jichoni mwako', na tazama, boriti liko katika jicho lako?
5 Mnafiki! Toa kwanza boriti lililo katika jicho lako, ndipo utaona sawasawa kulitoa kibanzi kilicho katika jicho la nduguyo.
 
Mada hii haibagui mtu wala dini yake. Inawahusu watu wote, hata walokole. Na wao wakiomba kwa kujionesha, maombi yao hayafiki kwa Mungu. Period
Mungu anangalia dhamira ya mtu.Kujionyesha au kujificha hakuna maana yoyote kwa Mungu.Kama kusudi la ombi lako ni baya ata ungeomba wazi au kujificha hakuna maana.Ndio maana wanasema bwana utazama moyo(unaweza ficha kila mtu lakini huwezi kumficha Mungu)
 
HAKIKA
 
Aisee. Na je vipi wale wanaoweka spika(megaphone) nje ya masinagogi yao na kuomba kwa sauti kubwa hadi mtaa wa nne wanasikia, wanajionyesha?
Maswali madogo madogo naomba uwe unamuuliza chatGPT, anajibu kwa haraka sana; 🙂 mimi niulize maswali mazito mazito tu; au sio mkuu.
 
Hayo ni mawazo yako tu. Kwani wewe ndiye Mungu unayeyajibu, au unaongea kwa niaba yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…