UKWELI MCHUNGU: Wazazi wengi hawana upendo wa kweli

Wengi kwa maana gani? Nusu, robo, robo tatu au asilimia ngapi?
 
Hadi nimeandika najua nnachokiandika.

Ikatokea hapa leo kila mtoto akamrudishia mzazi wake maumivu alompatia jamii hii hii ndo ya kwanza kunyoosha kidole.

Mfano mzazi wako anakuumiza hadi unashindwa kuelezea we utamfanya nini?? Utampiga? Utamuua? Naandika nnachokijua mkuu. Kuna mzazi anatesa hadi unatamani Biblia ingeweka na kipengele cha kukutetea wewe mtoto. Ila ndo hivyo.
 
Mtoto mwenye kipato akifariki utasikia mama analia MUNGU UMENIWEZAAAA KWA NINI UMEMCHUKUA JIMMY,MBONA UMENIKOMOA MIMI.....,sasa wengine inabidi mstop kulia muangaliane sasa huyu mama alitaka achukuliwe nani?
[emoji2][emoji2][emoji1787][emoji1787][emoji2957]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Na watoto wakigundua tabia za namna hii Kwa wazazi upendo wao Kwa mzazi unapungua. Pia wao wanapunguza kupendana na kushirikiana.
Wanaishi kinafiki nafiki. Kisa walizaliwa tumbo moja.
Hii ni kweli kabisa
 
Upo sahihi kuna mama jiran huyo ni hatari anaemtumia pesa ndo.mtoto asiempa pesa kila siku anamuombea mabaya na kusema sio mwanae
 
Kinachonishangaza, unakuta mzazi alishindwa maisha,akakuzaa kwenye umaskini,alafu anakulaumu eti huna pesa, wakati yy alishindwa kama unavyoshindwa! Wazazi wengi hawana Upendo kweli
 
Mwenye upendo wa kweli ni mama mzazi hawezi kukuacha hata nyakati za tabu. Waliobaki upendo wao utegemea wananufaika vipi kwako.
 
Kinachonishangaza, unakuta mzazi alishindwa maisha,akakuzaa kwenye umaskini,alafu anakulaumu eti huna pesa, wakati yy alishindwa kama unavyoshindwa! Wazazi wengi hawana Upendo kweli
Ambao wamezikuta hawawezi kukuelewa.
 
Anaeweza elewa mada kama hizi nj mtu aliyepitia haya, na hata hua ukifanikiwa ukisema unamsaidia huyo mzazi unafanya tu kwa ajili unatafta radhi za mola.wako lkn kama sivyo hushighuliki nae.kwa lolote. Uzi huu umenikumbusha maisha yangu, yan wengin hata uumwe ufe kwake anaona sawa tu lkn.mwanae mwingine akiugua anafanya kupata wazimu.
Niliwahi kuomba pesa ya matumizi nikiwa chuo baada ya bibi kushindwa kunisaidia pesa ya chakula alichonijibu mama yangu " kwa sasa sina pesa ya kukupa kwani nimeagiza gari nashughulika na mambo makubwa " imagine kwa wakti ule nilitamani anipe hata 5000 niweze kula kwenye mikoa ya watu lkn hayo ndo yalikua majibu yake.ki ukwel watu wakisema nani kama mama mimi najisemea hakuna kama bibi. mungu atusaidie
 

Mimi huwa nawashangaa watu wanaowatukuza na kuwaabudu mama zao eti hakuna kama mama(Mungu je?) Hawajui kwamba hiyo ni kutokana na ubinafsi wa wao ili watoto wasahau na kuwadharau Baba zao. Nachoamini Mimi wazazi wote ni Sawa,Ila,ukiingia kwenye kumi nane ya mwanamke (mama) utaniona hii dunia chungu, yaani watu hawajui tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…