Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Cheo cha Mkuu wa Nchi ni Cha Kimamlaka, Sikumbuki ni Lini mara ya Mwisho nimevutiwa kusikiliza au kujua Mkuu wa Nchi anahutubia Taifa Letu Takatifu, Bi mkubwa amekuwa too soft afu pia vibaraka Wanaomzunguka wanazidi kumuingiza Chaka tu ili nao wapate pakuanzia, Wengi hawana nia ya Kumuona akifanikiwa kwa sababu nao wanataka kiti chake

Majority ni hao Cabinet secretaries wengi wanataka kiti kikuu afumue aweke Wasaidizi na sio washindani

The Late President wa Kenya Moi aliwahi Kusema The presidency is a jealous Institution
 
Sisi Watumishi wa Umma tunamuelewa saana, madaraja, mishahara, OC zilizoshiba.

Mi shabiki wa Chadema ila Maza namuelewa sana anaganga majeraha ya mtangulizi wake
 
Kwahiyo jamaa hawatoboi si kwamba hawapigiwi kura za kutosha bali wanadhoofishwa na system?.Hivi majuzi nae omary mapuri(kada wa ccm) amepewa teuzi huko kwenye system za uchaguzi.
 
Mikopo kwa akina mama alisitisha kitambo tu! Na hata kama atakuwa ameirejesha kinya kimya, bado utokaji wake umejaa urasimu wa kutisha.

Wamama mtaani wanahangaika na mikopo ya vicoba, na pia ile ya moto kutoka Loan sharks! Kwa hiyo nilichokisema kina ukweli ndani yake.
 
Tena aki na mama ndo hawampendi kabisa. Kuna mama mmoja anasikiliza radio one sasa kuna muda wanaweka ujumbe wa Samia Suluhu Hassan utasikia wamama wanakwambia mwenzao "zima kwanza/toatoatoa.../we punguza sauti kwanza/
Hii ni kweli,Mimi naishi Mwanza,Wamama hawampendi Samia!
 
Wanaomchukia Rais SSH ni wale waliozoea zile bata za awamu ya tano. Wale waliokuwa wanaongea lugha yao ya asili katika vikao vya halmashauri hapa nchini.

Walizoea kujiona wao ndio watawala wa milele kwa kutegemea wingi wa watu wa kabila lao. Kifo cha kabla cha mpendwa JPM kikawafanya wakaanza kujihisi kama yatima aliyepoteza wazazi wote wawili.

Hizi nongwa zote wanazoendeleza sababu ni kuhisi mirija yao kukatwa. Na Samia amekua akitumia akili sana kuhakikisha daraja la busisi linamalizika kwa wakati na amezianzisha siasa za uchifu huko kanda ya ziwa makusudi kabisa ili kuwaonyesha hao waungwana kwamba hawajapoteza kila kitu.

Ni aina fulani ya kuwapa faraja hivyo hizi nongwa zote zinazoendelea chanzo chake ni hiyo vita ya siri inayoanzia kwa wale wafuasi wa hayati JPM.

Wanatamani sana wamlaumu Mungu lakini mioyo yao inafahamu kuwa hiyo ni dhambi kubwa.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kupendwa na kuwa na wasiwasi naye.

SSH anapendwa ila watu wana wasiwasi kuwa anaingizwa Mkenge. Yeye ni bendera fata upepo. Mamlaka yanaonekana pale ambapo unakaa kwenye nafasi yako kwa uimara na uthabiti.
Nini kinafanya apendwe ni aina ya uongozi wake au anapendwa tu yeye kama yeye kama ilivyo kwa Kikwete?
 
Usimuamshe aliyelala
 
Tena aki na mama ndo hawampendi kabisa. Kuna mama mmoja anasikiliza radio one sasa kuna muda wanaweka ujumbe wa Samia Suluhu Hassan utasikia wamama wanakwambia mwenzao "zima kwanza/toatoatoa.../we punguza sauti kwanza/
Weeeeeee !!!
 
Iko mimama huwa inajitesa yenyewe na sijui hats huwa na akili gani ? Vicoba imekuwa kama lifestyle yao unakuta anacheza vikoba kwa miaka 20 mfululizo Nyumba hana gari hana kula ya shida kila Sikh mbiombio😁😁😁
 
I say what I say
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…